Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-11 20:48:46    
China yafanya uingiliaji kati miongoni mwa watu wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa ukimwi

cri
    Pamoja na kuongezeka kwa mfululizo kwa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi nchini, serikali imechukua hatua za uingiliaji kati katika baadhi ya sehemu dhidi ya watu wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya ukimwi.

    Watu wanaokabiliwa na hali hiyo ni pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya, makahaba na wasenge. Kwa kawaida ugonjwa wa ukimwi huenea kwanza miongoni mwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, kisha kuenea miongoni mwa watu wa kawaida. Kutokana na takwimu iliyotolewa na wizara ya afya ya China, katika China bara sasa kuna watu laki 8.4 walioambukizwa virusi vya ukimwi, hali ambayo virusi vya ukimwi vinaanza kuenezwa kwa watu wengi wengine. Wataalamu husika wanaona kuwa endapo tusiidhibiti hali hiyo, idadi ya watu wenye virusi vya ukimwi huenda itaongezeka kuwa milioni 10 nchini China ifikapo mwaka 2010. kama tutachukua hatua za tahadhari kuanzia sasa, inakadiriwa idadi ya watu watakaoambukizwa virusi vya ukimwi itaweza kudhibitiwa kuwa chini ya milioni 3 ifikapo mwaka 2010.

    Kutokana na kwamba sindano na siringi zilizokwisha tumika pamoja na na vitendo vya ngono ni njia rahisi ya kuambukizwa virusi vya ukimwi nchini China, ili kuzuia ueneaji wa ukimwi, baadhi ya mikoa na miji ya China sasa imeanza kuchukua hatua za uingiliaji kati ambazo ni pamoja na kuwaruhusu watumiaji wa madawa ya kulevya yenye sumu kidogo badala ya kutumia madawa ya kulevya yenye sumu kali, pia kuwaelimisha watu hao watumie sindano na siringi ambazo hazijatumika pamoja na kodomu.

    Hivi sasa, katika mikoa mitano ya sehemu ya kusini magharibi ya China, watumiaji madawa ya kulevya wameanza kutumia madawa yenye sumu kidogo ambapo mkoa wa Guangdong ulioko sehemu ya kusini ya China utaanza hivi karibuni nao utajaribu njia hiyo, kiongozi wa kituo cha udhibiti wa maradhi cha mkoa wa Guangdong Bw. Lin Peng alisema kuwa baada ya njia hiyo kujaribiwa katika baadhi ya sehemu, watumia madawa ya kulevya wanaruhusiwa kupata kwa njia halali aina ya dawa ya kulevya yenye sumu kidogo ya kumezwa.

    Habari zinasema kuwa kutokana na kwamba sindano na siringi haziuzwi katika maduka ya kawaida ya madawa, hivyo watumiaji wa madawa ya kulevya wanatumia sindano na siringi moja. Juu ya hali hiyo, mji wa Huaibei mkoani Hunan ulioko katika sehemu ya kusini ya China, mwaka huu umeanza kutumia njia ya kuwapa sindano na siringi ambazo hazijatumika ili kuwaepusha kuambukizwa virusi vya ukimwi, pia wataweza kubadilisha sindano na siringi mpya kwa zile zilizokwisha tumiwa bila malipo.

    Aidha, ili kupunguza uambukizaji wa virusi vya ukimwi kwa vitendo vya ngono, asasi moja isiyo ya kiserikali ya mpango wa uzazi wa majira ya mji wa Liuzhou, mkoa wa Guanxi, kusini mwa China, unatoa kondomu kwa makahaba na kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa ukimwi. Katibu mkuu wa tasisi hiyo bibi Long Yan alisema kuwa serikali yetu ya Liuzhou ni yenye busara sana ambayo inaruhusu asasi zisizo za kiserikali kama yetu kushughulikia kazi hiyo. Tunafanya hivyo siyo kuwachochea kufanya ukahaba bali ni kufuatilia afya yao na kuzuia ueneaji wa ukimwi.

    Nchini China, kutumia madawa ya kulevya na ukahaba ni makosa ya kwenda kinyume cha sheria, ambapo polisi inawafuatilia sana watu wanaojihusisha na vitendo hivyo. Sasa, polisi licha ya kukubali kuchukua hatua za uingiliaji kati, inaimarisha pigo dhidi ya watumiaji wa madawa ya kulevya na ukahaba. Watu husika wanasema kuwa baada ya kutekeleza sera hizo, shughuli za uingiliaji kati zitapata ufanisi mkubwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-11