Tarehe 16 mwezi Oktoba, China ilifanikiwa kurusha angani chombo cha safari za anga kilichobeba binadamu. Leo katika kipindi hiki tunawaletea habari hizo. Chombo cha Shenzhou cha China kinachobeba binadamu, kimetengenezwa kwa sayansi na tekinolojia ya kiwango cha juu, na kina umaalumu mwingi wa kipekee kikilinganishwa na vyombo vya anga ya juu vya kisasa vya nchi nyingine duniani.
Chombo cha Shenzhou kinaundwa na vyombo vidogo vitatu vya kuruka kwenda kwenye mhimili, kurejea duniani, uendeshaji na kipande cha nyongeza, kina jumla ya urefu wa mita 8.86 na uzito wa kilo 7,790, na ni chombo chenye nafasi kubwa zaidi ya kutumika ulimwenguni kwa hivi sasa. Wanaanga wanaweza kufanya shughuli zao bila tatizo lolote, wanaweza kuondoka kwenye viti vyao, na kuingia katika chombo cha kuruka kwenye mhimili kwa kupita kwenye mlango wake, na kufanya majaribio ya aina mbalimbali ya kisayansi.
Kwenye vyombo vya hivi sasa vya nchi za nje, wanaanga baada ya kutekeleza majukumu yao na kurejea duniani kwa kutumia vyombo vidogo vya kurejea, vyombo vile vya kuruka kwenye mihimili yake, vinabaki angani na kuwa takataka kwenye anga yao juu. Lakini betri ya inayotumika nguvu ya jua iliyoko katika mabawa ya chombo kidogo cha kuruka kwenye mhimili wake, inaweza kutoshaleza mahitaji yake ya umeme kwa muda wa zaidi ya nusu mwaka, na kina weza kuendelea kutekeleza majukumu yake ya majaribio katika anga ya juu na majukumu ya upimaji juu ya sayari na dunia, kikiwa kama satelite moja ya sayansi na tekinolojia.
Kabla ya kurushwa angani kwa vyombo vya Urusi ya zamani na Marekani, vilikuwa vikifanyiwa majaribio mara nyingi ya kubeba kima, mbwa au nyani, ili kuthibitisha usalama wa mfumo wa kuhakikisha hifadhi ya uhai. Lakini kwa nini wanyama hawakuchukuliwa katika majaribio ya chombo cha anga cha China?
Msanifu mkuu wa chombo cha Shenzhou, Bw Chi faren alitaja sababu tatu, ya kwanza ni kwamba mfumo wa uhai wa wanyama ni tofauti na ule wa binadamu, hivyo hata data zilizopatikana siyo za uhakika sana; Pili, wanyama akiwemo kima, baada ya kuwekwa katika chombo cha anga ya juu, huwa hawatulii kwenye viti vyao, na ni rahisi kusababisha ajali; Tatu, China imeshakuwa na teknolojia iliyoendelea zaidi ambayo inaweza kufanya majaribio kwa zana zinazofanana na hali ya uhai wa binadamu na kuhifadhi data mbalimbali za kuruka kwenye anga ya juu ya bina damu.
|