• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 17-Oktoba 23)

    (GMT+08:00) 2020-10-23 15:45:42

    Maandamano ya Sars Nigeria: Ghasia zaibuka Lagos baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji

    Majengo yamechomwa moto na kumeripotiwa kwa milio ya risasi katika miji mikubwa ya Nigeria wakati wa maandamano.

    Shirika la kimataifa la Amnesty limesema watu wapatao 12 waliuawa na polisi na wanajeshi siku ya Jumannne.

    Jeshi la Nigeria limekanusha ripoti hiyo na kudai kuwa ya uongo,waliandika katika kurasa ya Twitter.

    Mamlaka iliweka amri ya kutotoka nje lakini baadhi walipuuzia agizo hilo.

    Waandamanaji dhidi ya polisi wamekuwa barabarani kwa kipindi cha wiki mbili sasa.

    Waandamanaji wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha kampeni yao dhidi ya kikosi maalum cha polisi kinachojulikana kama Sars.

    Rais Muhammadu Buhari alikisitisha kikosi hicho Oktoba 11. Lakini waandamanaji wameendelea na maandamano wakitaka mabadiliko zaidi katika vikosi vya usalama, pamoja na kubadilisha utendaji wao wa kazi.

    Watu walioshuhudia milio ya risasi wameiambia BBC kuwa waliwaona jinsi polisi walivyokuwa wanamimina risasi Jumanne jioni.

    Baadhi ya majengo yalichomwa moto mjini Lagos na polisi waliweka zuio barabarani.

    Kituo cha Televisheni Nigeria chenye uhusiano na chama tawala kilichomwa moto.

    Walioshuhudia wanasema watu wasiokuwa na sare walipiga risasi kwenye mkusanyiko wa waandamanji wapatao 1,000.

    Rais Buhari hakuzungumzia kufyatuliwa kwa risasi ila amewataka watu wawe watulivu na wavumilivu na waelewa wakati jitihada za mabadiliko zikiwa zinafanyika.

    Maandamano yamefanyika Uingereza, Afrika Kusini na Kenya dhidi ya polisi wakatili Nigeria,wakati maafisa katika maeneo hayo wakilaani matukio hayo.

    Aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni nchini Marekani Hillary Clinton amemtaka rais Buhari na jeshi kuacha kuwaua vijana wanaoandamana wa vuguvugu la #EndSARS ".

    Na aliyekuwa makamu wa rais nchini Marekani ambaye ndio mpinzani mkuu wa rais Donald Trump katika uchaguzi wa mwezi ujao Joe Biden - pia ametoa wito kwa mamlaka kusitisha ghasia dhidi ya waandamanaji.

    Na anayewania urais Marekani Joe Biden ameitaka mamlaka ya Nigeria kusitisha vurugu hizo za maandamano.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako