1: Ardhi, Maliasili na Idadi ya Watu

Idadi ya watu

Hali ya Leo

China ni nchi inayoongoza duniani kwa idadi ya watu, kufikia mwishoni mwaka 2002, idadi ya watu wa China ilikuwa ni bilioni 1.28453 mbali na idadi ya watu wa mikoa ya Hong Kong, Macau na Taiwan. Hii ni wastani wa moja kwa tano ya watu wote duniani. China pia ni nchi yenye watu wengi kwa wastani wa eneo, kwa wastani kuna watu 135 katika kila eneo la kilomita moja. Lakini watu hawapatikani kwa wastani katika kila sehemu bali wengi wanakusanyika katika sehemu ya mashariki, wachache katika sehemu ya magharibi. Katika sehemu ya mashariki kwenye mwambao, kwa wastani kila katika eleo la kilomita moja kuna watu zaidi ya 400, katika sehemu ya katikati kuna watu 200 na katika sehemu ya magharibi katika kila eneo la kilomita moja watu hawafiki 10. Hivi sasa wastani wa kuishi kwa wananchi wa China umeongezeka na kuwa miaka 71.4 ( miaka 69.63 kwa wanaume na 73.33 kwa wanawake), umri huo unazidi wastani wa umri wa kuishi duniani kwa miaka mitano, na unazidi nchi zanazoendelea kwa miaka 7, lakini unapungua kwa miaka mitano ukilinganishwa na nchi zilizoendelea.

Mwaka 2002 mwendo wa ongezeko la idadi ya watu wa China ulizidi kupungua, mwishoni mwa mwaka huo idadi ya watu ulikuwa bilioni 1.28453. Miongoni mwa watu hao, wakazi wa mijini ni milioni 502.12 ambao ni 39.1% ya watu wote; watu wa sehemu za vijijini walikuwa milioni 782.41 ambao ni 60.9 ya watu wote. Idadi ya wanaume ni milioni 661.15 na wanawake milioni 623.38. Watoto kutoka umri wa miaka sifuri hadi 14 ni 22.4%, wenye umri wa miaka tokea miaka 15 hadi 64 ni 70.3%, wazee wenye zaidi ya umri wa miaka 65 ni 7.3%, idadi ya wazee imefikia milioni milioni 93.77. Watoto waliozaliwa katika mwaka 2002 walikuwa milioni 16.47, ambao ni wastani wa 12.86 kwa 1000 ya watu wote; waliokufa walikuwa milioni 8.21, ambao ni wastani wa watu 6.41 katika 1,000; ongezeko la watu lilikuwa milioni 8.26, ambao ni sawa na watu 6.45 kwa kila watu 1000.

Hali ya Ongezeko la Idadi ya Watu na Uzazi wa Mpango

Mwaka 1949 Jamhuri ya Watu wa China ilipoasisiwa, jumla ya idadi ya watu wa China ilikuwa milioni 541.67. Kutokana na utulivu wa jamii, maendeleo katika uzalishaji na hali ya matibabu kubadilika kuwa nzuri, pamoja na kupuuzwa kimawazo madhara ya ongezeko la idadi ya watu na kutokuwa na uzoefu, idadi ya watu iliongezeka haraka, hadi kufikia mwaka 1969 idadi ya watu wa China ilifikia milioni 806.71. Ili kukabiliana na tatizo hilo, kuanzia miaka ya 70 ya karne iliyopita, China ilianza kutekeleza sera ya uzazi wa mpango na kudhibiti mwendo wa ongezeko la idadi ya watu, matokeo yakawa hadi mwaka 2002 ongezeko limepungua na kufikia wastani wa watu 12.86 kwa 1,000. Hivi sasa China imekuwa katika hali ya kiasi kidogo cha uzazi, kiasi kidogo cha vifo na kiasi kidogo cha ongezeko.

Kutokana na "mpango wa 10 wa maendeleo ya miaka mitano" uliopitishwa na bunge la umme la China, katika kipindi cha miaka mitano ya mpango huo (mwaka 2001-2005), ongezeko la idadi ya watu kwa wastani halitazidi watu 9 katika 1,000. Hadi kufikia mwaka 2005 idadi ya watu wa China itadhibitiwa kuwa chini ya bilioni 1.33 na kufikia mwaka 2010 idadi ya watu wa China itadhibitiwa kuwa chini ya bilioni 1.4.

Uzazi wa mpango ni sera ya kimsingi ya kitaifa nchini China. Uzazi wa mpango unatekelezwa kwa njia ya muunganisho wa uongozi wa kiserikali na hiari ya umma. Uongozi wa serikali unamaanisha kuwa serikali kuu pamoja na serikali za mitaa zinatoa sera na mpango wa ujumla katika udhibiti wa ongezeko la idadi ya watu, kuinua ubora wa idadi ya watu, kuboresha miundo ya idadi ya watu, na kutoa huduma za afya ya uzazi, kupata uzazi bora na malezi bora. Hiari ya umma inamaanisha kuwa wanaofikia umri wa kupata watoto wapange mimba na kuzaa kwa kuzingatia umri, hali ya afya, kazi na uchumi wa familia chini ya mwongozo wa sera na sheria za kitaifa, na kuchagua njia inayofaa kuepuka uja uzito.

Sera kuhusu uzazi wa mpango zinazotumika sasa nchini China ni kuchelewesha umri wa ndoa na uja uzito, kuzaa kwa watoto wachache na malezi bora; na mume na mke kuzaa mtoto mmoja tu. Katika sehemu za vijijini, mume na mke wakiwa kweli wana shida fulani wanaruhusiwa kuzaa watoto wawili; na katika sehemu za makabila madogo madogo sera ni tofauti kutokana na hali tofauti ya idadi ya watu, maliasili, uchumi, utamaduni na mila, kwamba kwa kawaida mume na mke wanaweza kuzaa watoto wawili na katika sehemu nyingine wanaweza kuzaa watoto watatu, na kabila lenye idadi ndogo sana ya watu wa kabila fulani hawawekewi kikomo cha watoto.

Tokea sera za uzazi wa mpango zianze kutekelezwa, kuchelewesha umri wa kuoa, kuzaa, kuzaa watoto wachache na kutoa kwa malezi bora imekuwa desturi katika jamii. Pamoja na hayo uzazi wa mpango umewawezesha wanawake kujinasua kuzaa mara nyingi na adha za nyumba, hali ya afya ya watoto na mama wazazi pia imekuwa bora zaidi.

Uzazi wa Mpango

1 2 3 4 5