Mwezi Julai, mwaka 2000, serikali ya China ilipeleka Kikundi cha Madaktari wa Fuoshan na Zhongshan wa Mkoa wa Guangdong, China, kwenda guinea ya Ikweta kufanya kazi ya miaka miwili nchini humo. Katika miaka hiyo miwili, madaktari wa China waliwatibu wagonjwa wengi, kufanya operesheni nyingi na kuwaokoa waguinea wengi waliokumbwa na wagonjwa mblaimbali, walisifiwa sana na serikali na wananchi wa Guinea Ikweta.
Guinea Ikweta ni nchi iliyoko katikati ya Afrika. Hali ya hewa ya huko ni joto sana, na mazingira ya tiba ni ya hali duni. Madaktari wa China kila siku waliwatibu wagonjwa wengi wa huko waliokumbwa na umaskini na magonjwa mbalimbali. Mbali na hayo, madaktari wa China walishughulikia pia kazi ya utunzaji wa afya ya maofisa wa ngazi za juu wa huko. Madaktari wa china walichapa kazi kwa bidii na kuonesha ujasiri, mshikamano na upendo kwa watu na kusifiwa sana na wananchi wa huko.
Madaktari wa China waliofanya kazi nchini Guinea Ikweta walifanikiwa kumwokoa mtoto mwenye umri wa miaka 10 wa shemeji yake Rais Mbasogo wa Guinea Ikweta. Wakati rais huyo alipofanya ziara nchini Hispania, mtoto wa shemeji yake alikuwa amelazwa hospitali kwa siku 7, mkewe alimpigia simu mkuu wa hospitali ya huko kumwagiza kutuma madaktari wa China kumtibu mtoto wa dada yake. Madaktari wa China Zhao Qinghua na Ke Yang walimpima na kuona tumbo la mtoto huyo lilionesha hali mbaya na uvimbe, ambapo mtoto huyo alikuwa akipumua kwa taabu sana. Wakafanya upasuaji mara moja, lakini sku za baadaye virusi vliingia mwilini mwa mtoto huyo, hali yake likuwa bado ni mahtuti, madaktari wa China walimfanyia tena upasuaji na kumtunza kwa mwezi mmoja, wakafanikiwa kuokoa maisha ya mtoto huyo. Mke wa rais alifuatilia sana hali ya mtoto huyo, baada ya mtoto kkuponeshwa, aliwapigia simu na kuwashukuru sana madaktari wa China.
Madaktari wa China walioko ncini Guinea Ikweta walikuwa na mwasiliano mengi na wananchi wa nchi hiyo, wagonjwa waliotibiwa nao walikuwa ni rais wa nchi hiyo na mkewe, majemadari wa jeshi, raia wa kawaida, hata wazururaji wa mijini, wakulima wa milimani na watu maskini walioumwa wote walihudumiwa vizuri na madaktari hao wa China.
Katika hospitali ya Malabo ya mji wa Guinea Ikweta, madaktari wa China kila siku walikutana na raia wa kwaida waliokumbwa na magonjwa wa umaskini, waliwatibu kwa moyo wa dhati, hata kila mara walisahau taabu zao wenyewe za kukabiliwa na tisho la ugonjwa, kila siku walifanya juhudi kubwa za kuwatibu wagonjwa. Wakati walipofanya kazi nchini Guinea Ikweta kwa miaka miwli, madaktari wa China waliwatibu wagonjwa wapatao elfu 98, pia kuwatibu wagonjwa elfu 46 waliolazwa katika hospigali, na pia kuwatibu watu elfu wapatao 12 walioumwa kwa ghafla, kuwaokoa wagonjwa wenye hali mahuti 2400, na kufanya upasuaji ara 2100, kila daktari wa China alifnaya kazi kubwa zaidi kliko madaktari wa nchi nyingine katika hospitali hiyo.
Kutokana na huduma zao nzuri na moyo wao wa kutoa mchango, madaktari wa China walisifiwa na watu wa Afrika na kupata urafiki wa dhati kutoka kwa wananchi wa Afrika. Daktari Zhao Qinghua hawezi kusahau kuwa siku moja alipokea mtoto mmoja wa familia maskini ambaye alikuwa akizirai kwa siku tatu kwa sababu ya kutokuwa na pesa ya kununua dawa, daktari huyo wa China alimpa dawa yao bila malipo na kumwokoa kwa bidii, mtoto huyo hatimaye akapona. Katika siku ya kuzaliwa kwa mtoto huyo, wazazi wa mtoto huyo walikwenda hospitali kumpa daktari Zhao keki ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mtoto wao wakimshukuru kwadhati. Keki hiyo aliinunua baba mzazi wa mtoto huyo kwa mshahara wa mwezi mmoja baada ya kupata ajira hii imeonesha shukrani za dhati za watu wa kawaida wa nchi hiyo kwa madaktari wa China waliofanya kazi nchini humo.
Ingawa hospitali ya Malabo iko mji mkuu wa Guinea Ikweta, lakini hali yake ya tiba ilikuwa ni duni. Madaktari wa China walipaswa kushinda taabu mbalimbali za kukosa maji na umeme. Na Ugonjwa wa Ukimwi ulioambukizwa nchini humo ulikuwa tishio kubwa kwao.
Siku moja jamaa wa mgonjwa wa Ukimwi alikwenda hospitali kumwomba daktari wa China Bwana Ke Yang kumfanyika baba yake upasuaji wa tumbo, kwani daktari mweingine hakubali kumtibu baba yake ugonjwa wa tumbo kwa sababu yeye ni mgonjwa wa Ukimwi, jamaa hyyo alimwomba kwa dhati daktari Ke, alisema, ndio madaktari wa China tu walioweza kumsaidia. Daktari Ke hakusitasita akakubali na kumfanyia baba yake upasuaji wa tumbo na kuonesha bila kujali mgonjwa huyo aliambukizwa Ukimwi. Daktari Ke alimwambia mwandishi wa habari kuwa alipofanya kazi nchini Guinea Ikweta aliwahi kufanya upasuaji wagonjwa wapatao 1000, 38 miongoni mwao ni watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi.
Tarehe 24, Juni, mwaka 2002, Ikulu ya Guinea ya Ikweta ilifanya sherehe ya kutoa tuzo ya medali ya uhuru kwa madaktari 20 wa China waliokamilisha jukumu lao nchini humo ili kusifu mchango waliotoa kwa ajili ya wananchi wa Guinea Ikweta, ambapo Rais Mbasogo alipompa nishani ya fedha mkuu wa kikundi cha madaktari wa China Bwana Xiong Huafeng alimwambia kuwa, nyinyi ni marafiki zangu wazuri sana.
2004-05-21
|