13: Utibabu wa Jadi

Hali ya Tiba ya Jadi

Tiba ya jadi ya kichina ni mfumo wa tiba wenye nadharia ya kipekee, ambayo ilijengwa kutokana na kutibu wagonjwa na uzoefu wa muda mrefu.

Tiba ya jadi ya kichina ni jumla tiba za makabila mbalimbali ya China zikiwa ni pamoja na za makabila ya wahan, watibet, wamongolia na wauigur. Miongoni mwa tiba za jadi za kichina, kutokana na kuwa idadi ya wahan ni kubwa zaidi, kuwa na maneno mapema zaidi na kuwa na historia kwa miaka mingi zaidi, hivyo tiba ya kabila la wahan ina athari kubwa nchini China na hata duniani. Baada ya tiba ya nchi za magharibi kuingia na kuenea nchini katika karne ya 19, tiba ya kabila ya wahan ilijulikana kwa "tiba ya kichina" ili kuitofautisha na "tiba ya nchi za magharibi".


1 2 3 4 5 6 7