Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-25 18:24:29    
Mpango wa amani ya Mashariki ya Kati

cri

    Tangu mwezi Machi mwaka 2001 serikali ya Sharon ilipoanza kushika hatamu za kiserikali, Israel ilichukua hatua kali za mfululizo kwa Palestina, hasa baada ya tukio la "9.11" mwaka 2001, Waziri Mkuu wa Israel Ariel Shron alkiwa kwa kisingizio cha " kupambana na Ugaidi" aliimarisha zaidi hatua za kijeshi dhidi ya sehemu ya Palestina, na aliona kuwa, mamlaka ya utawala wa Palestina lililoongozwa na Yasser Arafat ni Jumuia iliyowuunga mkono ugaidi, na kuitaka Palestina kubadilisha viongozi, hivyo mazungumzo kati ya Palestina na Israel zilikwama

    Mwezi Juni mwaka 2002, Rais Bush wa Marekani alitoa mpango wa amani ya Mashariki ya Kati. Baada ya hapo, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Russia na Marekani wa mkutano wa Pande 4 kuhusu suala la mashariki ya Kati walikuwa na mazungumzo mara nyingi, na wakaafikiana kutunga Mpango wa amani wa Mashariki ya Kati, mwezi Disemba mwaka 2002 mpango huo ulipitishwa kwenye mkutano wa Washington. Lakini kutokana na uzuiaji wa Israel, Marekani haikuwahi kutangaza mambo halisi kuhusu mpango huo.

    Mwezi Machi mwaka uliopita, mamlaka ya utawala wa Palestina ilifanya mageuzi na kuweka wadhifa wa waziri mkuu na kuunda baraza jipya la mawaziri. Tarehe 30 mwezi Aprili, wawakilishi wa mkutano wa pande nne kuhusu suala la Mashariki ya Kati walikabidhi nyaraka za mipango ya amani ya mashariki ya Kati kwa Palestina na Israel kwa nyakati tofauti, na kutangaza mambo halisi kuhusu mpango huo. Tarehe 4 mwezi Juni, Palestina, Israel na Marekani zilifanya mkutano huko Yakaba, mji bandari wa bahari ya Jordan, zilitangaza kwamba mpango wa amani ya Mashariki ya Kati ulianza kufanya kazi rasmi.

    Mpango wa amani ya Mashariki ya Kati unatekelezwa kwa vipindi vitatu: kipindi cha kwanza (tangu kutangzwa kwa mpango huo hadi mwezi Mei), Palestina na Israel kusimamisha vita; Palestina itapambana na shughuli za ugaidi, kufanya mageuzi ya kisiasa kwa pande zote, kuanzisha mfumo mpya wa kisiasa na kushirikiana na Israel kuhusu suala la usalama; Israel inapaswa kuondoa jeshi kutoka ardhi ya Palestina iliyokaliwa tangu tarehe 28 mwezi Septemba mwaka 2000, kusimamisha ujenzi wa makazi ya wayahudi, kubomoa makazi yaliyojengwa baada ya mwezi Machi mwaka 2001 na kuchukua hatua zote za lazima ili watu wa Palestina kuishi maisha kama kawaida. Kipindi cha pili ( kuanzia mwezi Juni hadi mwezi Disemba mwaka 2003) ni kipindi cha mpito, kazi muhimu ni katika, kuanzisha nchi ya Palestina yenye mpaka wa muda na alama ya mamlaka mweshoni mwa mwaka 2003. Na miaka miwili bada ya hapo ni kipindi cha tatu, Palestina na Israel zinapaswa kukamilisha mazungumzo kuhusu hadhi ya mwisho ya mwaka 2005 na kuanzisha nchi ya Palestina.

    Lakini , kwa kuwa serikali ya Israel siku zote inashikilia kwa ukali sera vikali kwa Palestina na vikundi vya Palestina vyenye siasa kali havikuachia mashambulizi dhidi ya Israel, mzunguko mbaya wa kufanya mashambulizi dhidi ya vitendo vya kikatili uliendelea bila kusita kati ya Palestina na Israel. Mbali na hayo, serikali ya Bush ya Marekani inaipendelea zaidi Israel, hivyo Palestina ilikumbwa na hali ngumu zaidi. Mwezi Septemba mwaka uliopita, mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel yalikwama na mpango wa amani ya Mashariki ya Kati ulishindwa kutekelezwa.

    Mwezi Disemba mwaka uliopita, Bw. Sharon alitoa mpango wa hatua za upande mmoja. Mpango huo si kama tu ulipindua kikamilifu mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel, bali pia unatofautiana kimsingi na mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliotungwa hapo awali.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-25