Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-19 19:40:49    
AIDS (UKIMWI) 02

cri

UKIMWI moto

    Endapo viini vya UKIMWI vilivyoko mwilini vitafaulu kwa kiasi kikubwa kuburuga silaha zako za kujihami, basi mwili wako utakuwa na uwezo mdogo wa kupambana magonjwa. Viini vya (magonjwa maalum mbalimbali ambavyo hapo awali vilikuwa havithubutu kukuingilia sasa vitakunyemelea kwa vile wewe umekuwa askari UKIMWI asiye na silaha zake kamili za kujitetea. Kwa mfano kama viini vya magonjwa ya tumbo, au vya magonjwa ya kifua vitabahatisha kuingia mwilini mwako kwa njia yoyote ile, vitakuta hakuna upinzani mkali; na kwa hiyo magonjwa hayo yatapata mteremko wa kukufyeka. Ukweli ni kwamba ukikumbwa na UKIMWI moto kitakachokuua sio viini vya UKIMWI moto kitakachokuua sio viini vya UKIMWI bali ni hayo magonjwa mengine yatakayokunyemelea kutokana na hali yako duni ya kujihami.

UKIMWI vuguvugu

    Endapo silaha zako za kujihami hazitaburugika sana basi uwezo wako wa kujihami hautakuwa duni sana, na kwa hiyo viini vya magonjwa vitakavyojaribu kukunyemelea vitakiona cha mtema kuni. Hata hivyo utakuwa unasumbuliwa sumbuliwa na magonjwa. Lakini wakati mwingine huenda hiyo UKIMWI yako iliyo vuguvugu ikaweza kubadilika na kuwa UKIMWI Moto kufuatana na mabadiliko fulani fulani yatakyowezak utokea mwilini mwako, ama katika hivyo viini vya UKIMWI vitakavyoendelea kuishi mwilini mwako.

UKIMWI Baridi

    Endapo viini vya UKIMWI vilivyoingia mwilini vitashindwa kuburugu silaha zako za kujihami basi wewe hutasumbuliwa na magonjwa ya kunyemelea ama kuotea, na afya yako itaendelea kuwa ya kawaida. Isipokuwa yawezekana pia hiyo UKIMWI yako baridi ikaweza kubadilika hapo baadaye na kuwa vuguvugu au moto kutokana na mabadiliko yatakayoweza kukutokeaa wewe au kutokea hao viini vya UKIMWI vilivyomo mwilini mwako.

Ugonjwa wa UKIMWI(AIDS)?umetoka wapi? Mbona hapo zamani haukusikika?

    Ugonjwa huu umeanza kutambulikana kuanzia mwaka 1981. kumekuwepi na kulaumiana kwingi duniani kuhusu chimbuko la UKIMWI. Wengine wamesema kwamba ugonjwa umeanzia huko AMERIKA ambako ndiko ulipoanza kutambulikana na ambako kwa sasa hivi ndiko kwenye wagonjwa wengi zaidi kuliko mahali pengine. Wengine wamesema kwamba ugonjwa huu chimbuko lake ni AFRIKA n.k. Hakuna mwenye uhakika kwamba ugonjwa umetokea wapi au kwa nani. Linalojulikana ni kwamba viini vya UKIMWI ni viumbe wengine, na ya kwamba vina hali ya kigeugeu?mara vibadilishe umbo; n.k. Kwa hiyo yawezekana kwamba hapo zamani ugonjwa huu haukuwepo kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano huenda viini vya UKIMWI vilikuwa havijawahi kupata nafasi ya kuishi katika mwili wa binadamu, au kama vilikwishapata nafasi hiyo pengine havikuwa na ukali mkubwa.

    Yawezekana pia kwamba ugonjwa huu ulikwishalipuka hapo zamani kisha msimu wake ukapita bila wakale wetu kuweza kuutambua. Lakini hayo yote ni mawazo yasiyo na uhakika.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-19