13: Utibabu wa Jadi

Akyupancha

Akyupancha ni sehemu muhimu ya tiba za jadi za kichina, hapo awali ilikuwa mbinu moja ya tiba, na hatimaye ikaendelezwa kuwa elimu moja. Elimu ya akyupancha ni sayansi ya kuweka utaratibu wa kuhusu teknolojia ya tiba ya akyupancha na nadharia ya msingi wa tiba.

Akyupancha imeshakuwa na historia ya miaka mingi sana, na iliendelezwa zaidi baada ya kupata maendeleo makubwa ya kuyeyusha chuma katika mwaka 476 hadi mwaka 25 kabla ya Kristo. Tiba ya akyupancha iliingia katika nchi jirani zikiwemo Korea na Japan katika mwaka 256 hadi mwaka 589.

Katika kipindi cha Enzi ya Sui na enzi ya Tang (mwaka 581 hadi mwaka 907) akyupancha ilipata maendeleo makubwa. Hivi sasa hospitali zaidi ya 2,000 za tiba za kichina zimekuwa na sehemu za tiba za akyupancha; utafiti kuhusu sayansi ya akyupancha umepiga hatua kubwa katika kurekebisha mfumo wa kazi za viungo vya mwili, kuondoa maumivu na kuongeza nguvu ya kukinga maradhi.


1 2 3 4 5 6 7