Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-14 19:03:26    
Mrithi wa sanaa ya mchezo wa kivuli

cri

   

    Mchezo wa kivuli pia unaitwa "mchezo wa kivuli cha taa". Mchezo huu unachezwa hivi: msanii anamulika na mwangaza wa taa kwenye ngozi za wanyama zilizokatwa katika maumbo ya binadamu, wanyama au vitu vingine, na kuonyesha vivuli vya maumbo hayo kwenye pazia. Ngozi hizo ni nyembamba na kutiwa rangi mbalimbali za kupendeza. Msanii anachezesha ngozi huku akifuata muziki au mazungumzo ya wahusika. Ngozi za maumbo huchezeshwa kwa mfululizo, kwa hivyo kwenye pazia zinaweza kueleza visa mbalimbali.

    Jimbo la Shaanxi ni chimbuko la sanaa za mchezo wa kivuli. Kwa mujibu wa kitabu cha historia, mchezo huo ulianza mapema karne ya 11K.K., na kuenea sana katika Enzi ya Sui (581-618) na Enzi ya Tang (618-907). Sanaa ya mchezo wa kivuli inagawanyika katika madhehebu ya mashariki na magharibi.

    Mrithi wa sanaa ya madhehebu ya magharibi ni Bwana Chen Xiuwen, ambaye alizaliwa mwaka 1958 katika ukoo wa mkulima wa Wilaya ya Longxian, Shaanxi. Ukoo wake umeshughulikia sanaa hiyo kwa vizazi vitatu. Babu yake alikuwa hodari wa kukata ngozi za maumbo na kuonyesha mchezo wa kivuli. Alikuwa tajiri wa kikundi cha sanaa.

    Baba yake, Chen Zhaoxian alikuwa mwakilishi wa wasanii wa madhehebu ya magharibi. Katika kipindi cha miaka 40, alikata ngozi 3,000 zenye maumbo ya aina mbalimbali, ambazo zilionekana kuwa na ubingwa mkubwa na hali ya juu. Mwaka 1956, ngozi zake zilipewa tuzo katika Mashindano ya Kwanza ya Vikaragosi na Mchezo wa Kivuli ya Shaanxi. Mwaka 1987, ngozi zake 150 zilichukuliwa na kuhifadhiwa katika Jumba la Sanaa la China, mwaka 1989 aliorodheshwa katika kitabu "Wasanii Mashuhuri wa Kienyeji wa China"   

    Bw. Chen Xiuwen alianza kujifunza ukataji wa ngozi za maumbo kutoka kwa babaye tangu utotoni mwake. Ustadi wake umekomaa baada ya yeye kuwa mkubwa, sasa ni gwiji wa sanaa ya mchezo wa kivuli. Ana uhodari wa kutumia rangi, kusanifu maumbo ya wahusika, kurembesha nakshi, kutumia wahusika, kurembesha nakshi, kutumia visu kwa makini na kwa mistari myepesi na kupiga chuku.

    Kwa miaka 20 sasa, ngozi za maumbo alizokata zimevuka 600, ziliuzwa Japani, Ufaransa na Marekani, pia zimehifadhiwa katika taasisi na majumba ya sanaa ya manispaa na majimbo ya nchini.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-14