12: Wanawake

Ushiriki wa wanawake katika Shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii

Ushiriki wa wananwake katika mambo ya kisiasa

Kwa mujibu wa katiba ya China, wanawake wa China wana haki sawa ya kisiasa na wanaume: wanawake wa China wana haki sawa na wanaume ya kuchagua na kuchaguliwa; wana haki sawa ya kujihusisha na usimamizi wa mambo ya taifa na kupewa ajira kwenye ofisi za kiserikali. Kati ya wajumbe wa bunge la umma la China, kuna wabunge 604 wanawake, ambao wanachukua asilimia 20.2 ya wajumbe wote nchini. Kuna wajumbe 373 wanawake kwenye baraza la 10 la mashauriano ya kisiasa la China. Ili kuhakikisha kwa kiasi fulani cha wanawake wanaoshiriki katika mambo ya kisiasa, China imeanzisha mfumo wa kuwaandaa na kuwachagua makada wanawake. Mwaka 2003, wanawake 7 wa China waliteuliwa kuwa viongozi wa serikali kuu, nao ni naibu waziri mkuu wa baraza la serikali Bibi Wu Yi, manaibu spika wa bunge la umma la China Bibi He Luli, Gu Xiulian na Wuyunqimuge, mjumbe wa mambo ya taifa Bibi Chen Zhili, naibu mwenyekiti wa halmashauri ya mashauriano ya kisiasa ya China Bibi Liu Yandong na Hao Jianxiu. Kati ya wizara 28 za serikali, kuna waziri mwanamke mmoja, manaibu waziri wanawake 15; makada wanawake 5056 wanaoteuliwa kuwa viongozi katika serikali za ngazi tatu za mkoa, wilaya na tarafa. Wanawake wengi wameongeza mwamko wa kushiriki katika mambo ya kisiasa. Katika uchaguzi wa wabunge wa kisehemu, wanawake wanaoshiriki katika upigaji kura wanafikia asilimia 73.4.

Malengo muhimu yaliyotolewa kwenye Mwongozo wa 2001-2010 wa maendeleo ya wanawake nchini China ni: kuinua kiwango cha wanawake cha kushiriki katika usimamizi wa mambo ya nchi na jamii; kuongeza idadi ya wanawake wanaoshiriki katika usimamizi wa utawala, katika ngazi mbalimbali za serikali lazima kuwe na kada mmoja mwanamke au zaidi; katika idara za serikali kuu, mikoa na wilaya, makada wanawake watachukua kiasi fulani cha nafasi; ili kuinua hali ya wanawake ya kushiriki kwenye demokrasia na mambo ya serikali.

Serikali ya China imeweka mazingira mazuri ya kijamii kwa wanawake kushiriki kwenye mambo ya kisiasa kama vile, kuimarisha kazi ya kuwaandaa makada wanawake ili kuinua kiwango cha wanawake wa kushiriki kwenye mambo ya kisiasa na uwezo wa ushindani, kuimarisha kazi ya kuwaandaa wataalamu na wasimamizi wanawake ili kuongeza sifa yao ya kisiasa na uwezo wao wa utendaji.

Kutokana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini China, wanawake wengi zaidi wa China wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli za aina mbalimbali za kijamii.

Ili kutekeleza mkakati wa kuendeleza sehemu ya magharibi, wanawake wa China wanashiriki ipasavyo katika shughuli za kujenga maskani mazuri katika sehemu ya magharibi na kuboresha mazingira ya maskani; Shirikisho Kuu la Wanawake la China liliteuliwa kuwa moja kati ya idara bora 500 duniani na Shirika la Maendeleo ya Mazingira la Umoja wa Mataifa.

Ili kutekeleza "Muongozo wa ujenzi wa maadili ya raia", idara husika zimetekeleza "Mpango wa Ujenzi wa maadili ya raia vijana wa China", kuanzisha harakati ya uzalendo ya kuwahamasisha watoto wasome vitabu ili kuwahimiza wawe na maadili na mienendo mizuri. Idara hizo pia zimekuwa zikizidisha elimu ya familia, kueneza ujuzi wa kuzaa watoto wenye afya, kuwatunza vizuri na kuwaelimisha vizuri. Kuanzisha shule laki 3 za wazazi nchini kote, ambapo mashirika yanayoshughulikia elimu ya familia yameanzishwa katika wilaya zaidi ya asilimia 70 nchini, ili kuinua kiwango cha wazazi cha kuwaelimisha watoto wao nyumbani.

Shughuli za huduma za jamii kama vile "Mpango wa kuwasaidia wasichana maskini", "Mpango wa afya" na kadhalika zimechangisha fedha za misaada yuan milioni 300 kutoka kwa wachina walioko nchini China na nchi za ng'ambo, ambayo imetoa mchango mkubwa katika kuboresha hali ya maisha na maendeleo ya watoto wanaoishi katika sehemu maskini.

Harakati ya Kujenga Familia Bora za Kistaarabu

Mashirikisho ya wanawake yalianzisha harakati za kuchagua familia bora za ustaarabu kuanzia miaka ya 50 ya karne iliyopita. Hadi mwishoni mwa mwaka 1999, familia karibu elfu 30 zilichaguliwa na kupewa sifa ya familia bora za ustaarabu za ngazi ya mkoa. Ili kuzisaidia familia kufuatana na jamii ya zama za hivi sasa inayobadilika siku hadi siku, kuhimiza njia ya maisha ya ustaarabu, afya na sayansi, mashirika ya wanawake nchini kote yamefanya shughuli za aina mbalimbali za utamaduni wa kifamilia. Kuwasaidia wakazi kuwa na mtazamo mzuri kuhusu maisha na thamani ya vitu. Zaidi ya hayo, mashirikisho ya ngazi mbalimbali ya wanawake pia yamewasaidia wakazi kujenga familia zenye masikilizano.

Katika sehemu za vijijini, China imeanzisha shughuli za kuwasaidia wakulima kuondokana na umaskini na kujiendeleza kwa njia za kisayansi na teknolojia. Kuwaongoza wakulima kuachana na desturi zinazopitwa na wakati, kuinua mwamko wao wa kujenga mwili na kuboresha mazingira, kuinua kiwango cha maisha kwa kuchapa kazi. Pia inaendelea kukamilisha miradi ya aina mbalimbali kama vile kutengeneza mabomba ya maji, mifereji, barabara, vyoo na vizuizi vya mifugo, ili kubadilisha sura ya familia na vijiji. Katika mitaa ya mijini, pia zimefanywa shughuli za aina mbalimbali kama vile, "naupenda mtaa wangu" na "naipenda familia yangu", kuwakaribisha majirani nyumbani na kuwahimiza wakazi wanaokaa kwenye jengo moja wafahamiane, na kuongeza wajibu wa kijamii kwa wanafamilia. Mikoa kadhaa imeanzisha shughuli za kutoa elimu ya mazingira kwa kauli mbiu ya "wanawake, maskani na mazingira", kueneza ujuzi wa hifadhi ya mazingira, kuinua mwamko wa hifadhi ya mazingira kwa familia zote, na shughuli za kusafisha na kuboresha mazingira ya mtaa, na kusukuma mbele ujenzi wa mtaa wa kistaarabu.


1 2 3 4 5 6 7