• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 30-Juni5 )

    (GMT+08:00) 2020-06-12 18:06:55

    Mkuu wa majeshi aomba msamaha kwa kuenda kanisani na Trump.

    Mkuu wamajeshi nchini Marekani amekiri kuwa alikosea kuungana na Rais Donald Trump wakati alipotembea kuenda kanisa lililopo karibu na Ikulu ya Marekani ambalo liliharibiwa na waandamanaji.

    Kwa mujibu wa Jenerali Mark Milley, tukio hilo la Juni tarehe moja na ambalo lilizua utata lilionesha taswira kwamba jeshi linajihusisha na siasa za ndani ya nchi.

    Bwana Trump alitembea hadi kwenye kanisa hilo na kupiga picha akiwa ameshikilia Bibilia baada ya maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd, kuvunjwa kwa nguvu.

    Mkuu huyo wa majeshi anasema kwamba hakustahili kuwa hapo, na kusisitiza kwamba uwepo wake hapo wakati wa tukio hilo ulionyesha taswira kwamba majeshi yanajihusisha na siasa za ndani ya nchi. Bwana Milley alikiri kwenye video kwamba alifanya makosa na kuwa amepata funzo kutokana na tukio hilo.

    Pia alisema kuwa alighadhabishwa na mauaji ya "kinyama" ya George Floyd. Aliongeza kwamba maandamano yaliyofuatia hayakuangazia mauaji hayo tu, bali pia yaligusia vitendo visivyokuwa vya haki vilivyotendewa Wamarekani weusi kwa karne kadhaa

    Jenerali huyo alikuwa amevalia sare za kijeshi wakati alipotembea pamoja kuenda katika kanisa hilo na wakosoaji wanasema hatua hiyo iliashiria anaunga mkono utumizi wa wanajeshi dhidi ya waandamanaji.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako