12: Wanawake

Shirikisho Kuu la Wanawake wa China

Shirikisho hili ni jumuiya yenye uwakilishi mkubwa inayowashirikisha wanawake wa makabila mbalimbali na wa fani mbalimbali nchini China, chini ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China ili kujipatia ukombozi zaidi. Shirikisho Kuu la Wanawake wa China ni daraja la mawasiliano kati ya chama cha kikomunisti cha China na serikali ya China na wanawake, na ni moja ya mihimili muhimu ya jamii kwa utawala wa nchi. Shirikisho Kuu la Wanawake wa China lilianzishwa mwezi March mwaka 1949, mwanzoni liliitwa Shirikisho la Wanawake la Kidemokrasia la taifa la China. Mwaka 1957 lilibadilishwa jina na kuwa Shirikisho la Wanawake la Jamhuri ya Watu wa China, mwaka 1978 lilibadilishwa kuwa Shirikisho Kuu la Wanawake wa China. Jukumu lake la kimsingi ni kuwaunganisha na kuwahamasisha wanawake kushiriki katika ujenzi wa uchumi na maendeleo ya kijamii, kuwakilisha na kulinda maslahi ya wanawake na kuhimiza usawa kati ya wanaume na wanawake.

Mashirika Mengine ya Wanawake

Mashirika mengine ya wanawake nchini China ni kama yafuatayo:

-Shirika la vijana wa kike la dini ya Kikristo la taifa la China

-Shirikisho la wanakampuni wanawake wa China

-Kamati ya wanajiografia wanawake wa taasisi ya jiografia ya China

-Kamati ya wanawake waliosoma Ulaya na Marekani

-Kamati ya kazi ya wataalamu wanawake katika taasisi ya utafiti ya wataalamu wa China

-Shirikisho la wanasayansi na wanateknolojia wanawake la China

-Kamati ya utalii ya wanawake ya Shirikisho la Utalii la China

-Shirikisho la Mahakimu wanawake wa China

-Shirikisho la maofisa wanawake wa uendeshaji wa mashitaka wa China

-Kamati ya wasanifu wanawake wa miji wa shirika la mipango ya miji la China

-Chama cha madaktari wanawake wa China

-Chama cha wapigaji picha wanawake wa China

-Kamati ya wanawake ya shirikisho la kuhimiza ujenzi wa sehemu kongwe la China

-Shirikisho la wanakampuni wanawake wa Chama cha wanaviwanda na wafanyabiashara cha China

-Kamati ya wanafanyazi wanawake wa shirikishio kuu la wafanyakazi la China

-Tawi la mameya wanawake la shirikisho la mameya la China

-Taasisi ya utafiti wa utamaduni wa familia ya China

-Kituo cha utoaji huduma za kisaikolojia cha wanawake cha Beijing

-Idara ya utafiti wa wataalamu wanawake ya taasisi ya utafiti wa maendeleo ya nguvukazi ya China

-Kituo cha utafiti wa kulingana cha wanawake wa Kimataifa

-Taasisi ya utafiti wa afya ya uzazi ya mkoa wa Yunnan

-Kituo cha utafiti wa wanawake wazee cha shirikisho kuu la wanawake wa China

-Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wa China

-Shirikisho la kuhimiza haki na maslahi ya wanawake la mji wa Taipei

-Kituo cha Uchunguzi wa Wanawake cha Huakun


1 2 3 4 5 6 7