• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 3-Oktoba 9)

    (GMT+08:00) 2020-10-09 16:08:35

    BOT yasema uchumi wa Tanzania unaendelea vizuri licha ya athari za COVID-19

    Benki Kuu ya Tanzania BOT imesema uchumi wa nchi hiyo unaendelea kufanya vizuri licha ya athari kubwa za kiuchumi kuenea ulimwenguni kutokana na janga la COVID-19.

    Kwenye taarifa yake BOT imesema tathmini ya utendaji na mtazamo wa uchumi iliyofanywa na kamati yake ya sera ya fedha imeonyesha kuwa uchumi utakua kwa makadirio ya asilimia 5.5 mwaka 2020. Aidha mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 3.3 kutoka mwezi Julai hadi Agosti mwaka huu, na utakuwepo kati ya asilimia 3 na 5 katika mwaka wa fedha wa 2020/21 kama ilivyokadiriwa awali.

    Mbali na hapo taarifa imesema ukuaji wa mikopo kwenye sekta binafsi ni mkubwa na kuweza kuhimili changamoto za mnyororo wa usambazaji duniani zinazotokana na janga la COVID-19.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako