Ili kukabiliana na hali ngumu ya hivi sasa katika mapambano dhidi ya ukimwi nchini China, hivi karibuni, serikali ya China imeanza kutekeleza sera mpya za kuwasaidia wagonjwa wa ukimwi na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
Sera hizo ni pamoja na kuwatibu bila malipo wagonjwa ambao ni wakulima au wakazi wa mijini wenye shida za kiuchumi; katika maeneo yanayoathiriwa vibaya na maambukizi ya ukimwi, watu wakiwa hiari wanapata ushauri na kupimwa damu bila malipo; na watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kutokana na ukimwi wanapewa elimu bure.
Hivi sasa, idadi ya watu wenye ukimwi imefikia laki 8.4 katika China Bara, na maambukizi ya ugonjwa huo yapo katika kipindi muhimu ambapo ukimwi umeanza kuenea mionogni mwa watu wa kawaida kutoka kwa watu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa. Serikali ya China inahamasisha nguvu za jamii nzima na kuchukua hatua zenye ufanisi ili kuzuia uenezi na maambukizi ya ukimwi.
2004-04-10
|