Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-04-21 18:59:46    
Chumvi yenye madini ya joto

cri
Katika miaka 10 iliyopita, serikali ya China ilifanya jitihada kubwa katika kuondoa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto mwilini. Sasa hali ya ukosefu wa madini ya joto nchini China imeboreshwa sana, wagonjwa wenye ukosefu wa madini ya joto sasa hivi wanapungua siku hadi siku.

    Bibi Wang Huimin anaishi mjini Beijing. Yeye hununua matunda, mboga na vitu vingine vya mahitaji ya maisha katika soko moja lililo karibu na nyumbani kwake. Mwandishi wetu wa habari alipomwona alikuwa akinunua chumvi. Mwandishi wa habari aligungua kuwa, Bibi Wang alichagua chumvi yenye alama ya "nyongeza ya madini ya joto. Bibi Wang alisema

    "tumepata maelezo mengi kuhusu faida ya madini ya joto kutoka katika magazeti na radio. Watu wenye ukosefu wa madini hiyo wanashambuliwa na magonjwa mengi. Hivyo, katika miaka mingi iliyopita, familia yangu inashikilia kutumia chumvi yenye madini ya joto. Mbali na hayo, wenzangu na marafiki zangu pia wanatumia chumvi yenye madini hiyo."

    Takwimu za Wizara ya Afya ya China zinaonesha kuwa, sasa wachina waliotumia chumvi yenye madini ya Joto wanafikia 90%, magonjwa ya goita, ububu na kuwa kiziwi yanayosababishwa na ukosefu wa madini ya Joto mwilini yamepungua sana. Katika miaka ya 70 hadi 80 ya karne iliyopita, wachina waliokuwa wakitumia chumvi yenye madini ya Joto walikuwa wachache. Kutokana na ukosefu wa madini hiyo mwilini, wagonjwa wa goita walifikia milioni 35, na viziwi na mabubu walifikia laki 2.5. hali ya ukosefu wa madini hiyo iliathiri vibaya afya za watu na kuzuia sana maendeleo ya uchumi wa China.

    Ofisa wa Wizara ya Afya ya China Bw. Chen Shaoxian alijulisha:

    Serikali ya China siku zote inatilia maanani kazi ya udhibiti wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto mwilini, ambapo iliwekwa kwenye kazi muhimu ya serikali. Hivi sasa China imeanzisha mfumo wa ushirikiano wa idara mbalimbali chini ya uongozi wa serikali na jumuiya mbalimbali za jamii kushiriki kwenye shughuli hiyo. Katika mchakato wa kuondoa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto, kushikilia kutumia chumvi yenye madini ya Joto ni hatua muhimu.."

    Ili kuthibitisha ubora wa chumvi yenye madini ya joto, serikali ya China iliwekeza Yuan Bilioni 1, ilitumia mkopo kutoka Benki ya dunia kufanya marekebisho ya ufundi kwa zaidi ya viwanda 100 vya chumvi nchini China. Mbali na hayo, ili kuhakikisha utengenezaji na utoaji wa chumvi yenye madini ya joto, serikali ilitunga sheria ya kuuza chumvi. Kueneza elimu ya udhibiti wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto pia ni hatua muhimu. Hivyo, China iliweka tarehe 15 mwezi Mei kuwa siku ya udhibiti wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto.

    Mbali na hayo, China ilitilia maanani kueneza elimu kuhusu ukosefu wa madini ya joto. Fujian, mkoa wa pwani wa Kusini-Mashariki ya China ulifanya kazi nyingi zenye mafanikio. Mkoa wa Fujian una maliasili nyingi ya chumvi, bei ya chumvi ya kawaida ni rahisi sana kuliko chumvi yenye madini ya joto. Watu walinunua zaidi chumvi ya kawaida. Kutokana na hali hiyo, idara za afya na elimu za Fujian zilishirikiana kwa pamoja, zilifanya shughuli mbalimbali za kueneza elimu ya ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto katika shule za msingi na sekondari. Ofisa wa Idara ya afya ya mkoa wa Fujian Bw. Chen Wenjia alisema

    "Kila mwaka tunafanya shughuli za kuwaelimisha wanafunzi mara moja au mbili ili kueneza elimu ya udhibiti wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto kwa kila mwanafunzi, kuwawezesha kuanzisha fikra ya kulinda afya zao tangu wanapokuwa watoto."

    Kwenye shughuli za elimu, kuna kazi moja ya kuwafundisha watu namna ya kutofautisha chumvi ya kweli yenye madini ya joto na chumvi bandia. Baada ya kupewa ujuzi huo, wanafunzi wanawafundisha wazazi wao. Katika miaka minne iliyopita, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari milioni moja mkoani Fujian walishiriki kwenye shughuli hiyo. Sasa, watu wanaotumia chumvi hiyo mkoani Fujian wameongezeka kwa kiasi kubwa. Hivyo, njia hiyo inaenezwa katika sehemu nyingine nchini China.

    China iliimarisha kazi ya usimamizi na ukaguzi wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto. Katika miaka 10 iliyopita, China ilifanya uchunguzi mkubwa wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto mara 4. Kutokana na matokeo ya uchunguzi huo, China ilitunga kanuni ya kuongeza madini hayo kisayansi, katika mwaka 2000 China ilitangaza kigezo kipya cha chumvi.

    Ofisa wa Wizara ya afya ya China Bw. Chen Shaoxian alisema:

     "mwaka 2000, China iliitangazia dunia kwamba, kimsingi hali ya ukosefu wa madini ya joto imeondolewa nchini China. Matokeo ya uchunguzi wa hali ya ukosefu wa madini ya joto uliofanyika mwaka uliopita yalionesha kuwa, kiasi cha watu waliotumia chumvi yenye madini hayo kimefikia 90%, wagonjwa wa gotia walipungua sana na kukaribia kiwango cha 5% cha kimataifa."

    Mwenyekiti mtendaji wa UNICEF Bibi Karin Sham Poo alisema:

    "Mafanikio makubwa yamepatikana katika udhibiti wa ugonjwa wa ukosefu wa madini ya joto nchini China. Kiasi cha watu waliotumia chumvi yenye madini ya joto kikifikia 90% katika nchi Fulani, tunaweza kusema kuwa, nchi hiyo imepata mafanikio makubwa. China ilitimiza lengo hilo na kuwa mfano mzuri kwa nchi nyingine."

Idhaa ya kiswahili 2004-04-21