Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2003-12-15 15:33:53    
Makala ya pili ya chemsha bongo kuhusu vivutio vya
utamaduni na utalii wa eneo la magharibi ya China

cri
    Kila mtu aliyetembelea Tibet kwa mara ya kwanza huvutiwa na kusisimka sana mbele ya kivutio cha hali ya kiasili ya huko. Huko Tibet, anga ni ya buluu inayopendeza kweli, mawingu yako chini karibu unaweza kuyagusa, mlima wa theluji unaonekana kama santa monika mwenye ukimya, utukufu na uzuri, na ziwa chini ya mlima wa theluji linawavutia sana watu hata wakiangalia ziwa hilo wanaweza kujisikia kama wanatakasika. Aidha, maisha ya watibet na utamduni wa kitibet una vivutio vingi zaidi.

    Kila asubuhi, jua linapochomoza, watalii huweza kuamshwa na milio ya kugongana ya vyombo vya kuongozea sala, ambapo wanaweza kuona kuwa waumini wa Tibet wanaume kwa wanawake, wazee kwa watoto wanazungusha vyombo vya kuongozea sala, huku wakitafakari na kutembea taratibu.

    Waumini hao wa dini ya Buddha ya kitibet ni mahujaji. Huko Tibet, watu wengi kabisa wanaamini dini ya Budha ya kitibet. Dini ya Budha ilienea huko Tibet kutoka China bara, Nepal na India kuanzia karne ya 7, ikapatana na dini Ben ya kienyeji ya huko ikawa dini ya Budha ya kitibet ambayo ni dini inayoaminiwa na watu wengi zaidi wa Tibet.

    Kama ukiishi na kutalii huko sehemu ya Tibet, utasikia mara kwa mara sauti ya kusoma msahafu kama uliosikia hivi sasa, na usielewe hata kidogo, pia utaweza kuvutiwa sana na utiifu na udhati ulio wa kujisahau walio nao waumini dini.

    Bwana Zhang Xiaoping mwenye umri wa miaka 60 ni mwandishi wa habari wa Beijing, amekwenda Tibet mara 17, safari moja ilikuwa ya muda mrefu, ambapo alifanya kazi huko kwa miaka 6. Bwana Zhang aliwahi kufika sehemu nyingi huko Tibet, na alimwona mtibet mmoja. Kila alipotaja Tibeit huonekana na hisia nyingi juu ya Tibet.

    Anasema, niliwahi kwenda Tibet kwa mara zaidi ya 10, Tibet daima inaonekana ni dunia iliyojaa mwanga wa jua, uhai na rangi mbalimbali. Mbele yangu, Tibet ni kama vitabu vya Encyclopaedia ambavyo huwezi kuvimaliza. Na huwa ninavutiwa zaidi na watibet wanaoabudu kwa udhati na utii wao kwa miungu ya mbinguni, ardhini na maumbile, wanaonekana kama ni watoto na wajukuu wa dunia asilia na kujaliwa nayo. Hivyo kila mmoja wao anaishukuru dunia asilia.

    "Utenzi wa mfalme Gesal" ni shairi maarufu zaidi la kabila la watibet, utenzi huo ni mrefu zaidi wa kihistoria duniani. Inasemekana kuwa Gesal alikuwa mungu mmoja peponi, alikuja duniani kwa ajili ya kuwasaidia watu kuangamiza mashetani, ambapo alikuwa shujaa mwenye mbinu nyingi za kuwashinda mashitani na aliwapenda raia wa kawaida, na alirudi peponi baada ya kukamilisha jukumu lake. Katika miaka kumi kadhaa iliyopita, serikali ya China iligharamia fedha nyingi na kutumia nguvu kubwa kuratibu "utenzi wa mfalme Gesal", na kuepusha utenzi huo wenye thamani kubwa kupotea duniani.

    Bwana Wangdui anaishi sehemu iliyoko karibu na Kasri ya Budara mjini Lahsa, anapenda sana fasihi, kila mara anatunga shairi na maneno ya nyimbo, anapotaja utenzi wa mfalme Gesal anabubujika kama wasanii walivyo.

    Anasema, "Utenzi wa mfalme Gesal" ni vitabu vya elimu kamili (Enclopaedia) vya kabila la watibet, nyimbo nyingi kuhusu utenzi huo ni za kienyeji zinazowafurahisha watibet. Utenzi huo umeelezea sherehe za dini, mambo ya kijeshi, mila za jamii, mfumo wa ndoa na desturi za maisha za watibet wa zama za kale. "Utenzi wa mfalme Gesal" unapendwa na watibet, na tafsiri zake za kirusi, kiingereza, kifaransa, kihindi na kimongolia zimeenea katika nchi na sehemu mbalimbali.

    Katika sikukuu ya Xuedun ya kabila la watibet, maana ya Xuedun ni mtindi hivyo tunasema sikukuu hiyo pia inaitwa sikukuu ya mtindi, tamasha kubwa hufanyika mwazoni mwa Julai kwa kalenda ya kitibet yaani mwishoni mwa Agosti na mwanzoni mwa Septemba ya kalenda ya kimataifa. Katika sikukuu hiyo, wasanii wanafanya maonyesho ya opera ya kitibeit yenye historia ya miaka mia kadhaa, ambapo watibet walikunywa mtindi huku wakitazama maonyesho na kujiburudisha.

    Bwana Basanglubu ni mkuu wa Idara ya utafiti wa makabila ya Taasisi ya sayansi ya jamii ya Tibet, anapenda sana kutazama maonyesho ya opera ya kitibet tangu alipokuwa mtoto. Na amefanya utafiti wa utamaduni wa Tibet kwa miaka mingi. Kuhusu utamaduni wa Tibet Bwana Basangrubu anasema:

    Utamaduni wa kabila la watibet unang'ara tangu enzi na dahari, nao ni kama lulu kwenye hazina ya utamaduni wa taifa la China. Mbali na dini Ben ya kienyeji huko Tibet na dini ya Budhaa ya kitibet, utamaduni wa kienyeji wa Tibet kama vile opera ya kabila la watibet, nyimbo za kienyeji na michoro ya kitibet, yote hayo ni yenye mitindo pekee.

    Ndugu wasikilizaji, ni vigumu kumfahamisha hali ya Tibet kwa kipindi hiki cha dakika 8 hivi, ukipata nafasi ya kuitembelea Tibet, utashuhudia vivutio vyote vya Tibet.

    Sasa tunatoa masuali: Suali la kwanza: Watu walio wengi wa kabila la wa-Tibet ni waumini wa dini gani? Suali la pili: Shairi la historia lililo maarufu zaidi la kabila la watibet linaitwaje?