Mwanzoni mwa mwezi huu, UNESCO ilifanya mkutano wa 27 kupitisha ombi la China la kuweka mandhari ya "mito mikubwa mitatu iendayo sambamba" kwenye orodha ya urithi wa maumbile wa dunia, na pia imekubali makaburi ya wafalme 13 wa enzi ya Ming na kaburi la mfalme wa kwanza wa enzi hiyo, Zhu Yuanzhang, kuorodheshwa katika urithi wa utamaduni wa dunia. Hadi sasa, kwa ujumla kuna sehemu 29 nchini China zilizoorodheshwa na UNESCO katika uridhi wa dunia.
Katika mkutano huo, nchi 32 pamoja na China ziliwasilisha maombi 37 ya kutaka sehemu zao kuwekwa katika kumbukumbu za utamaduni wa kale na mandhari ya maumbile ya urithi wa dunia. Ombi la serikali ya China lilikuwa ni kuweka mandhari ya kiasili ya "mito mikubwa mitatu iendayo sambamba" kwenye orodha ya urithi wa dunia, na makaburi ya wafalme 13 wa Enzi ya Ming na kaburi la mfalme wa kwanza wa enzi hiyo yakiwa kama ni nyongeza ya sehemu zenye kumbukumbu za utamaduni wa kale zilizokubaliwa za "makaburi ya wafalme wa Enzi ya Ming na Qing".
"Mito mikubwa mitatu iendayo sambamba" inalenga mito ya Nujiang, Lancangjiang na Jinshajiang, sehemu ya mwanzo wa Mto Changjiang. Mito hiyo mitatu yote inaanzia nyanda za juu za mikoa ya Qinghai na Tibet, ambapo watu huita paa la dunia, na baada ya kuingia kwenye sehemu ya kaskazini magharibi mkoani Yunnan inakwenda sambamba kati ya milima mikali kwa zaidi ya kilomita 400. Nafasi fupi kati ya mito ya Lancangjiang na Jinshajiang ni kilomita 66 tu na nafasi fupi zaidi kati ya mito ya Langcangjiang na Nujiang haifikii kilomita 19, mito mikubwa iendayo sambamba bila kukutana ni hali pekee duniani. Eneo ambalo mito hiyo mitatu inapita ni kilomita za mraba elfu 41, ambapo ni sehemu yenye viumbe vya aina nyingi, mimea zaidi ya aina 6,000, na aina za wanyama karibu 200. Kadhalika pia kuna aina nyingi za ndege na wadudu, ambao ni nadra sana kuonekana mahali pengine duniani. Huko ni sehemu yenye vielelezo vya wanyama na mimea maafuru duniani na pia ni sehemue yenye mandhari ya aina zote katika kizio cha kaskazini.
Makaburi ya wafalme 13 wa Enzi ya Ming mjini Beijing na kaburi la mfalme wa kwanza wa enzi hiyo lililopo katika mji wa Nanjing pia yamekubaliwa kuwa urithi wa utamaduni wa dunia. Afisa wa Idara ya Taifa ya Urithi ya China Bi. Zhang Shuangmin anatuambia,
"kufuatana na kanuni za UNESCO, ombi letu la kuorodhesha makaburi hayo ya wafalme ni kama nyongeza ya kumbukumbu za enzi ya Ming na Qing zilizokwisha kubaliwa, thamani yake ni kubwa na inalingana kabisa na kigezo kilichowekwa na UNESCO."
Kaburi la mfalme wa kwanza wa Enzi ya Ming hadi sasa limekuwa na miaka 600, hilo ni kaburi waliozikwa mfalme Zhu Yuanzhang na mkewe. Zhu Yuanzhang alikuwa mfalme wa kwanza wa Enzi ya Ming iliyoanzia mwaka 1368 hadi 1644 nchini China. Mtindo wa ujenzi wa kaburi lake uliathiri ujenzi wa makaburi yote ya wafalme wa enzi hiyo.
Makaburi ya wafalme 13 wa Enzi ya Ming yako katika mlima wa Tian Shoushan, kwenye kitongoji cha Beijing upande wa kaskazini. Makaburi hayo yamechukua eneo la kilomita za mraba zaidi ya 40. Kuanzia mwaka 1409, kwa muda wa miaka zaidi ya miaka 200, ujenzi wa makaburi haukuwahi kusimama. Makaburi hayo mpaka sasa bado ni mazima, na yana thamani kubwa katika utamaduni na historia.
Novemba, mwaka 1985 China ilitia saini "mkataba wa urithi wa dunia". Tokea mkutano wa 11 wa Kamati ya Urithi wa Dunia kukubali kasri la kifalme mjini Beijing na sehemu nyingine 6 hadi leo China imekuwa na sehemu 29 zenye kumbukumbu za utamaduni wa kale na sehemu za kiasili kuorodheshwa kwenye "urithi wa dunia". Afisa wa Idara Kuu ya Kumbukumbu za Kale, Zhang Shuangmin, anasema,
"China ni nchi yenye historia ya miaka elfu 5, ina sehemu nyingi zenye kumbukumbu za utamaduni wa kale. Kutokana na hesabu isiyokamilika, sehemu zenye kumbukumbu za kale zisizohamishika zimekuwa karibu laki 4.".
Kwa kuwa sehemu nyingi zenye kumbukumbu za kale za China zimeorodheshwa katika urithi wa dunia, tatizo la namna ya kuhifadhi sehemu hizo limekuwa kazi kubwa zaidi. Katika miaka ya karibuni, baadhi ya sehemu zenye kumbukumbu zinatumika kupita kiasi, uharibifu unaofanywa kutokana na shughuli za utalii umekukwa mkubwa. Bi. Zhang Shuangmin alisema, serikai ya China imetia maanani tatizo hilo. Anatuambia,
"Kwa ujumla hali ya sehemu hizo ni nzuri baada ya kuorodheshwa katika urithi wa dunia, na kila sehemu inajitahidi kutunza hifadhi kwa hatua na sheria. Mathalan, mkoa wa Sichuan umeweka kanuni na sheria kwa ajili ya hifadhi ya sehemu zote za urithi wa dunia zilizoko mkoani humo, na Beijing pia imetangaza kanuni za kutunza vizuri Ukuta Mkuu. Mwaka huu Idara ya Taifa ya Urithi wa China iko katika kutunga sheria kwa ajili ya kuhifadhi sehemu zote zenye kumbukumbu za kale na kuzikamilisha sheria kwa ajili ya China nzima.
Inafahamika kwamba hivi sasa kuna sehemu nyingi za kiasili na zenye utamaduni wa kale nchini China ambazo zinatayarishwa kabla ya kupeleka maombi ya kuorodheshwa katika urithi wa dunia.
Idhaa ya Khiliiswa 2004-04-30
|