Bwana Liu Dongsheng
Matokeo ya Tuzo Kuu ya Sayansi na Teknolojia ya China ya mwaka 2003 yalijulikana tarehe 20 mwezi Februari hapa Beijing. Mwaka huu wanasayansi wawili wa China walipata tuzo hiyo yenye heshima kubwa kabisa nchini China, nao ni mtafiti wa Taasisi ya mambo ya Jiolojia na fizikia ya ardhi ya China Bwana Liu Dongsheng na msanifu mkuu wa China wa Mradi wa kupeleka binadamu kwenye anga ya juu Bwana Wang Yongzhi. Rais wa China Hu Jintao alitoa tuzo hiyo kwa wanasayansi hao wawili.
Tangu kuanzishwa kwa tuzo ya sayansi na teknolojia ya China mwaka 2000, umuhimu wake mkubwa umekuwa ukifuatiliwa sana duniani. Sababu moja ni kwamba, zawadi ya tuzo hiyo inafikia Yuan milioni tano na kila mwaka ni wanasayansi wawili tu wanaoweza kupewa tuzo hiyo, ambao wanapaswa kutoa mchango mkubwa kabisa katika sayansi na teknolojia ya kisasa nchini China. Bwana Liu Dongsheng ambaye anajulikana kama 'mwana mazingira" nchini China.
Bwana Liu Dongsheng ana umri wa miaka 86, hadi sasa anakumbuka kuwa tarehe 20 mwezi Aprili mwaka 1980 kimbunga chenye mchanga na mavumbi kilitokea mjini Beijing. Maafa hayo yalileta mavumbi yenye milimeta 0.01 kwa mji wa Beijing. Bwana Liu Dongsheng alikadiria kuwa, kama maafa hayo yakitokea mara 10 kila mwaka, basi baada ya miaka milioni mbili, mji wa Beijing utafunikwa na mchanga wenye urefu wa mita 200.
Bwana Liu Dongsheng ni mwanasayansi wa ardhi, wanyama wa kale wenye uti wa mgongo, jiolojia na fizikia ardhi ambaye pia ni mwanachama wa taasisi ya jiolojia na fizikia ya dunia ya taasisi Kuu ya sayansi na teknolojia ya China. Alitumia muda wa miongo kadhaa kufanya utafiti katika uwanda wa juu wa udongo manjano. Aligundua kuwa, uwanda huo uliundwa kwa udongo manjano kwa miaka milioni mbili, na una matabaka ya udongo wenye mita 200. Alisema kuwa, kutafiti mambo ya zamani ni ufunguo wa kuelewa mambo ya sasa na ya siku zijazo.
Rais Hu Jintao wa China tarehe 20 mwezi Februari katika Jumba kuu la Umma alimpatia Tuzo Kuu ya sayansi na teknolojia ya China ya mwaka 2003 Bwana Liu Dongsheng. Tuzo hiyo ni ya heshima ya juu kabisa nchini China.
Bwana Liu Dongsheng alipokuwa kijana alikuwa mwanafunzi wa mwanasayansi maarufu wa wanyama wa kale wa China Bwana Yang Zhongjian. Katika wakati ule alikuwa akipendelea sana utafiti wa ardhi. Katika kazi yake ya miaka 60, Bwana Liu Dongsheng ametembelea sehemu nyingi duniani. Alipokuwa na umri wa miaka 74 alifanya utafiti katika kisiwa cha King George kilichoko kwenye ncha ya Kusini ya dunia; alipokuwa na umri wa miaka 79 alikwenda ncha ya kaskazini ya dunia kufanya utafiti, mbali na hayo ameshawahi kupanda mara nyingi milima yenye zaidi ya mita elfu 6 katika uwanja wa juu wa Qinghai na Tibet.
Mwanataaluma huyu wa Taasisi ya Uhandisi ya China alieleza historia ya mabadiliko ya hali ya hewa ya Uwanda wa juu wa udongo manjano katika miaka milioni 2.5 iliyopita.
uwanda wa juu wa udongo manjano ya China
Alisema kuwa, ardhi ya ncha ya Kusini ya dunia ilitoa habari za jiolojia kuhusu vipindi vinane vya zama za theluji vya miaka laki 7.5, na ardhi ya uwanda wa juu wa udongo manjano ya China ilitoa habari kuhusu vipindi 32 vya zama za theluji kwa miaka milioni 2.6. Hivyo rekodi kuhusu historia ya mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia inatoa uelewa mzuri zaidi kuliko ile ya ncha ya Kusini ya dunia.
Alisema kuwa, uwanda wa juu wa udongo manjano wa China ulisababishwa na upepo. Mbali na hayo makala zake zilitumiwa na wanasayansi wa nchi za kigeni kwa zaidi ya mara elfu 3. Kutokana na michango yake katika maeneo mbalimbali, mwaka 2002 alipewa tuzo ya Thaler, tuzo kubwa katika utafiti wa mazingira wa kimataifa.
nchi ya Kusini ya dunia
Alisema kuwa, "wanasayansi wanapenda udongo manjano ni kama wanamuziki wanaopenda piano. Wanamuziki wanaandika muziki mzuri kwa piano, na wanasayansi wanapata mafanikio ya sayansi na uvumbuzi mpya kutokana na udongo manjano.
Watu kadhaa wanamwita Bwana Liu Dongsheng "Baba wa udongo manjano", lakini yeye anajiita "mwana wa udongo manjano". Alisema kuwa, kazi yake ndogo ilikamilishwa kutokana na msingi wa wanasayansi wengi wa zamani, na wanafunzi wao walitafiti uhusiano wa udongo manjano na mabadiliko ya hali ya hewa kwa hatua zaidi, yeye alifanya kazi ya mpito tu.
Katika maisha ya kazi ya Bwana Liu Dongsheng, alitumia muda mwingi kufanya kazi katika maeneo yasiyo na watu kama vile jangwa, mapori na misitu. Mkewe Bibi Hu Changkang ambaye pia ni mtafiti wa Taasisi ya "wanyama wenye uti wa mgongo" na "binadamu wa kale". Alimsifu mume wake kuwa anafanya kazi kwa bidii sana. Katika uwanda wa udongo manjano, bila kujali kazi ni kubwa au ndogo, Bwana Liu Dongsheng alikuwa anafanya kazi yeye mwenyewe.
Bwana Liu Dongsheng alisema kuwa, "mimi sina akili za kipekee kuliko watu wengine, kuchapa kazi ni njia pekee ya kupata mafanikio."
Ingawa kazi ya utafiti wa sayansi na teknolojia na uchunguzi wa kisayansi ni ngumu na yenye taabu kubwa, lakini Bwana Liu Dongsheng anaona kuwa, kazi yake ni yenye furaha kubwa zaidi kuliko uchungu. Alisema kuwa, yeye ni mwana wa dunia, anapenda kuwa sehemu ya dunia.
Idhaa ya kiswahili 2004-03-10
|