9: Hifadhi ya Mazingira

Ushirikiano wa kimataifa

Ushirikiano na maingiliano ya kimataifa kwenye sekta ya mazingira 

China ikiwa nchi kubwa kabisa inayoendelea na nchi yenye mazingira makubwa zaidi, imekuwa mhusika kwenye sekta ya mazingira ya kimataifa. China inafanya juhudi kubwa katika kushiriki shughuli za kidiplomasia kuhusu mambo ya mazingira duniani, na imetoa mchango na kufanya kazi za kiujenzi katika sekta za mazingira na maendeleo duniani

Mwaka 1972, ujumbe wa serikali ya China ulihudhuria mkutano wa kwanza kuhusu mazingira ya binadamu uliofanyika huko Stockholm. Mwaka 1992, waziri mkuu wa wakati huo Li Peng aliongoza ujumbe wa serikali ya China kuhudhuria mkutano wa wakuu kuhusu mazingira na maendeleo uliofanyika huko Rio de Janeiro, ambapo China ilitangulia kusaini "Mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa" na "Mkataba kuhusu aina nyingi za viumbe", hatua hiyo imesifiwa sana na jumuia ya kimataifa. Mwezi Agosti mwaka 2002, waziri mkuu Zhu Ronji aliongoza ujumbe wa serikali ya China kuhudhuria mkutano wa wakuu kuhusu maendeleo endelevu uliofanyika huko Johannesburg, ambapo alitangaza kuwa serikali ya China imethibitisha na kukubali "Mkataba wa Kyoto", hatua hii ilisifiwa na watu wengi wa jumuiya ya kimataifa.

Katika mkutano wa mazingira ya kimataifa na mazungumzo ya mkataba wa kimataifa, China ilishikilia tangu mwanzo hadi mwisho kanuni kuhusu nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea zinabeba wajibu wa pamoja ambao pia wa tofauti katika kulinda mazingira ya dunia nzima, ambapo China inasimama imara kwenye upande wa nchi zinazoendelea, inapinga umwamba kwenye sekta ya mazingira, na kupinga kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha suala la mazingira. Kutokana na historia na hali halisi ya hivi sasa, nchi zilizoendelea zote ni nchi zinazobeba wajibu mkubwa kuhusu suala la mazingira, na nchi zinazoendelea ni nchi zinazodhuriwa. Hivyo nchi zilizoendelea zinabeba jukumu la kuchukua hatua kwanza na kuzisaidia nchi zinazoendelea katika juhudi zao za kushiriki kwenye shughuli za kulinda mazingira ya dunia nzima.

Aidha, jumuiya za kiraia za hifadhi ya mazingira za nchi mbalimbali duniani kama vile Mfuko wa mazingira asilia ya dunia, na Mfuko wa kulinda wanyama duniani zimeanzisha ushirikiano na idara husika na jumuiya za kiraia za China, na matokeo yenye juhudi yamepatikana katika shughuli hizo.

China imevumbua kwanza aina ya "kamati ya ushirikiano wa kimataifa wa mazingira na maendeleo ya China". Kamati hiyo iliundwa na watu mashuhuri na wataalamu duniani zaidi ya 40, ambayo ni shirika la ngazi ya juu la utoaji ushauri la serikali. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, kamati hiyo imetoa mashauri mengi ya kiujenzi kwa serikali ya China, kamati hiyo imesifiwa kuwa ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa mazingira ya kimataifa.

Mikataba ya kimataifa ya mazingira ambayo China imeasini

China ikiwa na msimamo wa kuwajibika na juhudi za hifadhi ya mazingira na maliasili duniani, imejiunga au kusaini mikataba na makubaliano ya kimataifa zaidi ya 30 kuhusu hifadhi ya mazingira na maliasili. Mikataba hiyo ni kama ifuatayo:

"Mkataba wa kimataifa wa kuzuia uchafuzi wa mafuta baharini" (mwaka 1954, London)

"Mkataba kuhusu kuvua samaki na kutunza maliasili ya viumbe baharini" (mwaka 1958, Geneva)

"Mkataba wa kimataifa wa usimamizi wa shughuli za kuvua pomboo" (Mwaka 1946, Washington)

"Mkataba wa Asia ya kusini mashariki kuhusu hifadhi ya mimea" (mwaka 1956, Rome)

