• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 17-Oktoba 23)

    (GMT+08:00) 2020-10-23 15:45:42

    Marufuku kutoka nje usiku jijini Paris, hofu yatanda upya virusi vya Corona Ulaya

    Mamilioni ya raia barani Ulaya walikabiliwa na vikwazo vipya vya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona huku serikali zikiimarisha juhudi za kupunguza kuongezeka kwa maambukizi baada ya shirika la afya duniani WHO kuripoti kiwango cha "kutia wasiwasi" cha ongezeko la asilimia 44 la maambukizi barani Ulaya katika muda wa wiki moja.

    mji wa Paris na miji mingine ya Ufaransa iliwekwa chini ya marufuku ya kutotoka nje katika saa za usiku ambayo itadumu kwa takriban mwezi mmoja.

    Uingereza imepiga marufuku mikusanyiko katika nyumba katika mji wake mkuu London pamoja na maeneo mengine huku eneo la wakazi wengi nchini Italia likithibiti kufunguliwa kwa mabaa na kuahirisha hafla za michezo.

    Nchini ujerumani Kansela Angela Merkel amewatolea wito raia wa nchi hiyo kushirikiana pamoja kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona wakati ambapo nchi hiyo imetangaza idadi kubwa ya maambukizi ya siku ya COVID-19.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako