13: Utibabu wa Jadi

Tiba za Makabila Madogo Madogo

Hali ya Tiba za Makabila Madogo Madogo

Tiba za jadi ya kichina ni pamoja na tiba za kabila la wahan na za tiba za makabila madogo mbalimbali. Kutokana na tofauti za historia na utamaduni, hali ya maendeleo ya tiba za makabila madogo madogo ni tofauti pia. Tiba za baadhi ya makabila madogo licha ya kuchukua sehemu fulani ya tiba ya kabila la wahan, imechukua baadhi ya sehemu ya tiba za nchi za nje. Kwa mfano tiba za kabila la watibet licha ya kuchukua sehemu fulani ya tiba za kabila la wahan, inachukua sehemu fulani ya tiba za jadi za Ingia ya kale, wakati tiba za kabila la wamongolia zinachukua sehemu fulani ya tiba za Russia.

Tiba za Jadi za Kabila la Watibet

HALI YA TIBA ZA KITIBET

Tiba za kitibet ni moja ya sehemu muhimu ya tiba za jadi za kichina, ambayo imevumbuliwa katika uzoefu wa muda mrefu wa kutibu wagonjwa katika maeneo ya makabila madogo madogo ,hususan katika maeneo ya kabila la watibet ikiwemo ya mikoa ya Tibet, Qinghai, Sichuan na Gansu, licha ya hayo tiba za kitibet pia zimeenea sana katika nchi za Asia ya kusini zikiwemo India na Nepal. Kutokana na mazingira maalumu ya jamii na maumbile, dawa za kitibet zinatumia zaidi wanyama na mimea ya sehemu za baridi kali na zenye hewa kidogo.

Katika tibet, kutokana na kuwa mawazo ya kidini yameingia katika pande mbalimbali za jamii na kuwa nguvu kubwa inayoongoza, hivyo tiba za kitibet zinaingiliana na dini ya Buddha ya kitibet tangu ilipoanza kuweko.

NDAHARIA YA KIMSINGI YA TIBA ZA KITIBET

Katika uzalishaji mali, maisha na uzoefu wa tiba, tiba za kitibet zimekuwa na mfumo wake wa kipekee wa nadharia.

Nadharia ya chimbuko tatu

Nadhari ya tatu za kitibet inaona kuwa mwilini mwa binadamu kuna chimbuko tatu za "Long", "Chiba" na "Beigen"; Msingi wa vitu vya aina 7 ambavyo ni rutuba ya chakula, damu, shahamu, mifupa, ute ulioko katikati ya mifupa na shahawa; Vinyesi vya binadamu vikiwa ni pamoja na kinyesi cha haja kubwa, kinyesi cha haja ndogo na jasho. Chimbuko tatu zinatawala msingi wa vitu vya aina saba pamoja na mabadiliko ya vinyesi vya aina tatu. Katika hali ya maisha ya kawaida mambo hayo matatu yanategemeana na kuzuiana, hali ambayo inaleta mazingira ya kupatana na kuendana. Wakati moja au zaidi ya moja ya mambo hayo matatu yakiingia kwenye hali ya kustawi au kuzorota kutokana na sababu fulani, unaweza kutokea ugonjwa wa "Long", "Chiba" au "Beigen", tiba zinatakiwa kuyarekebisha uhusiano wa mambo hayo matatu na kuyarejesha katika hali ya kupatana.

UMAALUMU WA TIBA ZA KITIBET

TIBA ZA MADAWA

Wakati inapotibu mgonjwa, tiba za kitibet huwa zinatumia kitu kinachoongoza dawa kwenda katika sehemu yenye matatizo, kwa mfano wakati mwingi sukari inatumika kuongoza dawa katika kuponya mgonjwa mwenye homa, na kutumia sukari ya guru (sukari nyeusi) kutibu mgonjwa aliyeugua kutokana na kupatwa na baridi.

Mbali na hayo, namna ya kumeza dawa pia kuna kanuni zake. Kwa mfano donge la dawa kwa kawaida linasindikizwa na maji, lakini mgonjwa aliyeugua kutokana na baridi, anatakiwa kusindikiza dawa kwa maji moto; kwa mgonjwa yanayotokana na joto, basi atafanya kinyume chake na kusindikiza dawa kwa maji baridi.

MBINU YA UTAPISHAJI

Mbinu ya kufanya mgonjwa kutapika kwa kumpa dawa ya utapishaji ni moja ya tiba za kitibet, ambayo inaweza kutibu matatizo ya chakula kubaki kwenye utumbo wa chakula, kula chakula chenye sumu kwa bahati mbaya au wadudu walioko ndani ya matumbo ya binadamu walijisogeza karibu na koo na kushindwa kurejea ndani au kwa tatizo la kuwa na makohozi kooni, isipokuwa wadhaifu, wazee, wajawazito pamoja na watoto wachanga. Kwa watu wale waliokula vitu vyenye sumu, muda mrefu ukipita muda mrefu, wasitapishwe kwa kula dawa, kwani vitu vyenye sumu haviko tena katika utumbo wa chakula.

MBINU YA UPAKAJI WA DAWA

Kutumika dawa ya kupaka ni moja ya mbinu rahisi ya tiba za kitibet, hata watu wa kawaida wanaweza kuitumia. Tiba za kitibet zinaona kuwa upakaji wa dawa, ambayo ni ya aina ya mafuta, unaweza kutibu udhaifu wa mwili, kuchoka kupita kiasi na kuwa una usingizi sana.

TIBA YA KUOGA KWA MAJI YENYE DAWA

Mbinu ya kuoga kwa maji yenye dawa ni moja ya tiba ya kitibet. Maji yanayotumika zaidi ni ya chemchem yenye madini ya sulfur.

Tiba za Kimongolia

HALI YA TIBA ZA KIMONGOLIA

Tiba za kabila la wamongolia nchini ziliendelezwa hatua kwa hatua kuwa tiba za jadi za kimongolia katika uzoefu wa tiba katika miaka mingi iliyopita, na pia ni sayansi ya tiba inayoendana na umaalumu wa kikabila na mazingira ya huko. Tiba za kimongolia zinajulikana kwa kutumia dawa kidogo na zenye ufanisi mwingi, rahisi kutumika na ya gharama ndogo.

NADHARIA YA MSINGI WA TIBA ZA KIMONGOLIA

Tiba za kimongolia zinatumia uhusiano za chimbuko tatu za "Heyi", "Xila" na "Badagan" kufafanua hali ya mwili na kuugua ugonjwa kwa binadamu. "Heyi" ni nguvu ya uwezo wa mwili wa binadamu. Mawazo, maneno, vitengo na kazi za maungo ya mwili vyote vinatawaliwa nayo. Endapo "Heyi" haifanyi kazi zake barabara, uwezo wa maungo ya mwili wa binadamu utafifia na kuonekana kutokuwa na umakini, kupaa usingizini na kuwa msahaulifu.

"Xila" maana yake ni moto. Ujoto wa mwili, viungo vya mwili pamoja na nguvu ya kuchangamka vyote vinahusika na "Xila". "Xila" ikionekana kuwa na nguvu kubwa zaidi, binadamu huwa na homa au mwepesi kukasirika. "Badagan" ni kitu kama ute mwilini mwa binadamu kikionekana kuwa baridi. Pindi "Badagan" haifanyi kazi sawasawa, binadamu ataonekana kuwa baridi na kuwa na ute mwingi.

TIBA MAALUMU ZA KIMONGOLIA

TIBA ZA KUTOA DAMU

Kupasua au kutoboa mshipa wa damu inayorudi kwa moyo ili kutoa damu yenye matatizo.

TIBA YA KUFYONZA NGOZI KWA CHUPA

Tiba hiyo hufanyika kwa chupa ya kufyonza ngozi ya mwili kwa chupa na kutoa damu kwa pamoja. Kwanza kuchagua sehemu moja ya kufyonza ngozi, baada ya kuondolewa chupa ya kufyonza, kutoboa ngozi iliyoinuka ya sehemu hiyo kwa sindano, kisha kutumia chupa ya kufyonza tena ili kutoa damu yenye matatizo pamoja na maji ya rangi ya manjano. Tiba hiyo inaleta matokeo haraka wala haina uchungu na hatari.

Mbali na hayo, tiba za kimongolia kuna mbinu nyingine za kuwaponya wagonjwa zikiwa ni pamoja na kutumia maziwa ya farasi yaliyoumuka (kwa hamira), akyupancha na kumia mikono kurejesha mfupa ulioteguka.

Tiba za Kiuigur

HALI YA TIBA ZA KIUIGUR

Zamani za kale Xinjiang ilikuwa ya eneo la magharibi. Urahisi wa mawasiliano kati ya sehemu ya magharibi na sehemu ya mashariki yalichangia maendeleo ya biashara na maingiliano ya kiutamaduni, tiba na dawa za sehemu ya mashariki na magharibi zilikuweko kwa wakati mmoja katika Xinjiang, sehemu ya kati ya Asia ya kati, hali ambayo ilihimiza maendeleo ya tiba na dawa za sehemu hiyo. Mfumo wa tiba za kiugur uliendelezwa kwa uzoefu wa tiba na kujifunza kutoka uzoefu wa tiba wa sehemu za mashariki na magharibi.

Tiba na dawa za kiuigur zinachukua nafasi kubwa katika tiba za jadi za kichina, hivi sasa aina 202 za dawa za kiuigur zimeorodheshwa kuwa dawa za ngazi ya kitaifa za China. Katika mkoa wa Xinjiang, ambayo imekuwa moja ya sehemu nne zenye idadi kubwa ya wazee wenye umri wa miaka mingi duniani, tiba na dawa za kiuigur imeenea kila mahali. Dawa za miti-shamba zinazoota kwenye milima yenye theluji, jangwa na mbuga zinafanya kazi ya kipekee katika tiba za kichina.

Tiba za Jadi za Kikorea

HALI YA TIBA ZA KIKOREA

Tiba za jadi za kikorea ni mfumo wa tiba za jadi zilizoanzishwa juu ya msingi wa utamaduni wa kikorea na kujumuisha uzoefu wa kuzuia maradhi na kutibu wagonjwa. Toka zamani za kale, kabila la wakorea lilikuwa maingiliano ya kirafiki ya muda mrefu na kabila la wahan, utamaduni na tiba za makabila hayo mawili pia yaliingiliana tokea zamani.

CHANZO CHA TIBA ZA KIKOREA

Tiba za kikorea zina sehemu mbili ambazo ni dawa za kabila la wahan na dawa za kikorea.

Kutokana na kuwa tiba za kikorea zimeingiza elimu ya tiba na dawa za jadi za kichina, hivyo tiba za kikorea zinatumia dawa za jadi za kichina kama silaha za kabila la wakorea kupambana na maradhi. Kwa mfano, kitabu kijulikanacho kwa "Dawa za Sixiang", dawa zote zilizoelezwa ni za kichina ambazo ni za aina 271, na dawa zilizoelezwa katika kitabu kijulikanacho kwa "Tiba za Mashariki" ni za makundi makubwa 15 zenye aina zaidi ya 1,400. Matumizi ya dawa za kabila la wakorea yamekuwa na historia ya miaka mingi, hususan baada ya mwaka 1949 matumizi ya dawa zilizokuwa zinatumika na wakorea kutibu wagonjwa zilikusanywa na kuandikwa katika kitabu cha dawa.

Tiba za Jadi za Kabila la Wazhuang

HALI YA TIBA ZA KABILA LA WAZHUANG

Kabila wa wazhuang linachukua nafasi ya kwanza kwa wingi wa idadi ya watu miongoni mwa makabila madogo madogo nchini China. Tiba za jadi za kabila la wazhuang ziliundwa hatua kwa hatua baada ya enzi ya Tang zikijifunza elimu ya tiba za jadi za kabila la wahan.

Maendeleo ya tiba za jadi za kabila la wazhuang katika zamani za kale ingawa hayakuandikwa kwa maneno, lakini yamejulikana hadi vizazi vya baadaye kutokana na njia za waalimu kuwafundisha wanafunzi na watu kuambiana. Vyeti vya mseto wa dawa za jadi za kabila la wazhuang vilienea miongoni mwa watu wa kabila la wazhuang, ambavyo vimechangia maendeleo ya tiba za jadi za kichina.

DAWA ZA JADI ZA KABILA LA WAZHUANG

Dawa za kabila la wazhuang ni dawa za zinazoendelea katika kabila hilo, ambazo bado hazijakamilika na kuwa na mfumo wake pekee. Watu wa kabila la wazhuang wanaishi katika sehemu ya joto upande wa kusini wa milima ya Qinling, ambapo kuna rasilimali kubwa ya wanyama na mimea, tena watu wa kabila hilo wanapenda kula nyoka, panya na ndege wa milimani, hivyo dawa nyingi za jadi za kabila la wazhuang zinatokana na wanyama na mimea.

Umaalumu wa dawa za jadi za kabila la wazhuang ni kuponya wagonjwa waliopatwa na sumu zikiwa ni pamoja na za nyoka, wadudu, chakula, dawa, mishale yenye sumu na mchango wa tumboni.

Tiba za Kabila la Wahui

Tiba za kabila la wahui ni mchanganyiko wa tiba za jadi za kichina na tiba za kiislamu. Katika maendeleo ya miaka mingi, tiba za kabila la wahui zimekuwa na mbinu zake za kipekee, ambazo ni dawa kuchanganywa na chakula. Kwa mfano, wahui wanachanganya mafuta ya ufuta na Glauber's salt kutibu ugonjwa wa kutokuwa na choo ( constipation) .

Tiba za Jadi za Kabila la Wamiao

Tiba za jadi za kabila la wamiao zinaona kuwa sumu, udhaifu, jeraha, chakula kulundikana tumboni, vijidudu na wadudu ni aina 6 za vitu vinavyoathiri afya ya watu na kuwafanya kuugua ugonjwa.

Nyingi za dawa za jadi za kabila la wamiao zinatengenezwa kutokana na mimea, wanyama na aina chache za madini. Kutokana na takwimu zisizokamilika, hivi sasa dawa za jadi za kabila la wamiao zimefikia aina zaidi ya 1,500, aina 200 kati ya hizo zinatotumika mara kwa mara. Dawa za jadi za kabila la wamiao zinapatikana kwenye milima ya Miaoling, Wumeng na Wuling. Katika miaka ya karibuni kwenye maeneo wanayoishi watu wa kabila la wamiao vimeanzishwa vituo vya uzalishaji wa dawa za jadi.


1 2 3 4 5 6 7