• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 20-Juni26 )

    (GMT+08:00) 2020-06-26 16:07:41

    Kenya yawataka wenye virusi vya COVID-19 kutibiwa nyumbani ili hospitali zisizidiwe uwezo

    Kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa COVID-19 wasio na dalili, Kenya imeanza kutekeleza utaratibu wa kutaka watu hao watibiwe nyumbani ili mfumo wa afya wa nchi hiyo usizidiwe uwezo.

    Utaratibu wa wagonjwa kutibiwa nyumbani utafanya wagonjwa hao hasa katika miji ya Nairobi na Mombasa kutibiwa nyumbani. Kufuatwa kwa utaratibu huo kunaifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza kwenye eneo hilo kufuata utaratibu huo, wakati idadi ya maambukizi ikiendelea kuongezeka.

    Katibu mkuu tawala wa wizara ya afya ya Kenya Bibi Mary Mwangangi amesema asilimia 78 wa wagonjwa hawana dalili au wana dalili ndogo, hali inayowezesha utekelezaji wa kuwapatia matibabu wakiwa nyumbani, kwa kuwa wanaweza kupatiwa matibabu hayo vizuri wakiwa nyumbani. Amesema kwa sasa haiwezekani tena kwa miji ya Nairobi na Mombasa, ambayo inabeba mzigo mkubwa, kuwatenga wagonjwa katika hospitali.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako