• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 26-Oktoba 2)

    (GMT+08:00) 2020-10-02 15:29:36
    Magawa: Mfahamu Panya kutoka Tanzania anayeweza kugundua mabomu yaliotegwa ardhini duniani.

    Panya mkubwa kutoka Afrika amepewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini. Magawa ameweza kunusa mabomu 39 na silaha 28 ambazo hazijalipuka katika maisha yake.

    Shirika la matibabu ya wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA limemtuza medali ya dhahabu "kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia".

    Inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu milioni sita ya kutegwa ardhini katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia. Nishani ya dhahabu ya PDSA, imeandikwa maneno "Kwa juhudi za wanyama au kujitolea kazini ".

    Kwa wanyama 30 waliopewa tuzo hiyo, huyu ni panya wa kwanza. Panya huyo aliye na miaka saba alipewa mafunzo na shirika lisilo la kiserikali- Apopo kutoka Ubelgiji lenye makao yake nchini Tanzania. Shirika hilo limekuwa likiwalea wanyama wanaofahamika kama - PanyaShujaa- kugundua uwepo wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu miaka ya 1990.

    Wanyama hao wanafuzu baada ya kuwapa mafundisho.

    Kulingana na Apopo, Magawa - aliyezaliwa na kulelewa Tanzania - akiwa na uzani wa kilo 1.2 (2.6lb) na urefu wa senti mita 70 (28in) .

    Japo ni mkubwa kuliko spishi zingine za panya, Magawa ni mdogo ni mwepesi kiasi kwamba hawezi kulipua mabomu akitembea juu.

    Panya hao wanafundishwa kubaini kemikali iliyotumiwa katika vilipuzi, kumaanisha wanaweza kupuuza vyma vikuukuu na kutafuta mabomu kwa haraka zaidi. Wanapopata kilipuzi wanakuna juu yake na kuwaonesha binadamu wafanyakazi wenzao.

    Magawa ana uwezo wa kusaka mabomu katika eneo lenye ukubwa wa uwanja wa mpira wa tennis kwa muda wa dakika 20 - jambo ambalo Apopo linasema itamchukua mtu aliye na kifaa cha kubaini vifaa vya chuma kati ya siku moja hadi nne. Panya huyo anafanya kazi kwa saa moja na nusu kwa siku nyakati za asubuhi na anakaribia kustaafu.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako