Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-06 22:12:16    
Maswali yanayoulizwa na vijana wanapotembelea angaza

cri
    Swali: Virusi vya Ukimwi vinapoingia mwilini mwa binadamu vinazaliana vipi?

    Jibu: Virusi vikiingia mwilini, vinaingia katika damu ya binadamu na kwenda katika chembechembe nyeupe za damu. Sehemu ya kirusi huugana na kiini cha chembe nyeupe ya damu, na huanza kugawanyika, kutoa virusi vipya. Baadaye chembe nyeupe ya damu inagawanyika, na virusi vipya kutoka na kwenda kushambulia chembe nyingine nyeupe za damu. Matokeo yake chembe chembe nyingi za damu zinakuwa zimeshambuliwa na virusi.

    Swali: Kwa nini inasemekana kuwa Ukimwi ni ugonjwa unaopunguza kinga mwilini?

    Jibu: Binadamu wengi wanapozaliwa kinga mwilini na uwezo wao binafsi wa kupambana na maradhi. Kinga hii ni kazi na inayofanywa na chembe chembe za damu nyeupe. Chembe chembe hizi zinaposhambuliwa na vimelea vya maradhi, uwezo wake wa kupambana na maradhi hupungua, na ndio maana mtu mwenye virusi huugua mara kwa mara.

    Swali: Je kuna sehemu nyingine katika mwili wa binadamu ambapo virusi vya Ukimwi hukaa?

    Jibu: Ndio, virusi vinakaa katika maji maji ya shahawa, maji maji ya ukeni, maziwa na pia katika mate na machozi asilimia tatu (3%) ya wenye maambukizi ya virusi vipo pia katika mate na machozi.

    Swali: Tunaambiwa kuwa Ukimwi maana yake "Upungufu wa Kinga Mwilini". Inakuwaje mwenye virusi vinavyoshambulia kinga mwilini aambiwe ana virusi vya Ukimwi?

    Jibu: Ni kwa sababu hivi virusi ni vile vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini, ndio maana anaambiwa ana virusi vya Ukimwi.

    Swali: Ni muda gani unapita tangu mtu kuambukizwa virusi hadi kuanza kuonyesha dalili za kuanza kuugua Ukimwi?

    Jibu: Mtu anasemekana ana ugonjwa wa Ukimwi anapokuwa na dalili zinazoonyesha upungufu mkubwa wa kinga. Wakati huu unapowadia anakuwa na dalili nyingi mbalimbali. Zipo dalili kadhaa au magonjwa ambayo yanapotekea ni dalili dhahiri kuwa mtu huyu ana upungufu mkubwa wa kinga mwilini, yaani ugonjwa wa Ukimwi.

    Muda unapopita tangu kupata virusi hadi ugonjwa wa Ukimwi unategemea mambo mengi, kama vile aina ya kirusi, na hali ya mwambukizwaji. Sababu zitakazomfanya mtu apate dalili mapema ni kama vile:

    - Umri: Watoto chini ya miaka 5 na watu wa umri wa miaka 40 au zaidi huugua mapema

    - Kuwepo kwa magonjwa mengine

    - Lishe duni

    Ugonjwa huunza kutokea kwa wastani kati ya miaka 2 hadi 10 tangu mtu alipoambukizwa. Wako watu wachache ambao huanza kuugua mapema sana, hata miezi 6 tu baada ya maambukizi, au hata zaidi ya miaka 10/

    Swali: Tunaelimishwa kuwa tunaweza kujikinga kutoka maambukizi ya Ukimwi tukitumia mipira ya kondom, na wengi wanasema haifai kabisa, je ukweli ni upi?

    Jibu: Kujikinga na maambukizi ya Ukimwi yanayotokana na ngono kunawezekana kabisa, kwa njia tatu kuu:

    a) Kuacha ngono kabisa, ua kuahirisha ngono mpaka wakati muafaka; na wakati huo ukifika kusisitiza ngono salama.

    b) Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu aliyepima.

    c) Au kutumia mipira ya kondom kwa kila tendo la ngono/tendo la ndoa.

    Mipira imedhihirishwa kisayansi kuwa inapotumiwa kwa usahihi na kwa kila tendo la ngono hukinga maambukizi ya virusi.

    Swali: Je naweza kupata maambukizi kupitia mate iwapo nitabusiana?

    Jibu: ili virusi vya Ukimwi viingie mwilini inabidi kuwepo na jeraha, kidonda au mchubuko. Hivyo basi, ukibusiana na ulimi na mtu aliye na virusi vya Ukimwi na hali una jeraha, kidonda au michubuko kinywani au kwenye ulimi, basi pana uwezekano wa kupata maambukizi; bali uwezekano ni mdogo.

   Swali: Je mapenzi salama ni yapi?

    Jibu: Ni kufanya mapenzi au ngono ambayo hakuna kabisa kuingiliana na mabapo majimaji ya mwanamke au wanaume hayataingia kwa mwenzi au mpenzi wake. Mapenzi haya yanaweza kuwa ya kugusana, kupapasana au kusuguana. Na iwapo kutakuwa na mwingiliano, basi itumiwe kinga ya mpira wa kondomu (ya kike au kiume).

    Swali: Nimesikia dawa za Ukimwi zipo, ila ni ghali na ndio maana hapa Tanzania hazijaenea sana, eti ni kweli?

    Jibu: Kuna dawa mbalimbali zinazotumika katika ugonjwa wa Ukimwi, kwa mfano

    - Dawa zinazotibu magonjwa yanayoitwa magonjwa ya "kushukia" au "magonjwa ambata". Haya ni magonjwa anayopata mtu mwenye virusi vya Ukimwi anapopungukiwa na kinga mwilini. Magonjwa haya ni kama kifua kikuu, nimonia(kichomi au homa ya mapafu) na baadhi ya matatizo ya ngozi.

    Dawa hizi zipo, zinapatikana katika mahospitali mengi hapa nchini; bali mgonjwa inabidi aonwe kwanza na daktari au tabibu. Dawa hizi haziponyi Ukimwi.

    - Zipo dawa mbalimbali ambazo zinasemekana husaidia kwa njia mojawapo au nyingine; mara nyingi dawa hizi zinatokana na mimea au miti.

    Pia mara nyingi dawa hizi zinatibu au kupunguza magonjwa "ambata" au "ya Kushukia" kama vile magonjwa ya ngozi, kuharisha na hata kuongeza hamu ya kula. Lakini dawa hizi pia haziponyi Ukimwi.

    - Kuna dawa za kisasa zinazopunguza kasi ya ongezeko la virusi. Hizi kwa sasa zinapatikana kwa uchache kwani ni ghali sana; na pia hazipatikani katika mahospitali au maduka mengi ya dawa. Kwa wale wanaoweza kumudu gharama ni kwamba inabidi dawa iandikwa na daktari mwenye utaalamu wa kutibu kwa kutumia dawa hizi. Dawa hizi zina masharti yanayobidi kufuatwa unapozitumia, pamoja na kuchukuliwa vipimo mbalimbali ili kuona kama dawa zitafanya kazi, na hazitamletea madhara mtumiaji.

    Dawa hizi pia haziponyi Ukimwi, bali hupunguza wingi wa virusi, na kupunguza kasi ya ongezeko la virusi. Matokeo yake matu mwenye virusi huweza kuwa na afya nzuri kwa muda mrefu, na magonjwa ya "kushukia" au "magonjwa ambata" hayatampata mara kwa mara.

    Lakini mtu mwenye virusi analazimika kutumia dawa hizi maisha yake yote na anapoaacha kuzitumia dawa hizi virusi huongezeka tena. Kwa kifupi bado hakuna dawa zinazoponya Ukimwi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-06