• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 30-Juni5 )

    (GMT+08:00) 2020-06-12 18:06:55
    Wakenya kuchangia ufadhili wa bajeti ya mwaka 2020/21

    Huku Wakenya wengi wakiendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha baada ya kupoteza ajira kutokana na janga la virusi vya corona, huenda wakakabiliwa na changamoto nyingine ya kupanda kwa bei ya bidhaa za kimsingi na kodi ya nyumba.

    Hii ni kutokana na hatua ya serikali kupendekeza kuongeza ushuru unaotozwa bidhaa za matumizi ya nyumbani, kama vile chakula na gesi ya kupikia, kulingana na Mswada wa Fedha wa 2020.

    Vile vile, gharama ya uzalishaji chakula itapanda baada ya serikali kupendekeza ushuru wa thamani (VAT), wa kiasi cha asilimia 14 kwa vifaa vya kilimo, kama vile trekta.

    Japo hizi ni baadhi ya mbinu ambazo serikali inapanga kutumia kuiwezesha kupata fedha za kutekeleza Bajeti ya Sh2.7 trilioni iliyosomwa Alhamisi na Waziri wa Fedha Ukur Yatani, zinahujumu mipango yake chini ya Ajenda Nne Kuu za Maendeleo.

    Kulingana na bajeti hiyo ambayo ilisomwa bungeni Alhamisi, serikali inatarajiwa kukusanya Sh1.62 trilioni kutokana na ushuru lakini itatumia Sh904 bilioni kulipia madeni.

    Na kwa kuwa serikali inapanga kutumia Sh1.8 trilioni kufadhili matumizi yake, hii ina maana kuwa kuna upungufu wa Sh600 bilioni katika bajeti hii.

    Ushuru wa VAT unaopendekezwa kutozwa bidhaa za kimsingi kama vile mahindi, unga wa ngano, maziwa na mayai na vyakula vinginevyo utapandisha bei ya bidhaa hizo wakati huu mgumu. Wakati huu bidhaa hizi hazitozwi ushuru huo. Kifupi hali ni hiviā€¦

    1: Vyakula kama unga, maziwa na mkate kutozwa ushuru wa thamani wa asilimia 14

    2: Gesi ya kupikia kutozwa VAT ya asilimia 14

    3: Trekta na vifaa vingine vya kilimo kutozwa VAT ya asilimia 14

    4: Ushuru wa mapato ya nyumba wapandishwa kutoka asilimia 10

    5: Akiba ya kununua nyumba kutozwa ushuru

    6: Wazee kulipa ushuru wa asilimia 25 kwa pensheni

    7: Wafanyabiashara mitandaoni kulipa ushuru wa asilimia 1.5 kwa mapato yao.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako