9: Hifadhi ya Mazingira

Hali ya hifadhi ya mazingira ilivyo sasa nchini China

Maelezo ya jumla

Ingawa uendelezaji wa viwanda nchini China umekuwa na historia ya miaka 50 tu, lakini kutokana na nchi kuwa na idadi kubwa ya watu, ongezeko kubwa la uchumi na matatizo kadhaa yaliyosabishwa na sera za zamani, masuala ya mazingira na maliasili yamekuwa makubwa dhahiri nchini China kwa hivi sasa, na hali ya mazingira imekuwa ikikabiliwa na matatizo mengi, kama vile mmomonyoko wa ardhi unazidi kuwa mbaya siku hadi siku, eneo la ardhi inayobadilika kuwa jangwa linapanuka siku hadi siku, eneo la misitu limepungua kwa kiasi kikubwa, mazingira ya kimaumbile yameharibiwa, na aina nyingi za viumbe zimeharibiwa na kupungua hata badhi yao kutoweka, na uchafuzi wa maji na hali ya hewa umekuwa mbaya.

Mwanzoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, chini ya uhimizaji wa mkutano wa mazingira ya binadamu wa Umoja wa Mataifa, kazi ya hifadhi ya mazingira ya China ilianzishwa. Baada ya maendeleo ya zaidi ya miaka 20, China imeanzisha mfumo kamili wa kisheria na kisera wa kushughulikia uchafuzi na kuhifadhi maliasili, na uwekezaji katika hifadhi ya mazingira unaongezeka siku hadi siku. Lakini ikilinganishwa na nchi zilizoendelea, mfumo wa kisera wa hifadhi ya mazingira wa China bado haujakamilika, sera nyingi bado zimewekwa kwenye mipango ya jadi na maagizo ya serikali katika ngazi mbalimbali. Katika sehemu nyingi nchini, idara za serikali za hifadhi ya mazingira bado hazijaongeza nguvu ya utekelezaji wa sheria, na utekelezaji wa sera mbalimbali bado haujaweza kuhakikishwa, hayo yamezuia moja kwa mjoa kuboreshwa kwa hali ya mazingira. Hivi sasa serikali ya China imeongeza zaidi mkakati na sera kuhusu hifadhi ya mazingira, ili kuhakikisha binadamu na mazingira vinaishi kwa kupatana wakati China inapotimiza maendeleo mazuri ya kasi ya uchumi na jamii.

Hali ya mazingira ya maji

Maliasili ya maji ya China imekusanyika katika mito 7 mikubwa ya Changjiang, Huanghe, Songhuajiang, Liaohe, Zhujiang, Haihe na Huaihe. "Taarifa kuhusu hali ya mazingira ya China ya mwaka 2003" iliyotolewa na Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China inaonesha kuwa, hali ya uchafuzi kwenye mito 7 mikubwa ya China inazidi kupungua siku hadi siku. Takwimu za mwaka 2003 zimeonesha kuwa, maji ya China yenye sifa ya ngazi ya kwanza, pili na tatu yamechukua 37.7 %, na kiasi hiki cha mwaka 2001 kilikuwa chini ya 33 %.

Katika mifumo 7 ya mito mikubwa, eneo la mtiririko wa Mto Haihe na Mto Liaohe linakumbwa na uchafuzi mbaya zaidi kutokana na takataka za mafuta na uzalishaji wa bidhaa za aina mbalimbali. Ni mito na maziwa pamoja na mabwawa ambayo yamechafuliwa zaidi na madini ya nitrogen na phosphorus, ambapo madini yamezidi kiwango kwenye maziwa na mabwawa.

Sifa ya maji chini ya ardhi kwa ujumla ni nzuri katika miji mingi na sehemu nyingi nchini China, lakini maji hayo ya baadhi ya sehemu pia yamechafuliwa kwa kiasi fulani. Na katika viini vya miji yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na viwanda, maji yaliyoko chini ya ardhi yamechafuliwa vibaya zaidi. Kiasi cha vitu vya kemikali vilivyo ndani ya maji vimekuwa vingi kupita vigezo vilivyowekwa.

Hali ya usafi wa hewa

Katika miaka ya hivi karibuni, sifa ya jumla ya hewa katika miji ya China inabadilika kuwa nzuri, lakini katika theluthi mbili ya miji ya China, sifa ya hewa bado haijafika ngazi ya pili ya kigezo cha kitaifa. Chembechembe zinazoelea ndani ya hewa ni vitu vinavyoleta uchafuzi kwa sifa ya hewa ya miji, na katika miji ya kaskazini ya China, uchafuzi wa chembechembe zinazochafua hewa ya miji ya kaskazini ni mbaya zaidi kuliko miji ya kusini mwa China. Miji ya kaskazini inayoathiriwa vibaya zaidi na chembechembe zinazochafua hewa iko katika sehemu za kaskazini, kaskazini magharibi, kaskazini mashariki, katikati na mashariki ya mkoa wa Sichuan na mji wa Chongqing.


1 2 3 4 5 6