Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-06 18:00:00    
Darizi za Yimeng

cri
    Wasichana wa sehemu ya Yimeng mkoani Shandong,China ni hodari wa kulima na kudarizi. Wakati wa msimu wa kilimo wanalima na wakati ambao hakuna kazi mashambani wanafundishana kushona nguo, viatu na kudarizi. Tulipokuwa kwenye matembezi katika sehemu hiyo tuliona wasichana waliokusanyika huku na huko wakishughulikia darizi zao. Darizi tulizoziona ni darizi za kukata.

    Darizi za kukata hutengenezwa hivi: bandika kitambaa kwenye karatasi ngumu au kitambaa kinene, halafu kunja katikati, shona ili kitambaa kikazike. Chora au bandika michoro unayopenda nyuma ya kitambaa, darizi kwa nyuzi za rangi mbalimbali. Baada ya kudarizi, paka gundi nyuma ya kitambaa. Kata kwa kisu kikali katikati ya kitambaa hicho baada ya kukauka, mwisho toa magunia, na hapo darizi itakuwa tayari.

    Katika kipindi cha mwanzoni, darizi za kukata zilikuwa zikitiwa kwenye viatu vya watoto, michoro yao ilikuwa ni kichwa cha chui, kichwa cha paka n.k. Baadaye kidogo, darizi hizo ziliendelezwa na kutiwa kwenye vitako vya soksi, vitandiko vya viatu, mito ya viti, baiskeli n.k. Baadhi ya wasichana wanazawadia wachumba wao darizi zenye picha za "vipepeo na maua" na "simba anayesukuma mpira", wakionesha mapenzi kwa wachumba wao kwa njia hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2004-04-06