• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 3-Oktoba 9)

    (GMT+08:00) 2020-10-09 16:08:35

    Papa Francis: Ubepari wa soko umeshindwa, udugu wa kibinadamu ni muhimu baada ya janga la COVID-19

    Papa Francis amesema janga la virusi vya Corona limethibitisha kuwa "nadharia za kufikirika" za ubepari wa soko zimeshindwa na dunia inahitaji aina mpya ya siasa inayohimiza mazungumzo na mshikamano, na inapinga vita kwa gharama zote.

    Jana jumapili, Papa Francis alizungumzia maoni yake kuhusu dunia baada ya kumalizika kwa COVID-19, na ametoa wito kwa viongozi wa nchi mbalimbali duniani pamoja na watunga sera wa kimataifa na kiuchumi duniani, kufanya kazi kwa bidii kueneza utamaduni wa kuvumiliana na kuishi pamoja kwa amani, kuingilia kati mapema vita inapotokea ili kuepusha umwagaji damu wa watu wasio na hatia, migogoro, uharibifu wa mazingira na maadili, na kushuka kwa tamaduni, mambo ambayo ulimwengu wa sasa unayashuhudia.

    Aliongeza kuwa, mizozo mikubwa ya kisiasa, ukosefu wa haki na usambazaji sawa wa rasilimali za asili imetokea na inaendelea kujitokeza, hivyo kusababisha balaa kubwa lililoziathiri nchi mbalimbali, licha ya maliasili zao na utaalamu wa vijana ambao ni sifa kwa nchi hizo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako