Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-28 21:52:38    
Nchi za Afrika na China zitakuwa na ushirikiano wa kunufaishana

cri

    Mkutano wa kwanza wa kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi duniani kuondokana na umaskini ulifunguliwa tarehe 26 mwezi huu huko Shanghai, China. Mada kuu ya mkutano huo ni kufanya juhudi kubwa ili kuongeza zaidi ufanisi katika kupunguza umaskini. Waziri mkuu wa China Wen Jiabao alitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano, akifahamsiha pendekezo la China kuhusu suala la kupunguza umaskini duniani, kwamba nchi mbalimbali zinapaswa kufanya juhudi za kujenga mazingira ya amani na utulivu katika nchi za dunia; kuanzisha utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi ulio wa haki na halali duniani; na nchi zlizoendelea ziwajibike kuzisaidia zaidi nchi zinazoendelea.

    Waziri mkuu wa China Wen Jiabao ameahidi kuwa China inashirikiana na nchi mbalimbali katika kazi ya kupunguza umaskini duniani.

    Leo mwandishi wetu wa habari amepata nafasi kumhoji Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda.

    Mwandishi: Mheshimiwa Rais wa Uganda, tafadhali uwaelezee wasikilizaji wetu wa Afrika ya mashariki hali kuhusu mkutano wa kupunguza umaskini duniani.

     Rais Museveni: Mimi sikuhudhuria mkutano wote nilihutubia tu jana. Bwana Wolfenson nilivyomsikia akisema ni kuwa  watu wengi walikuwa wamezungumzia juu ya hali za nchi namna ya kuweza kupambana na umaskini, hivyo baadaye watapambana kwa pamoja kuhusu hali ya umaskini na kutoa msimamo wao wa pamoja.

    Mwandishi: Serikali ya Uganda ina mpango gani kuhusu kupunguza umaskini?

    Rais: Kupunguza umaskini kutaleta maendeleo kwa nchi, na tukiweza kufanikiwa kupata maendeleo mwishowe, tutaweza kukomesha umaskini ili kupunguza umaskini na kupata maendeleo tunatakiwa kuwa na vitu vinne muhimu.

    Kwanza, Kuweka viwanda kwani tukiwa na viwanda vingi tunaweza kuwapa watu ajira .

    Pili, kuata masoko ili wananchi waweze kuuza mazao yao.

    Tatu, serikali kuwa na kiwango kikubwa cha fedha zinazotokana na kodi ili kuweza kutatua shida za wananchi na kujenga mahospitali, mashule na barabara, hii ndiyo njia ya tatu ambayo itatuwezesha kuondokana na umaskini.

    Nne kuwepo na mikopo midogo midogo kwa watu wenye uwezo mdogo.

    Mwandishi: Suala la kupunguza umaskini unahusika pia na kazi ya kuwasiaida watu walioambukizwa ugonjwa wa ukimwi, Uganda inajulikana kuwa imedhibiti vizuri maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, je, tunaweza kusema kuwa Uganda hakika itafanya vizuri kazi ya kupunguza umaskini?

    Rais: Kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi ni njia mojawapo ya kupunguza umaskini, kwa sababu kama mtu ana ugonjwa hana nguvu za kuweza kufanya kazi, na kama akiwa hivyo basi umaskini unazidi kwa kasi. Hiyo kupambana na hili gonjwa la hatari ni njia mojawapo ya kuondokana na umaskini.

    Mwandishi: Jana Rais Hu Jintao wa China alikutana na wewe na mlikuwa na mazungumzo, rais Hu ameahidi kuimarisha na kuendeleza zaidi urafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na nchi za Afrika pamoja na Uganda, wewe una maoni gani kuhusu ushirikiano huo wa kunufaishana?

Rais Museveni akihojiwa na mwandishi wa habari wa CCTV

    Kuhusu uhusiano wetu ni mzuri sana na tunashirikiana kwa pamoja. Rais Hu aliamua kuangalia ni jinsi gani China inaweza kupunguza kodi za bidhaa ambazo zinatoka Afrika kuja China kwa hii ni njia mojawapo nzuri ya kuongezeka kwa soko. Pia tuliweza kuzungumzia suala la Petroli. Afrika kuna wachina ambao wana ujuzi fulani ambao tunaweza kushirikiana nao tukaweza kupata sehemu za kuchimba mafuta ya petroli tukapata mafuta kwani sisi tuna maeneo ambayo labda tunaweza kupata mafuta ya petoli.

    Mtangazaji: Asanteni sana Mheshimiwa Yoweri Museveni wa Uganda kwa maelezo yake. Tunaona wasikilizaji wetu watafurahi maelezo aliyotoa kwa kiswahili rais wa Uganda.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-28