Mtu mashuhuri wa China ya kale Cao Cao na mashairi yake 2008/11/20 Kipindi cha Jian An kilichoanzia mwaka 196 hadi mwaka 220 mwishoni mwa Enzi ya Han Mashariki ni kipindi muhimu katika historia ya China. Katika kipindi hicho walijitokeza washairi wakubwa kama Cao Cao, Cao Pi na Cao Zhi, ambao walichangia ustawi wa fasihi ya China na kuipeleka katika kipindi kipya cha maendeleo
|
Tamasha la kimataifa la michezo ya sanaa lafanyika mjini Shanghai 2008/11/14 Tamasha la 10 la kimataifa la michezo ya sanaa linafanyika katika mji wa Shanghai, mji mkubwa uliopo mashariki mwa China. Wasanii kutoka Australia, Canada, Japani, Marekani, Ujerumani, Misri na nchi nyingine wamekusanyika huko kwa furaha. Katika muda wa mwezi mmoja wasanii hao watafanya maonesho zaidi ya 52 ya michezo ya sanaa.
|
Watu wa fani mbalimbali nchini China wamkumbuka mwongozaji mkubwa wa filamu Bw. Xie Jin 2008/11/06 Hivi karibuni mwongozaji mkubwa wa filamu wa China Bw. Xie Jin amefariki dunia kutokana na ugonjwa akiwa na umri wa miaka 85. Siku hizi watu wa fani mbalimbli nchini China kwa namna moja au nyingine wanafanya maombolezo ya kumkumbuka mwongozaji huyo wa filamu aliyetoa mchango mkubwa katika mambo ya filamu.
|
Utenzi wa kwanza katika historia ya fasihi ya China "Tausi Arukia Kusini Mashariki" 2008/10/30 "Tausi Arukia Kusini Mashariki" ni utenzi wa kwanza kabisa katika historia ya fasihi ya China, na ni moja kati ya maandishi maarufu ya fasihi ya China. Utenzi huo ulitokea katika kipindi cha Enzi ya Kusini iliyoanzia mwaka 420 hadi 589, asili yake ilikuwa ni utunzi miongoni mwa wenyeji katika Kipindi cha Jian An kilichoanzia mwaka 196 hadi mwaka 220 na baadaye ulirekebishwa katika muda mrefu. Utenzi huo una beti zaidi ya 350 zenye maneno zaidi ya 1,700, mambo yanayoelezwa ni hadithi ya mapenzi yanayosikitisha iliyotokea katika zama za kale nchini China.
|
Nyimbo zakuvutia usitake kuondoka mkoani Ningxia China 2008/10/16 Mliosikia ni wimbo wa kale unaoenea sana mkoani Ningxia nchini China. Wimbo kama huo unapewa jina la "Hua" maana yake ya kichina ni maua. Wimbo huo ambao unaimbwa kwa miaka mingi miongoni mwa wenyeji unawavutia watu wengi.
|
Mabadiliko makubwa ya uchapishaji wa vitabu katika miaka 20 iliyopita nchini China 2008/10/09 Kuanzia tarehe mosi mpaka tarehe 4 Septemba tamasha la 15 la kimataifa la vitabu lilifanyika katika mji wa bandari Tianjin. Miaka 22 imepita tangu tamasha hilo lilipoanzishwa mwaka 1986 mpaka sasa, tamasha hilo limekuwa moja ya matamasha manne makubwa ya kimataifa duniani.
|
|