Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-03-16 16:07:42    
Sanaa ya ukataji karatasi kwa kuigiza vyombo vya kale

cri

Vyombo vya kale vya kauri vya China vyenye historia ya miaka 4,000 kuanzia kipindi cha umajumui hadi mwisho wa enzi ya Qing, vinajulikana kwa umakini wake wa ufinyanzi, uzuri wa maumbo, upendezaji macho wa mabombwe na uangavu wa rangi. Baadhi ya vyombo hivyo vyenye thamani kubwa vinahifadhiwa kizazi baada ya kizaza, na kurithiwa mpaka leo, kwa mfano gudulia la kauri nyeupe na buluu la enzi ya Yuan lenye mabombwe ya "Xiao He anamkimbilia Han Xin usiku wa mbalamwezi" na mtungi wa kauri nyeupe na buluu wa enzi ya Ming wenye mabombwe ya "Chrysanthemum za kipupwe na ndege aimbae" ndio vyombo viwili vilivyorithiwa mpaka leo.
Kutokana na upendo wake kwa utamaduni wa kauri za China, zaidi ya miaka 7 iliyopita, Bwana Zhou Pingsen, mwalimu wa uchoraji wa shule ya msingi ya Dengfuxiang mjini Nanjing, alitoa wazo la kuonesha uzuri wa sanaa ya vyombo vya kale vya kauri kwa kukata karatasi. Alinunua picha nyingi na alifanya utafiti mara nyingi kuhusu vyombo halisi vya kauri vya kale, mwishowe alifaulu. Mpaka sasa ameshatengeneza  karatasi za kukatwa zenye mabombwe zaidi ya aina 100 ya vyombo vya kale vya kauri. Shirikisho la Wasanii wa Jiangsu liliwahi kufanya maonesho maalumu kwa ajili yake katika Jumba la Kumbukumbu za Historia ya Tai Ping Tian Guo mjini Nanjing.

Idhaa ya kiswahili 2004-03-16