"Mkataba kuhusu sehemu ya rasi" (mwaka 1958, Geneva)

"Mkataba wa ncha ya kusini" (mwaka 1959, Washington)

"Mkataba wa jumuiya ya hali ya hewa duniani" (mwaka 1947,Washington)

"Mkataba wa kimataifa kuhusu wajibu wa mambo ya kiraia juu ya uchafuzi wa mafuta duniani" (mwaka 1969, Brussers)

"Mkataba wa hifadhi ya mali za urithi za utamaduni na maumbile duniani" (mwaka 1972, Paris)

"Mkataba kuhusu kanuni zinazopaswa kufuatwa na nchi mbalimbali katika kufanya utafiti na kutumia nafasi za anga ya juu pamoja na mwezi na sayari nyingine" (mwaka 1972, Moscow)

"Mkataba wa kuzuia uchafuzi baharini kutokana na kutupa takataka na vitu vingine" (mwaka 1972, London)

"Mkataba kuhusu kupiga marufuku kuendeleza, kutengeneza na kulimbikiza vijidudu (viumbe) na silaha zenye sumu na kuteketeza silaha kama hizo" (mwaka 1972, London)

"Mabakuliano kuhusu kufanya mawasiliano kwenye bahari za kimataifa wakati uchafuzi unaosababishwa na vitu visivyo vya mafuta" (mwaka 1973, London)

"Mkataba wa kimataifa wa kuzuia uchafuzi unaosababishwa na meli" (mwaka 1978, London)

"Mkataba wa hifadhi ya vifaa na vitu halisi vya kinyuklia" (mwaka 1979, Viena)

"Mtakaba wa Vienna wa hifadhi ya ukanda wa ozone" (mwaka 1985, Viena)

"Mkataba kuhusu utoaji msaada wakati wa kutokea kwa tukio la dharura la kinyuklia au la mionzi ya x-ray" (mwaka 1985, Viena)

"Mkataba kuhusu tukio la kinyuklia na utoaji ripoti mapema" (mwaka 1985,Vienna)

"Mkataba wa Montreal kuhusu vitu vya kudhoofisha tabaka la ozone" (mwaka 1987, Montreal)

"Mkataba wa mfumo wa kituo cha ufugaji wa samaki wa Asia na Pasifiki" (mwaka 1988, Bangkok)

"Mkataba wa Basel kuhusu kudhibiti uhamishaji wa takataka zenye hatari kwa nchi za nje na kushughulikia takataka hizo" (mwaka 1989, Basel)

"Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa" (Mwaka 1992, Rio de Janeiro)

"Mkataba kuhusu aina nyingi za viumbe" (mwaka 1992, Rio de Janeiro)

"Mkataba wa Serikali za Jamhuri ya Watu wa China na Shirikisho la Jamhuri za kisoshalisti za kisoviet kuhusu ulindaji wa pamoja wa misitu na kukinga moto" (mwaka 1980)

"Mkataba wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Japan kuhusu kulinda ndege wanaohamahama na mazingira yao ya kuishi" (mwaka 1981)

"Mkataba wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Australia kuhusu kulinda ndege wanaohamahama na mazingira yao ya kuishi" (mwaka 1986)

"Mkataba wa Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya kiislamu ya Pakistan kuhusu ushirikiano wa matumizi ya kiamani ya nishati ya nyuklia" (Mwaka 1986)

Zaidi ya hayo, China pia imefanya juhudi za kuunga mkono nyaraka nyingi muhimu kuhusu hifadhi ya mazingira na maliasili za kimataifa, na kuingiza moyo wa nyaraka hizo kwenye sheria na sera za China. Nyaraka hizo ni pamoja na "Taarifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira ya binadamu" iliyotolewa mwaka 1972 huko Stockholm, Sweden, "Mwongozo mkuu wa hifadhi ya maliasili za dunia" uliotolewa mwaka 1980 na nchi nyingi duniani kwa wakati mmoja, "Taarifa ya Nairobi" iliyotolewa mwaka 1982 huko Nairobi, Kenya na "Taarifa ya Rio de Janeiro kuhusu mazingira na maendeleo" iliyotolewa mwaka 1992 huko Rio de Janeiro, Brazil.

