Msikilizaji wetu Cornelius Boke wa sanduku la posta Isibania Kenya ametuletea jibu la chemsha bongo kuhusu China ya leo akisema kuwa, China ya leo imepiga hatua kubwa sana kiviwanda kuliko miaka ya nyuma, China ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea sana duniani.
China inashikilia nafasi za mbele kabisa katika sekta za biashara ,ambapo bidhaa nyingi za mataifa ya Afrika, Asia na hata Ulaya zinatoka China.
Idadi ya watu wa China ni kubwa mno duniani kuliko nchi yoyote ile, China imefanya bidii kwa kuhudumia watu wake na kuwa na maisha mazuri, imepanua biashara na viwanda nje ili kupanua nafasi za kazi kwa watu wake.
China ina makabila mengi sana, hivyo basi demokrasia ya nchi hiyo inaendeshwa kwa njia halisi na haki kuliko mataifa mengi duniani yenye makabila mengi. Watu wa China wanashirikiana sana kwa jambo lolote lile kuhusu nchi yao.
Upande wa kijeshi China ina wanajeshi wengi sana na waliohitimu mafunzo ya hali ya juu duniani. Wanajeshi wa China wanashirikiana sana kulinda nchi yao na hata kupata mafunzo kwa nchi nyingine ili kusaidia kuleta amani duniani.
Michezo kwa watu wa China imeanza kuendelea kwa haraka sana kuliko miaka ya nyuma. Kwa sasa mwaka 2002 China ilishiriki kombe la duniani nchini Japan na Korea ya kusini na imefaulu kuomba kuandaa michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2008.
Upande wa elimu, China ina wasomi wengi sana duniani na wanaofanya nchi za nje. Watu wengi kutoka nchi za nje kama vile rubani, daktari, wanasheria na wengineo wanasoma nchini China, ambao wanaona wanaweza kupata mengi nchini China.
China ina uhusiano mzuri na sifa nzuri sana na nchi nyingi duniani. Zaidi ya nchi 163 duniani zina uhusiano mzuri wa kibalozi na China. Kama vile nchi ye Kenya, ina uhusiano mzuri sana na China na inapata misaada mingi kutoka China.
Anasema kuwa, watalii wengi kutoka Afrika, Asia na Ulaya wanaitembelea China kwa sababu ya hali ya hewa, usalama nchini China na utaalamu wa watu wa China, hivyo basi ni kwa sababu ya hatua hiyo iliyopigwa na China.
China ni mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, hivyo hasa inasaidia baraza hilo kutatua matatizo ya watu na nchi mbalimbali duniani.
Wizara ya Afya ya China ni ya hali ya juu sana kuliko mataifa mengi duniani, ambayo inazingatia vilivyo afya ya wachina, hivyo wastani ya maisha ya mchina ni miaka 71.8 ambapo ni nzuri sana kuliko mataifa mengi.
Maoni yake kweli yanatufurahisha, mimi naona suala hilo la maisha marefu ya watu ni kutokana na sababu mbalimbali, kwanza tunaweza kuona kwamba maisha ya wachina wengi yameboreshwa miaka ya hivi karibuni, ambapo serikali ya China imechukua hatua mbalimbali za kinga na tiba ya maradhi.
Msikilizaji wetu David L.Mguji wa chuo cha ufundi Ruanda sanduku la posta 595 Mbeya Tanzania anasema katika barua yake kwamba, anapenda kutoa maoni yake kwa Radio China kimataifa inayopendwa na wengi katika kundi la radio za kimataifa duniani kwa utoaji wake habari nzuri na chemsha bongo za kuelimisha wasikilizaji wake.
Anasema kwamba ingawa yeye si mshiriki wa kiwango cha juu lakini yuko mbioni, na anaipenda Radio China kimataifa kutokana na mambo yake mazuri ya kuelimisha jamii. Yeye anapenda kusikiliza Radio China kimataifa, lakini mara kwa mara humkatisha tamaa kutokana na usikivu wake dhaifu hapo Mbeya nchini Tanzania. Hivyo anaonelea kwamba kwa sababu China ni taifa la kimaendeleo ulimwenguni, na ana hakika kuwa vyombo vyake vya utangazaji viko katika hali ya kimaendeleo pia, hivyo Radio China kimataifa haina budi kuboresha zaidi mitambo yake isikike kwa uzuri na ufasaha zaidi katika nchi ambazo ina wapenzi wengi kama Tanzania.
Anasema kwa kweli hapo Tanzania kuna wapenzi wengi wanaopenda kuisikiliza lakini usikivu wake si mzuri kama tunavyozipata matangazo ya Ujerumani, BBC Uingereza, na Marekani nchini Tanzania. Hivyo itakuwa vizuri kama tutaboreaha mitambo yetu ikafikia hii au zaidi kuendana na wakati na teknolojia ya sasa au ikiwezekana wasikilizaji wetu wanaweza kusikiliza matangazo kupitia televsheni wawe wanawaona watangazaji kama vile BBC, Ujerumani tunavyowasikia na kuwaona kupitia ITV hapo Mbeya.
Maoni hayo ni mazuri, lakini utatuzi wa suala hilo ni kazi, suala ambalo haliwezekani kutatuliwa baada ya siku chache tu, kwani linahusiana na mambo mengi, lakini Radio China kimataifa inajitahidi, kwa mfano sasa matangazo ya idhaa yetu ya kiswahili sasa yamerushwa hewani kupitia Radio ya KBC, Nairobi Kenya, kila siku saa 11 na nusu hadi saa 12 jioni, siku za usoni tutajitahidi kusambaza vizuri zaidi matangazo yetu barani Afrika.
Anasema kuwa, lingine linahusu mashindano ya chemsha bongo kwa akili, anachotaka kusema ni kwamba katika matokeo ya chemsha bongo anatazamia washindi watachaguliwa kutoka nchi mbalimbali. Haelewi kwamba uchaguzi unachanganya lugha zozote kwa pamoja wakati wa kuandaa washindi au la. Hivyo yeye alikuwa anaonelea kwamba kama ni lugha ya kiswahili basi iwe na washindi wake binafsi akiwa na maoni kwamba wawepo mshindi wa kwamba hadi wa tatu wa kuizuru China ili kuweka mchanganyo wa lugha zote au rangi zote, na lugha zenye wasikilizaji wengi zipewe kipaumbele hajui kama tumeshampata lengo hapa katika kuiboreha radio yetu iliizidi kupendwa na wqengi.
Anasema kuwa hapa ana maana kwamba ili wasikilizaji wengine wasijione wanyonge kuwe na mpambano wa makundi. Mfano huwezi kushindanisha tembo au sungura katika mbio au mapigano au kunywa maji na kula majani au kubebeshwa mzigo ulio na uzito sawa n.k, hakika ujue matokeo yake kilicho kwenye fani hiyo siku zote kitashinda. Haitatokea hata siku moja sungurqa akanywa maji kumzidi tembo au tembo kukimbia sana kumzidi sungura au sungura kubeba mzigo sawa na tembo itakuwa miujiza. Hii ni kujaribu kuonyesha tu ni jinsi gani Radio iweze kuwapedezesha na kuwavutia wanachama wake wote na kuzipatia wengine wengi.
Tunapenda kumfahamisha kwamba, kila kamati ya uchaguzi ya Radio China kimataifa inapochagua wasikilizaji washindi huchanganya lugha mbalimbali za radio yetu, kwa sababu matumizi ya shughuli hizo ni finyu, haiwezekani kuchagua washindi wengi au kutoa kipaumbele kwa sehemu fulanifulani, lakini kila mara sisi tunajitahidi kupata nafasi ili wasikilizaji wetu wapata bahati.
Anaongeza kusema kuwa ni hayo tu mawili lingine anatoa shukrani kwa kumkumbuka na kumtumia maswali ya chemsha bongo pamoja na kadi nzuri ya kustarehesha akili kwani alijua tumemkatia tamaa na kumsahau kabisa katika ulimwengu wa radio yetu kutokana na muda mrefu hajawaandikia barua. Sasa kutokana na utendaj wenu mzuri wa kuwathamini wanachama wote na kujalil maoni yao anarudi tena kwa kishindo katika kuiboresha radio yetu kwa kutoa michango mbalimbali ya mawazo.
Msikilizaji wetu Iss.Haka Hussein Abdulla wa sanduku la posta 699 Zanzibar Tanzania ametuletea jibu la chemsha bongo kuhusu China ya leo akisema kuwa, baada ya kusikiliza makala 5 anaona kuwa kutokana na bidiii na juhudi kubwa walizofanya na kuionyesha kwa ulimwengu mzima wananchi wa China pamoja na viongozi wao kujiletea maendeleo, ana uhakika kwamba nchi ya China iko siku itakuwa ni taifa kuu lenye kuongoza ulimwengu huu kama ilivyo Markeani hivi sasa, kwani dalili zote zinajionyesha wazi kwa kasi ya ukuaji, wa uchumi wa taifa la China, kasi ya maendeleo ya China hivi sasa imefanya nchi ya China ionekane kuwa ni ya kiko katika nyanja mbalimbali kuwa elimu, sayansi, teknolojia na kadhalika.
Anasema kuwa, pia nchi ya Chia inajiamini kutekeleza utamaduni wake katika kuuenzi na kuudumisha China ya leo ni ya kupendeza na kufurahisha, anatarajia sana atakuwa miongoni mwa watu watakaochaguliwa kuja kuitembelea ili aweze kujionea kwa macho yake maendeleo hayo ya taifa la China na anautakia urafiki kati yetu udumu milele.
Msikilizaji wetu Josephat Kishimba wa sanduku la posta 582, Kahama Shinyanga Tanzania ametuletea barua akisema kuwa, ana furaha kubwa sana kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kujibu maswali yote kwa kuwa ameweza kufuatilia vizuri kabisa makala zote 5, bila kukosa makala hata moja, ingawa wakati mwingine alikuwa anawapata kwa matatizo kwa sababu ya kukatikakatika kwa mawimbi ya sauti, hiyo nayo alishinda mojawapo
China ni nchi ambayo imepakana na nchi nyingi na ina majimbo mengi, China ni nchi ambayo inavutia sana watalii wa nchi mbalimbali , na China imeanzisha uhusiano na nchi nyingi za nje, na angeweza kujifunza kwamba China ni nchi inayojali sana haki za watu wake na ni nchi ambayo inajitahidi sana kuwekeza katika nchi za magharibi.
Anasema kuwa, China ni nchi ambayo inajitahidi sana kitekolojia na hata vifaa vyake na biadhaa zake ambavyo wanaipata, kwa kweli vina ubora zaidi na vinadumu sana.
Anasema kuwa, katika karne hii ya sasa dunia inakwenda kwa kasi sana katika kutumia taaluma za kisasa, nchi ya China ina mabingwa wa fani mbalimbali kwa mara nyingine tena anawapongeza wajumbe wapya wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China mafanikio mema katika China mpya ya karne ya 21. Hongera.
Idhaa ya Kiswahili 2004-04-27
|