Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-02-24 14:23:15    
"Nina imani kubwa na maendeleo ya uchumi wa China."----Ofisa wa habari wa Idara ya Takwimu ya China, Bw. Yao Jingyuan.

cri

    Ofisa wa habari wa idara ya takwimu ya China Bw. Yao Jing-yuan, amefanya kazi kwa miaka mingi katika eneo la uchumi nchini, amewahi kuteuliwa kuwa meya na mkurugenzi mkuu wa idara ya takwimu ya mji mmoja. Alipokuwa akihojiwa na mwandishi wetu wa habari, alikuwa ametoka kwenye mkutano na waandishi wa habari.

    Bw. Yao Jing-yuan alisema kuwa "mwaka 2003, kasi ya ongezeko la uchumi wa China ilifikia 9.1%, hayo yalikuwa matokeo yasiyotazamiwa na watu wengi, lakini kwangu mimi, naona ni jambo lililotazamiwa". Ongezeko hilo ni la kasi kubwa, ambalo baadhi ya wataalamu walikuwa na mashaka kwamba ongezeko hilo la uchumi limekuwa kubwa kupita kiasi. Maoni yangu ni kwamba kwa ujumla uchumi wa China uko katika hali nzuri, na sababu ni kwamba kasi ya ongezeko na ubora wa uchumi vinakwenda sambamba. Licha ya hayo, hali ya uwekezaji, ununuzi na usafirishaji nje wa bidhaa pia vimeonesha kuwa uchumi wa China uko katika hali nzuri.

    Hata hivyo, Bw. Yao Jing-yuan alisema kuwa ingawa uchumi wa China ulikuwa na ongezeko la 9.1% mwaka jana katika hali ambayo uchumi wa China uliathiriwa na maafa ya kimaumbile na maambukizi ya ugonjwa wa SARS, lakini kulikuwa na matatizo ya kukosa uwiano katika mifumo ya uzalishaji mali, kati ya miji na vijiji na kati ya uwekezaji na ununuzi wa bidhaa.

    Kutokana na hali hiyo, Bw. Yao Jing-yuan alisema, "Endapo tunakosa mikakati sahihi kuhusu hali hiyo, na kushindwa kuchukua hatua imara, kasi hiyo ya ongezeko la uchumi wa China haitaweza kudumishwa. Hivi sasa tumeweka msimamo mpya wa maendeleo, yaani kukuza uchumi wa China kwa pande zote, na kupata maendeleo ya uwiano na ya uendelevu. Maendeleo ya uchumi ya uwiano ni muhimu, na pia ni njia ya kudumisha maendeleo katika hali nzuri."

    Bw. Yao amefanya kazi katika idara ya takwimu kwa miaka kadhaa, siyo tu kwamba yeye ni ofisa wa habari wa idara ya takwimu ya China, bali pia ni mwanauchumi wa idara ya serikali. Hivi sasa, karibu kila siku anashughulikia takwimu zinazotoka sehemu mbalimbali za nchini ambazo zimempa data mpya kwa kazi zake za kiuchumi. Watu wengi wanaona hesabu nyingi ni za kuchosha watu, lakini yeye haoni hivyo. Alisema, "Kila siku napambana na hesabu nyingi, sioni kama ni kitu cha kuchosha, bali naziona hesabu hizo ni kama ni manoti ya muziki. Nyakati fulani hesabu hizo zinanipa imani na furaha juu ya mustakabali wa maendeleo ya uchumi wa taifa, lakini katika baadhi ya nyakati, matatizo yanayooneshwa na hesabu hizo yananifanya kuwa na wasiwasi."

    Katika miaka ya nyuma, kulikuwa na wataalamu wengi wa nchini na wa nchi za nje ambao hawakuamini takwimu zinazopatikana kuhusu jumla ya thamani ya uzalishaji mali wa China, lakini Bw. Yao alisema, "Ukweli ni kwamba takwimu zetu ni sahihi na zinaonesha hali nzima ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China. Kwani pamoja na utekelezaji wa mageuzi na ufunguaji mlango, utaratibu wa takwimu umeungana ni ule unaofuatwa na nchi nyingine duniani. Kisayansi, takwimu zilizotoka idara ya takwimu ya China hazina matatizo na zimekubaliwa na umoja wa mataifa, benki ya dunia na shirika la fedha duniani."

    Bw. Yao alisema kuwa kuanzia mwaka huu, China imebadilisha utaratibu wa kupiga mahesabu na kutoa takwimu kuhusu thamani ya uzalishaji mali wa China. Kutokana na utaratibu mpya, takwimu za jumla ya thamani ya uzalishaji mali zilinatangazwa na China siyo ya uamuzi wa mwisho, bali zinarekebishwa mara kwa mara kwa kufuata desturi ya kimataifa. Aidha, China imebadilisha desturi ya kutangaza makadirio kuhusu jumla ya thamani ya uzalishaji mali wa nchini katika mwisho wa mwaka. Bw. Yao alisema kuwa marekebisho katika upigaji hesabu na utaratibu wa kutangaza yataongeza hali ya kuaminika na ukweli wa takwimu za kiuchumi zinazotangazwa na China.

    Katika ukuta wa sehemu ya wazi ofisini mwa Bw. Yao imetundikwa bendera moja ya China, na chini yake imewekwa kabati moja iliyojaa vitabu. Bw. Yao alisema kuwa akiwa ofisa wa habari, bendera hiyo inamkumbusha jukumu lake la kutoa habari ya kweli kwa umma kuhusu hali ya uchumi na maendeleo halisi ya China. Hivyo unapaswa kuongeza elimu mara kwa mara kwa kusoma vitabu ili kufanikisha kazi zake.

    Bw. Yao Jing-yuan anawajibika sana kwa kazi zake za uofisa wa habari. Anaona kuwa utaratibu wa kutoa habari ni sehemu moja muhimu ya ustaarabu wa kisiasa wa China. Akiwa ofisa wa habari wa idara ya serikali, kazi zake siyo kutoa habari peke yake, bali pia anapaswa kujenga daraja moja la mawasiliano kati ya serikali na wananchi.

    Maneno anayosema ofisa wa habari ni maoni ya serikali wala siyo maoni yake binafsi. Hivyo, anapaswa kuongeza elimu na kujiendeleza mara kwa mara; kwa upande mwingine, anapaswa kuvieleza vyombo vya habari maoni ya serikali ambavyo vitawaeleza wananchi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-02-24