China yatekeleza mikataba ya mazingira ya kimataifa 

China ikiwa na msimamo wa kuwajibika kwa juhudi, imefanya juhudi za kutekeleza majukumu yake yanayowekwa kwenye mikataba mingi muhimu kuhusu mazingira ya kimataifa iliyojiunga nayo. Kuhusu mikataba mingi muhimu ya mazingira ya kimataifa, China imefanya mipango yake ya utekelezaji. Kwa mfano, China imetunga "Mpango wa China wa kuchuja hatua kwa hatua vitu vya kudhoofisha tabaka la ozone" na "Ripoti ya nchi kuhusu China kutekeleza mkataba wa aina nyingi za viumbe" na kadhalika, na China pia imechukua hatua nyingi zinazosaidia kutekeleza kihalisi mikataba ya kimataifa.

Sasa tunajulisha kwa kifupi hali kuhusu China kutekeleza "Mkataba wa Montreal kuhusu vitu vya kudhoofirisha ngazi ya ozone" na "Mkataba wa aina nyingi za viumbe"

China na "Mkataba wa Montreal"

Katika miaka 10 iliyopita, China imeshiriki kwa juhudi katika shughuli mbalimbali za kimataifa za kulinda tabaka la ozone. Mwaka 1986, 1987 China iliwatuma wajumbe kuhudhuria mkutano wa kikundi cha kulinda ngazi ya ozone na mkutano wa kusaini "barua ya makubaliano". Mwaka 1989 China ilijiunga rasmi na mkataba huo, na kwenye mkutano wa kwanza wa nchi zilizosaini mkataba, China ilitangulia kutoa pendekezo kuhusu "kuanzisha mfuko wa pande nyingi wa kulinga ngazi ya ozone". Mwaka 1990, China ilishirikiana na nchi mbalimbali duniani katika juhudi za kushiriki kwenye kazi ya marekebisho ya "Waraka wa makubaliano". Mwaka 1991, China ilijiunga rasmi na mswada wa marekebisho wa London kuhusu "Waraka wa makubaliano", na ilianzisha kwa wakati ofisi ya kikundi cha uongozi cha China cha kulinda ngazi ya ozone kilichoshirikisha wizara, kamati, makampuni makuu na mashirikiano makuu ya China yapatayo 15, ili kubeba kazi ya utekelezaji wa waraka huo wa makubaliano. Mwaka 1992, China ilitangulia kutunga "Mpango wa nchi ya China wa kuchuja hatua kwa hatua vitu vya kudhoofisha ozone", na mpango huo uliidhinishwa mwanzoni mwa mwaka 1993 na Baraza la serikalli na Kamati ya utendaji wa mfuko wa pande nyingi. Mwaka 1994, China ilitunga "Nyongeza za mpango wa mashirika ya tumbaku kuchuja hatua kwa hatua vitu vya kudhoofisha ozone".

Mpaka hivi sasa kupitia Benki ya dunia, Shirika la mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa, Shirika la viwanda na maendeleo la Umoja wa Mataifa, na Shirika la mipango ya mazingira la Umoja wa Mataifa, pamoja na nchi za Marekani, Canada, Ujerumani na Denmark, miradi 156 ya China imeidhinishwa na Kamati ya utendaji ya Mfuko wa pande nyingi, na kupata dola za kimarekani milioni 105. Kama miradi hiyo yote itakamilika, vitu vinavyodhibitiwa vitapungua kwa tani elfu 31.8.

China na "Mkataba wa aina nyingi za viumbe"

Baada ya kufanyika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira na maendeleo mwaka 1992, serikali ya China imezingatia hali yake halisi ya nchi, ikiwa na msimamo wa makini inatekeleza ahadi yake kwenye mkutano huo, kuthibitisha mikakti ya maendeleo endelevu ya uchumi wa taifa, na kuonesha ipasavyo mawazo ya mikakati hiyo katika sera mbalimbali za uchumi wa nchi. Mwaka 1994, Baraza la serikali la China liliidhinisha na kutangaza "Waraka kuhusu idadi ya watu, mazingira na maendeleo ya China katika karne ya 21", waraka huo umeonesha vilivyo mikakati ya maendeleo endelevu ya nchi. Mwaka 1996 Bunge la umma la China lilipitisha "Mpango wa 9 wa miaka mitano kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii ya Jamhuri ya Watu wa China na Mwongozo wa malengo ya mbali ya mwaka 2010", hii imebainisha zaidi sera ya China ya kushikilia mikakati ya maendeleo endelevu.

Serikali ya China inaona kuwa, matumizi ya kudumu ya maliasili na mazingira mazuri ya viumbe ni masharti ya kwanza katika kutekeleza mikakati ya maendeleo endelevu. China imechukua hatua za kulinda aina nyingi za viumbe, kuzuia mmomonyoko wa ardhi na hali ya jangwa kwenye ardhi, kuendeleza eneo la misitu na kuboresha mazingira ya viumbe mijini na vijijini, kukinga na kudhibiti uharibifu na uchafuzi kwa mazingira, na kushiriki kwa juhudi ushirikiano wa dunia nzima katika hifadhi ya mazingira, ili kutekeleza kwa ufanisi mikakati ya maendeleo endelevu. Mambo kuhusu kulinda aina nyingi za viumbe ili kuzitumia mwaka baada ya mwaka yameoneshwa katika sera, mipango na kazi mbalimbali za idara zote za serikali na mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii ya serikali za mitaa za ngazi mbalimbali.

Katika mchakato wa mpito wa kuanzishwa kwa uchumi wa soko huria badala ya uchumi wa mipango wa jadi, serikali ya China imefanya juhudi katika kuhimiza uzalishaji wa kilimo wa njia ya kisayansi na kiteknolojia ili kupata ongezeko la uchumi. Kutokana na ongezeko la haraka la idadi ya watu na matumizi ya maliasili kupita kiasi, hali ya mazingira ya viumbe inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, hali ya mmomonyoko wa ardhi, na hali ya ardhi inayobadilika kuwa jangwa inazidi kuwa mbaya, na maliasili za viumbe zinatumika kwa haraka kupita kiasi, yote hayo yamekwamisha vibaya maendeleo ya uchumi wa taifa, hasa kuzidisha hali ya umaskini kwenye sehemu zenye uharibifu wa mazingira ya viumbe. Serikali ya China inazingatia mageuzi ya sera za uchumi wa vijijini, kuwahamasisha wakulima kutumia njia ya kisayansi na kiteknolojia katika uzalishaji wa mazao, kuanzisha miradi ya ujenzi wa mazingira ya viumbe kama vile kupanda miti na majani na kuendeleza misitu, kushughulikia hali ya mmomonyoko wa ardhi na kuondoa hali ya jangwa, kuendeleza teknolojia ya kilimo cha kiviumbe na kadhalika. Hatua hizo zitatekelezwa na kwenda sambamba na kuendeleza uzalishaji mazao ya kilimo na kulinda aina nyingi za viumbe ili kudumisha matumizi ya kudumu.

Katika miaka mingi iliyopita, China imepata uzoefu mwingi wenye manufaa katika ujenzi wa mazingira ya viumbe kote nchini, kama vile uzoefu wa kujenga misitu mikubwa ya kukinga upepo, na kujenga mazingira yenye majani kwenye jangwa; kutengeneza mashamba kwenye miteremko ya milima kuwa mashamba ya kulima na kujenga mashamba yanayoweza kuzalisha mazao mengi zaidi katika hali ya utulivu; kujenga mejengo makubwa ya kuhifadhi maji mashambani na kufanya ujenzi wa miradi midogo ya kulimbikiza maji na kuzuia mmomonyoko wa ardhi; kurudisha misitu na malisho kwenye ardhi iliyotumiwa kwa kilimo, na kufufua hali ya mazingira ya maumbile ya kiasili; kupanda miti ya kiuchumi, kujenga misitu asilia na kupanda miti na majani kwa pamoja; kuanzisha shughuli za kilimo kwa kubana matumizi ya maji, na kutumia teknolojia za kisasa; kujenga mazingira yenye milima, maji, mashamba, misitu na barabara, na kuboresha hali ya eneo dogo la mitiririko ya mito; kupanda miti na majani kwenye milima iliyoachwa; kushughulikia hali ya kuvia, kuwa ya jangwa na kuwa na madini ya alkali kwa malisho na kadhalika, uzoefu huo na hatua za utekelezaji zote zimefanya kazi muhimu zenye juhudi kwa kulinda aina nyingi za viumbe.

 


1 2 3 4 5 6