Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-11 22:08:08    
Barua za wasikilizaji 11/5/2004

cri
    Msikilizaji wetu Mogire Machuki wa S.L.P 646, Kisii Kenya ametuletea barua ya emeli akisema akizungumza kipindi maalum cha kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa China na Tanzani alisema, kweli uhusiano ulipo kati ya China na Tanzania unaendela vizuri, hasa pale nchi hizi mbili zilipofanya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi , njia hii kwa mtinzamo wangu ni nzuri kwani nchi nyingi katika dunia zimepiga hatua kutokana na mahusiano hayo.

    Kwa mfano nchi ya China imekuwa kiungo muhimu cha maendeleo ya nchi za Afrika hasa katika kutoa huduma za kijamii ikiwa ni huduma za ujenzi wa shule na vituo vya huma za afya, kweli huduma hizo ni mahitaji ya msingi katika maisha ya binadamu.

    Nikiwa msikilizaji wa idhaa hii niipendayo ya CRI, siku hii nimekumbuka kwa kutathimini yale yaliyoweza kufanywa baina ya nchi hizi mbili, China na Tanzania.

    Ukiangalia kindanindani mahusiano haya mpenzi msikilizaji na rafiki yangu unaweza usielewe ni kwa vipi nchi hizi zimenufaika .

    Hasa nikiangalia jinsi nchi ya Tanzania ilivyoweza kushirikiana na China kama unafuatilia kwa makini kipindi cha daraja la urafiki kati ya China na Afrika unaweza kuona jinsi nchi hiyo inavyotoa msaada kwa nchi za Afrika.

    Wahenga walisema tenda wema uendezako usingoje shukrani, kwa kweli mema mengi tunayoendelea kuyapata kutoka China si ya kubeza na kuyaona kuwa si kitu.

    Anasema asante sana kwa brua yenu fupi ya kunijulisha juu ya vipindi maalum vya kuadhimisha miaka 40 ya urafiki mwema kati ya serikali za Tanzania na China, vipindi vyote tayari nimemaliza kuvisikiliza na kwa maoni yangu ni kuwa vipindi vilikuwa na mambo kadha wa kadha ya kuliwaza kuhusu miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania. Kama vile makala 5 zilizoonyesha ni nchi ambayo haina ubaguzi kwa mataifa ya Afrika na hili linadhihirika kutokana na miradi mbalimbali ya serikali ya China imetekeleza kwenye mataifa kadha wa kadha barani Afrika.

   Kwa kweli vipindi vilikuwa vya kuvutia sana na langu ni kuwa nawatakia maisha marefu watu wa China na udumu urafiki kati ya serikali ya China na Tanzania.

    Msikilizaji wetu Jim Godfrey Mwanyama wa sanduku la posta 1097, Wundanyi Taita Kenya ametuletea barua akiwajulisha kwamba idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa inasikika vizuri sana bila matatizo yoyote huko Nairobi, Kenya, pongezi nyingi sana kwetu na anataka tuendelee hivyo hivyo, na yeye na wenzake watazidi kututegea masikio yao kila wakati.

   Tunamshukuru msikilizaji wetu huyo kutuambia usikivu wake juu ya vipindi vyetu, kila tukipata habari kama hiyo tunafurahi na kutiwa moyo, tukakaza nia kuchapa kazi kwa juhudi kubwa zaidi ili wasikilizaji wetu wafurahie vipindi vyetu.

    Msikilizaji wetu Maluha Martin wa Pugu sesondari school Dar es Salaam, Tanzania ametuletea barua akisema kuwa dhumuni kubwa la kutuandikia barua hii ni kupenda kuwashukuru wafanyakazi wote wa Radio China kimataifa kumkubali kuwa mwanachama wa Radio China kimataifa, kwa hiyo anatushukuru, kwani anaona kwake yeye anaona kuwa ni bahati kubwa kujiunga na Radio China kimataifa yaani CRI.

    Anasema anapenda kuwashukuru kwa ukarimu wetu na kusema kuwa kwa njia hii ya kuwakirimu wasikikilizaji wetu tutaendelea kupata sifa kubwa duniani kote. Si hayo tu bali anapenda kuwashukuru kwa kumtumia barua ambayo ameipata mwaka huu mwanzoni pamoja na kumtumia kalenda ya mwaka huu, amefurahi na hajui afanye nini aweze kuionyesha furaha yake kwetu, kwa kweli anashindwa.

    Na vilevile anatushukuru sana kwa kumtumia kadi za salamu, kwa yoyote hayo anashukuru sana na kuzidi kusema kuwa Radio China kimataifa ni kiboko cha radio zote duniani, ataendela kusikiliza vizuri matangazo yetu na kuwasiliana nasi. Tunamshukuru msikilizaji wetu huyo, na tunawataka wasikilizaji wetu wasikilize vipindi vyetu na kushiriki mashindano ya chemsha bongo ya mwaka huu kuhusu ujuzi wa utamaduni wa sehemu ya magharibi ya China.

    Na sasa tunapenda kuwakumbusha tena wasikilizaji wetu wanaopendelela kutusikiliza na kuleta maoni na mapendekezo kuhusu vipindi vyetu anuani ya Radio China kimataifa. Anuani yetu ni China Radio International, Swahili Section, CRI-25, P.O.Box 4216, Beijing China. Narudia, China Radio International, Swahili Section, CRI-25, P.O.Box 4216, Beijing China; anuani yetu nyingine ni : China Radio International, P.O.Box 60829, Nairobi, Kenya, narudia: China Radio International, P.O.Box 60829, Nairobi Kenya.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-11