• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 20-Juni26 )

    (GMT+08:00) 2020-06-26 16:07:41

    Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zafikiria kuwa na mkakati wa pamoja kuhimiza utalii baada ya COVID-19

    Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zinapanga kutelekeza mikakati ya pamoja kuhimiza ufufuaji wa sekta ya utalii baada ya sekta hiyo kuporomoka kwa miezi kadhaa kutokana maambukizi ya virusi vya Corona.

    Naibu katibu mkuu wa sekta za uzalishaji na kijamii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Christopher Bazivamo, amesema jumuiya inawasiliana na serikali zote na sekta ya utalii ili kufanikisha utekelezaji wa hatua za pamoja kwenye kufufua sekta ya utalii. Amesema kwa sasa wanaoanisha sera na mikakati ya kuinua sekta ya utalii iliyokwama tangu mwezi Machi kutokana na nchi za kanda hiyo kuzuia usafiri na kufuta safari za ndege ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

    Amesema nchi za Afrika mashariki zinatarajia kuwa, hadi kufikia mwezi Julai kutakuwa na kupungua kwa asilimia 60 kwa watalii wanaoingia kwenye eneo hilo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako