Nchini China, kasi ya ukuaji wa uchumi wa eneo la magharibi ni ya polepole kuliko ule wa eneo la mashariki, hata idadi ya watu wa eneo la magharibi ni ndogo kuliko ile ya mashariki, lakini katika eneo la magharibi kuna vivutio vingi vya utalii na utamaduni. Ili kuwasaidia wasikilizaji wetu kuijua hali ya eneo la magharibi ya China, kuanzia leo tunawaletea makala 5 za chemsha bongo kuhusu vivutio vya utamaduni na utalii wa eneo la magharibi ya China katika kipindi hiki cha sanduku la barua. Katika Makala ya kwanza ya leo tunawafahamisha hali ya jumla ya vivutio vya utalii katika eneo la magharibi ya China, kwanza tunatoa masuali mawili, tafadhali msikilize kwa makini na kukumbuka vizuri na baadaye msikilize makala yetu kwa makini. Suali la kwanza: Kuna sehemu ngapi zenye mandhari nzuri katika magharibi ya China zilizoorodheshwa kwenye kumbukumbu za mabaki ya kale ya maumbile na utamaduni duniani? Suali la pili: Tafadhali taja majina ya sehemu mbili zenye mandhari nzuri katika magharibi ya China.
Katika mgawanyo wa mikoa na miji mikubwa 34 ya China, 12 iko kwenye eneo la magharibi ya China, eneo hilo ni theluthi mbili ya eneo la jumla ya ardhi ya China. Eneo la magharibi ya China ni kubwa sana, ambapo hali ya kiasili ya huko ni yenye sura mbalimbali za kijiografia, na kuna mabaki mengi ya kihistoria katika eneo hilo. Aidha, watu wengi wa makabila madogomadogo ya China wanaishi katika eneo hilo, mila na desturi ya makabila hayo zinawavutia sana watu. Kutokana na hayo yote, sehemu 10 zenye vivutio vizuri zimeorodheshwa na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kwenye kumbukumbu za mabaki ya kale duniani. Bwana Wang Hongbing ni mtaalamu wa elimu ya utalii wa China ambaye alitembelea sehemu nyingi nchini na nje. Kuhusu vivutio vya utalii katika eneo la magharibi ya China, Bwana Wang alisema: Eneo la magharibi ya China lina vivutio vingi vya utalii vya sehemu za kiasili, kama vile milima, mito, mapango, mbuga, misitu, mahekalu, mabaki ya kale, na mila na desturi za makabila madogomadogo. Vivutio hivyo karibu vyote bado viko katika hali asilia ambayo inapendeza zaidi kuliko vingine vilivyotengenezwa kwa nguvu za kibinadamu. Vivutio hivyo vya utalii, kila kimoja kina mtindo wake pekee na kinatofautiana na vingine vyote, na hakipatikani katika sehemu nyingine nchini. Katika eneo la magharibi ya China, vivutio vya aina zote vinaonekana kwa maumbile ya kiasili, na watu wa makabila madogomadogo wanaonekana kuwa na mila na desturi mbalimbali tofauti. Dada Wang Yongchen ni mwandishi wa habari anayependa sana utalii, ametembelea sehemu nyingi nchini China, na amepata picha nzuri juu ya eneo la magharibi ya China. Anasema, siwezi kusahau sehemu ya chanzo cha mto Changjiang kilichoko eneo la magharibi ya China, nilipotembelea huko, niliwasikia wasichana wa uwanda wa juu wa huko ambao waliimba nyimbo maalum zilizoimbwa na wafugaji farasi, sauti ya nyimbo hizo ni ya juu sana, hata waimbaji wa kawaida hawawezi kuimba kwa sauti ya juu ya namna hii. Dada Wang alisema, alipotembelea mkoa wa Qinhai wa eneo la magharibi ya China alivutiwa sana na Ziwa Qinhai, kwenye ziwa hilo kuna kisiwa cha ndege; mkoani Qinhai pia kuna mahekalu kadhaa maarufu; na watu wa mkoa huo wanapenda zaidi kuimba nyimbo za kienyeji za ?Hua??. Na mbuga kubwa ya Mongolia ya ndani ya eneo la magharibi ya China inawavuta sana, ambapo kila ifikapo majira ya joto, tamasha kubwa la Nadamu hufanyika kwenye mbuga kubwa ya Mongolia ya ndani, kwenye mkutano huo mkubwa zaidi ya sikukuu ya wenyeji wa huko, watu wanaweza kunywa divai ya maziwa ya farasi, kula nyama ya kondoo kwa mikono, ambapo wasichana wa kabila la wamongolia wanaweza kukuimbia nyimbo za mbuga ya Mongolia ya ndani, na wewe utajiburudika kwa starehe sana. Katika Wilaya ya Lijiang kuna bendi moja ya muziki wa kale, bendi hiyo inaundwa na wazee wengi wa kabila la wanaxi, wazee hao wanapiga vinanda vya kale ambavyo havitumiki tena katika sehemu nyingine, wanapiga nyimbo za kale zilizotungwa miaka mia kadhaa iliyopita. Hivi sasa wazee hao wanapiga muziki siyo kwa ajili ya kujiburudisha, pia wanapenda kuwaonyeshea watalii utamaduni wa kale wa sehemu hiyo. Katika eneo la magharibi ya China, hali ya mawasiliano inaboreshwa siku hadi siku, watalii wa nchini na nje wanaweza kufika huko kwa rahisi kutembelea kaburi la mfalme Qin Shihuang aliyekuwa mfalme wa kwanza wa zamani wa China, na wanaweza kutembelea mashimo ya sanamu za ufinyanzi za askari na farasi wa mfalme Qin; mji wa kale Lijiang mkoani Yunnan, Pango la Mogao la mkoani Gansu, Kasri la Budara la mkoani Tibet, Bonde la vijiji 9 vya kitibet mkoani Sichuan na kwengineko, sehemu hizo zote zenye vivutio vya utalii zinawavutia sana watalii wa nchini na nje. Ndugu wasikilizaji, sasa tunatoa masuali mawili , la kwanza: Kuna sehemu ngapi zenye mandhari nzuri katika magharibi ya China zilizoorodheshwa kwenye kumbukumbu za mabaki ya kale ya maumbile na utamaduni duniani? Suali la pili: Tafadhali taja majina ya sehemu mbili maarufu zenye mandhari nzuri katika magharibi ya China.
|