Kila ifikapo majira ya baridi, wakazi wa Mji wa Bozhou, jimboni Anhui wanapenda sana kufanya sherehe za harusi. Kwa kawaida katika sherehe hizo husikika sauti za ngoma na suona(filimbi ya China) na huonekana makundi ya watu wakiandamana huku wakimbeba bibiharusi kwenye kiti cha sedani kilichopambwa mapambo ya harusi.
Sehemu ya juu ya kiti kicho huwa kinapambwa kwa michoro yenye rangi mbalimbali na sanamu za watu za rangi. Niliwahi kuwatembelea wasanifu wawili wanaotengeneza viti vya sedani vyenye mapambo aina mbalimbali. Kwa mfano, juu ya mlango wa nyumba ya Xu Lianying aliyekuwa akiishi huko Tangjiaxiang zilitundikwa picha za kiti cha sedani kilichochorwa picha za watu kumi na zaidi kwa rangi mbalimbali na wakiwa wanaonyesha vitendo vya aina mbalimbali vya kuwavutia watu.
Wengine niliowatembelea ni familia ya ndugu Shan Tinggui na mke wake Liu Xinqin walioko Mtaa wa Yanwachi. Msanifu huyu, Shan Tinggui aliniambia kwa dhati: akisema "kutengeneza kiti cha sedani chenye rangi ni ufundi sanifu wa jadi. Tangu utoto wangu nilikuwa namuona babu yangu akitengeneza sanamu za watu kwa kutumia udongo huku akinisimulia hadithi. Wakati mwingine alipokuwa amefurahi sana, aliimba nyimbo. Wakati mwingine alitengeneza sanamu za udongo za buddha na kumpaka rangi usoni na kuonekana amefuga ndevu vizuri na kuvalia nguo nzuri na viatu. Wakati huo nilikuwa najifunza kidogo kidogo na kwa siri, ufundi wake hadi nikafanikiwa kuujua. Katika maonyesho ya kiti cha sedani chenye rangi cha kumkaribisha bibi harusi kwenye Tamasha la Utamaduni la Dawa za Miti-shamba za China kulitumika kiti cha sedani chenye rangi mzuri nilichokitengeneza". Walitumia udongo kutengeneza sanamu za watu, kisha walitumia vitambaa vya pamba na vya hariri vyenye rangi mbalimbali kuzishonea nguo sanamu hizo ambazo zilionyesha maumbo ya namna mbalimbali. Nilitoa shukrani za dhati kwa wasanifu hao wawili wenye kiwango cha juu cha ufundi.
Kwa maelezo ya msanifu Shan: paa la kiti cha sedani cha rangi inapambwa kwa ufundi; pembe zake nne zinaangaliana kwa mapambo ya vitu vinavyoonyesha baraka nyingi katika maisha; juu ya upenu kunatundikwa vipande vya vitambaa vya rangi na mipira ya rangi.
Kuta nne za kiti cha sedani cha rangi zinapimwa kwa ufundi wa hali ya juu na kupambwa picha za vinyago vilivyotengenezwa kwa udongo ambayo maudhui yake ni historia ya jadi. Vinyago hivyo vya udongo kwenye kiti cha sedani cha rangi hutengenezwa kwa ufundi wa kujivuna na wasanifu wa Mji wa Bozhou. Wasanifu hao kwa kuangalia sana hulka na maumbo ya watu walivumbua maumbo yaliyo kama miungu. Aidha, walitumia sanamu za vinyago vya udongo yenye rangi na vitu vya baraka vinavyoashiria mambo mengi ya mafanikio. Yote hayo ni ishara za maombi ya watu wanaotaka kuishi kwa amani, ustawi na utajiri, na mawazo ya binadamu yanayotamani furaha na starehe inavyotokana na uzuri wa kimaumbile. Usanifu huu unaoonekana kama ni lulu, na unasifiwa sana na watu.
Idhaa ya Kiswahili 2004-04-22
|