• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 26-Oktoba 2)

    (GMT+08:00) 2020-10-02 15:29:36
    TIMOITHY RAY BROWN: ALIYEKUWA MTU WA KWANZA KUTIBIWA HIV AMEFARIKI .

    Mtu wa kwanza kutibiwa virusi vya ukimwi HIV - Timothy Ray Brown amefariki kutokana na saratani. Bwana Brown ambaye pia alijulikana kama mgonjwa wa Berlin alipandikizwa uboho kutoka kwa mtu ambaye alikuwa na kinga dhidi ya HIV 2017.

    Hii ilimaanisha kwamba alikuwa anahitaji tena dawa za kukabiliana na virusi vya ukimwi, hivyo basi alisalia bila maambukizi yoyote ya virusi hivyo vinavyosababisha ukimwi kwa maisha yake yote.

    Shirika la kimataifa kuhusu wagonjwa wa ukimwi duniani limesema kwamba bwana Brown aliupatia ulimwengu matumaini kwamba dawa ya kutibu ukimwi inaweza kupatikana.

    Bwana Brown mwenye umri wa miaka 54, ambaye alizaliwa nchini Marekani , alipatikana na virusi vya HIV alipokuwa akiishi Berlin 1995.

    Na baadaye mwaka 2007 alipata saratani ya damu kwa jina Myeloid Leukemia. Tiba yake ilianza kuharibu uboho wake ambao ulikuwa ukizalisha seli hizo za saratani kabla ya kufanyia upandikizaji.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako