12: Wanawake

Hali ya Jumla ya Wanawake nchini China

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2002, idadi ya wanawake nchini China ilikuwa milioni 620, ikichukua asilimia 48.5 ya idadi yote ya watu nchini China. Serikali ya China inatilia maanani sana maendeleo ya wanawake, kuifanya sera ya usawa kati ya wanaume na wanawake kama sera mojawapo ya kimsingi ya kitaifa katika kusukuma mbele maendeleo ya jamii. Wakati inapotunga sera za jumla, serikali ya China hufuata kanuni za kuwashirikisha kwa usawa wanaume na wanawake na kuhimiza maendeleo ya pamoja. Serikali ya China imetoa uhakikisho imara wa kisiasa na dhamana ya kisheria kwa maendeleo ya wanawake.

Kuanzia katikati ya miaka ya tisini ya karne iliyopita, serikali ya China imetoa "Mwongozo wa Maendeleo ya wanawake wa China" wa miaka mitano na miaka kumi, ambao umelinda kihalisi haki na maslahi halali ya wanawake, kuboresha mazingira ya kijamii ya maendeleo ya wanawake nchini China na kusukuma mbele maendeleo ya pande zote ya kazi ya wanawake. Wanawake wa China si kama tu wana haki sawa na wanaume katika maeneo ya siasa, uchumi, jamii, utamaduni na nyumbani, na haki zao maalum zinafuatiliwa zaidi na serikali na jamii. Chini ya juhudi za pamoja, hadhi ya wanawake nchini China imeinuka kidhahiri, hali ya wanawake imeboreshwa na maendeleo ya wanawake nchini China yameingia katika kipindi kizuri.


1 2 3 4 5 6 7