13: Utibabu wa Jadi

Massage(Usingaji)

Mbinu ya kuzuia maradhi na kuimarisha afya kwa kukanda na kusugua kwenye sehemu maalumu zilizoko katika mfumo wa mzunguko wa damu na pumzi, ambayo inajulikana kama massage au usingaji.

Massage inafanyika kwa kuelekezwa na nadharia ya tiba za kichina, ambayo inaleta matokeo mazuri kwa tiba za magonjwa ya aina nyingi, zikiwa ni pamoja na ugonjwa wa mifupa ya uti wa shingo, kuchoka kupita kiasi kwa misuli ya sehemu ya viuno, kujitokeza kwa mifupa ya uti wa mgongo pamoja na kuteguka kwa mafundo ya miguuni na mikononi. Uwezo wa Massage ni pamoja na kurekebisha uwezo wa kazi za viungo vya mwilini uliosoweza kufanya kazi barabara, na kuuweka katika hali mpya ya uwiano kwa kutumia mbinu ya massage ili kuimarisha afya ya mgonjwa.

Pili, massage inaweza kusawazisha mifumo na mishipa ya mwilini pamoja na vitu vinavyodumisha uhai. Pindi mifumo na mishipa ya mwilini ikiwa katika hali isiyo ya kawaida, vitu vibaya vinaweza kusababisha ugonjwa kwa kupitia viungo vya mwili wa binadamu.

Tatu, massage inasawazisha misuli na mafundo ya mifupa, na inahifadhi mzunguko wa mifumo na mishipa ya mwili wa binadamu.


1 2 3 4 5 6 7