Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2003-12-15 15:35:40    
Makala ya tatu ya chemsha bongo kuhusu vivutio vyautamaduni na utalii wa eneo la magharibi ya China

cri
    Tukifuata mji wa kale Xian wa China kuelekea kaskazini ya magharibi ya China, njiani tunaweza kuona wanaume wengi wanaovaa kofia nyeupe mviringo na mikahawa mingi yenye chapa ya kiislamu, hali hii inaonesha kuwa, tumeingia sehemu kubwa wanakoishi waislamu wa China. Wanaume wanaovaa kofia nyeupe mviringo yaani kofia ya kiislamu ni wa kabila la wahui, kabila la wahui ni kabila mojawapo kati ya makabila 10 yanayoamini dini ya kiislamu nchini China. Watu wengi wa makabila hayo 10 wanaishi katika eneo la kaskazini magharibi ya China, miongoni mwao watu wa kabila la wahui na wawiur ni wengi zaidi kuliko makabila mengine.

    Watu wa kabila la wahui wanaishi katika mkoa ujiendeshao wa kabila la wahui la Ninxia, mkoa wa Qinhai na mkoa wa Gansu, na watu wa kabila la wawiur wanaishi katika mkoa ujiendeshao wa Xinjiangwiur. Watu wa Makabila mengine ya wakhazak, wakerkezhi, wauzhibik na watajik pia ni waumini wa dini ya kiislamu. Makabila hayo 10 yanaamini dini ya pamoja ya kiislamu, lakini urithi wa utamaduni na desturi za maisha ya kila kabila hilo ni tofauti.

    Bwana Huang Tinghui wa idara ya elimu ya makabila madogomadogo ya Taasisi ya sayansi ya jamii ya China anashughulikia utafiti wa utamaduni wa kiislamu. Alisema kuwa kama marafiki zetu wa nchi mbalimbali wanataka kuja China kujionea utamaduni wa kiislamu, wangeweza kwenda kwanza mikoa ya Ninxia na Gansu kufahamishwa maisha na utamaduni wa huko, halafu kwenda mkoa wa Xinjiang. Anasema: Kutokana na tofauti ya eneo la kijioglafia, utamaduni wa kiislamu wa China unagawika katika mifumo miwili. Mfumo mmoja unawakilishwa na utamaduni wa kabila la waxinjiangwiur, na mwingine unawakilishwa na utamaduni wa kabila la wahui. Utamaduni wa kabila la wahui ulitokana na upatanishaji wa utamaduni wa kiislamu na utamaduni wa kabila la wahan; na utamaduni wa Xinjiang ulitokana na upatanishaji wa utamaduni wa kiislamu na utamaduni wa kitujue.

    Kwanza tujionee huko Yinchuan, mji mkuu wa mkoa ujiendeshao wa kabila la wahui la Ninxia.

    Huko Yinchuan, kuna msikiti mkubwa maarufu uitwao Nanguan. Umbo la Msikiti la Nanguan linaonekana kuwa na mtindo dhahiri wa kiarabu, msikiti huo ulijengwa katika zama za miaka ya 80 ya karne iliyopita. Ndani ya ukumbi mkubwa wa msikiti huo, hakuna vinyago au michoro mingi, lakini ndani kuna vyumba vya kuogea, ukumbi wa swala, vyumba vya mapumziko na sebule. Katika siku zisizo na ibada, msikiti wa Nanguan huwapokea watu wanaokuja kutembelea.

    Msikiti huo ni kituo cha waiislamu wanaofanya shughuli za kidini, pia ni kituo chao cha kufanyia shughuli nyingine za kijamii. Huu ni umaalum wa misikiti ya kichina, vilevile ni umaalum wa utamaduni wa kiislamu wa China.

    Katika mchakato wa maendeleo ya utamaduni wa kabila la wahui, utamaduni huo ulipokea fikra fulani ya kiconfutius ya kabila la wahan la China , hivyo wachambuzi waliona kuwa, kutokana na fikra hiyo, watu walijizuia vitendo vyao, waumini wa dini ya kiislamu wa kabila la wahui hawajui sana kuimba nyimbo na kucheza ngoma kama watu wa kabila la wawiur walivyo.

    Katika mkoa ujiendeshao wa Xinjiangwiur, popote unapokwenda, unaweza kusikia nyimbo za furaha za aina hiyo. Miongoni mwa makabila 56 ya China, kabila la wawiur linatambulika kuwa ni kabila moja kati ya makabila kadhaa yanayopenda na kujua zaidi kuimba nyimbo na kucheza ngoma. Tofauti na wanaume wa kabila la wahui wanaovaa kofia ndogo nyeupe mviringo, wanaume wa kabila la wawiur wanapenda kuvaa kofia yenye pembe 4 ya rangi ambayo kijani ni rangi yake kuu.

    Muziki wa "Mukam 12"ni muziki maarufu wa kabila la wawiur, hili ni jina la jumla la muziki wa sehemu 12 , muziki huo pia unahusu ngoma mbalimbali. Muziki huo wa seti moja ulitungwa kuanzia karne ya 12, na uliwahi kuenea katika Asia ya kati na uwanda wa juu wa Iran katika karne ya 13. Baadaye, Mukam, neno hilo la kiarabu limekuwa jina la jumla la seti hiyo ya muziki, hata jina la kila sehemu ya muziki huo ni la lugha ya kiarabu au ya kiajemi.

    Katika mkoa wa Xinjiang, msikiti wa Ld Kah Mosque ni mkubwa zaidi na maarufu zaidi ulioko mjini Kashi, kusini mwa Xinjiang. Msikiti huo ulijengwa miaka zaidi ya 500 iliyopita, msikiti huo pia ni mkubwa zaidi kuliko mingine nchini China, na unajulikana sana kwenye kanda ya Asia ya kati na ya kusini. Wahusika walifahamisha kuwa, Ayatollah Seyyed Ali Khamenei aliyekuwa rais wa Iran na rais Ahmet Necdet Sezer wa Uturuki waliwahi kufanya ibada kwenye msikiti huo.

    Ndani ya Msikiti huo kuna vyumba 36 vya kusomea msahafu. Kwa kawaida, kila siku waumini dini wapatao elfu 2 au 3 wanafanya ibada huko, na kila ijumaa, waumini elfu 6 au 7 wanafanya ibada kwenye msikiti huo, baada ya kufanya ibada, waumini wote waume kwa wake, wazee kwa watoto hufanya shamrashamba kwenye uwanja mbele ya msikiti.

    Katika eneo la magharibi ya China, mbali na utamaduni wa kiislamu wa kichina, pia kuna vivutio vingi vya maumbile na mabaki mengi ya kale ya utamaduni, ambapo kuna jangwa kubwa la pili duniani Taklamagan, mbuga kubwa, milima mirefu na maziwa makubwa, pamoja na gofu la Loulan na gofu la Niya yanayojulikana duniani.

    Sasa tunatoa masuali mawili, Suali la kwanza: Katika eneo la magharibi ya China, ni makabila mangapi yenye waumini wa dini ya kiislamu? Suali la pili: Msikiti mkubwa zaidi kuliko mingine nchini China unaitwaje?