Kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, siku hizi kazi na maisha ya watu yanabadilika sana kutokana na matumizi ya mashine mbalimbali zenye teknolojia za hali ya juu. Mashine hizo zenye uwezo mkubwa zinawasaidia binaadamu kurahisisha kazi na kufanya maisha yawe ya furaha zaidi. Leo katika kipindi hiki tunawaletea maelezo kuhusu jambo hilo.
Bibi Ganna ana umri wa miaka 24, yeye ni Mwongozaji wa kipindi kimoja cha televisheni. Kila siku hawezi kufanya kazi yoyote bila msaada ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu.
Saa tatu asubuhi, Bibi Ganna anafika ofisini kwa wakati kama kawaida, kwanza anawasha kompyuta yake na kuangalia barua pepe yaani E-mail.
Kila siku Bibi Ganna anapata barua nyingi kwenye mtandao wa Internet, watu kutoka sehemu mbalimbali wanamwandikia barua kumwuliza hali mpya ya wachezaji nyota wa filamu au waimbaji nyota, lini filamu mpya zitaanza kutengenezwa n.k Bibi Ganna anasema:
" Barua pepe za watazamaji zinanisaidia kutambua mahitaji ya watu kwa haraka sana, na kutokana na barua hizo, naweza kupanga na kutengeneza vipindi vya televisheni kwa urahisi na kasi zaidi. Mbali na hayo, watu kadhaa waliniambia vipindi vyetu vina makosa gani, naweza kuviboresha kwa haraka iwezekanavyo. Baada ya kuangalia barua pepe kutoka kwa watazamaji, mimi hutafuta habari za karamu kwenye mtandao wa internet, kwa mfano filamu au vipindi vya televisheni gani vitatangazwa, nani atatangaza album mpya n.k. Kwa msaada wa mtandao wa internet, taz yangu imeongezeka sana, watu wanaweza kupata habari mpya wa karamu kwa haraka sana. kwa kawaida, kipindi kimoja kinaweza kukamilishwa katika siku moja. Lakini zamani kilihitaji siku mbili au zaidi."
Bibi Ganna alisema kuwa, kila anapokwenda, yeye hubeba Kompyuta yake ya mkononi. Kwa kuwa, katika sehemu kadhaa ni vigumu kutembelea mtandao wa internet, hulazimika kutumia simu yake ya mkononi kuinganisha kompyuta ya mkononi kwenye mtandao wa internet. Kwa kutumia njia hiyo, anaweza kutembelea mtandao wa internet kila mahali.
simu ya mkononi ya zamani simu ya mkononi ya kisasa
Bibi Ganna ana simu nzuri ya mkononi. Mwaka moja uliopita, vioo vya simu nyingi za mkononi vilikuwa ni vya rangi nyeusi na nyeupe ambapo kengele ni Rahisi sana lakini hivi sasa, watu wanatumia simu za mkono zenye vioo vya rangi, na kengele ni kama muziki safi
Mbali na hayo, simu ya mkononi ya kisasa inaweza kufanya kazi nyingi zaidi. Kwa mfano kucheza michezo, kutembelea mtandao wa internet, kurekodi sauti, kupiga picha za video n.k. vijana wengi wanapiga picha na kuzituma kwa marafiki zao kwa simu za mkononi. Bibi Ganna ana rafiki mmoja ambaye alitembelea Kenya mwaka uliopita. Alipokuwa katika mbuga ya Masai Mara rafiki yake huyo alimpiga picha simba mmoja halafu aliituma picha hiyo kwa Bibi Ganna aliyeko nchini China kwa simu ya mkononi. Bibi Ganna alipata picha hiyo baada ya sekunde kadhaa tu, alifurahi na kushangaa sana.
Wakati wa chakula cha mchana, Bibi Ganna anapenda kuangalia filamu kwa kompyuta yake ya mkononi. Ingawa kompyuta hiyo ni ndogo kuliko televisheni, lakini inaweza kuonesha picha na sauti nzuri. Ukikaa mbele ya kompyuta hiyo ni kama unaangalia filamu katika ukumbi.
Kompyuta ya mkononi
Hivi sasa katika vyuo vikuu vya China, wanafunzi wanapenda kutumia kompyuta ya mkononi kufanya mambo mbalimbali. Kwa mfano, kuandika kazi za nyumbani, kucheza michezo ya kompyuta, kuangalia filamu, kutembelea mtandao wa internet n.k. Na katika makampuni mbalimbali, wafanyakazi wanapenda kufanya mambo ya biashara kwa kopyuta ya mkononi, kama hawakumaliza kazi ofisini, wanaendelea kufanya kazi zao nyumbani.
Alasiri, kwenye njia ya kumwuhoji mwimbaji mmoja, Bibi Ganna alisikiliza muziki kwa mashine moja ndogo. Mashine hiyo inayoitwa MP3 ni kama kiboksi cha kiberiti, inaweza kuchukua nyimbo 30 zenye ubora wa CD. Bibi Ganna aliniambia kuwa, alipenda kuchukua nyimbo kutoka kwenye mtandao wa internet, na kuziweka katika katika mashine hiyo ya MP3. Sasa vijana wa China wanapenda kusikiliza muziki kwa mashine hiyo. Wanatundika MP3 mbele ya kifua kama mkufu, wanawake hasa wanaiweka Mp3 kama mashine ya lazima katika maisha. Mbali na hayo, vifaa kama kamera ya kitarakimu, kompyuta ya mkononi, kamusi ya mkononi n.k vinafurahiwa sana na vijana.
Bibi Ganna alisema kuwa, kwa mfano katika kazi yake, vyombo vyote alivyotumia ni mashine za kitarakimu, kamera ya video ya kitarakimu, mashine ya kurekodi sauti ya kitarakimu, na kituo cha kitarakimu cha utengenezaji wa vipindi vya televisheni n.k. bila msaada wa mashine ya kitarakimu, hawezi kufanya kazi yoyote.
Teknolojia ya hali ya juu inawasaidia watu kufanya kazi nyingi na kuleta furaha kwa maisha ya binadamu. Tunaamini kwamba, katika siku za usoni, watu watakuwa na wakati zaidi kufurahia maisha mazuri.
Idhaa Ya Kiswahli 2004-02-04
|