Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-05-28 22:06:38    
Michoro kwenye nyungo

cri
    Miaka ya hivi karibuni, michoro kwenye nyungo za Bonamo, aina mpya na pekee ya sanaa, yenye sifa ya mila ya Kabila la Wabuyi ilianza kujulikana na kupendwa nchini na nchi za nje kutoka viunga vya Mji wa Guiyang, jimboni Guizhou, nchini China.

    Bonamo, katika lugha ya Kibuyi maana yake ni Mlima wa Yunwa ambao uko kiungani mwa Mji wa Guiyang. Nyungo ni vifaa vya kawaida vilivyosukumwa kwa mianzi, na wakulima huvitumia kupeta mchele, kuanika unga wa nafaka na kuwekkea vitu. Lakini wakulima hodari wa Kabila wa Wabuyi wakitumia nyungo kama karatasi wanachora mimea, maua, samaki, ndege, wanyama, mito na milima, jua na mwezi, na hata kuandika hekaya na hadithi nyingine juu yake, na kuzifanya ziwe vitu vya sanaa vyenye sifa za kikabila.

    Chanzo cha michoro kwenye nyungo ni maisha ya vijiji vya Guizhou. Baada ya kuvuna mpunga na kupata mchele mpya, wakulima wa huko hutengeneza maandazi kwe mchele wa kunata kuwa chakula cha wakati wa kujenga nyumba, sherehe za ndoa, sikukuu, au wakati wa shughuli nyingi za kilimo. Wanatia rangi mbalimbali katika maandazi yakikauka na kuondolewa, alama mbalimbali za rangi zinabaki kwenye nyungo. Kwa kuwa alama hizi zinapendeza sana, zinawafanya wakulima hawa wajiwe na mawazo ya kuchora michoro kwenye nyungo hizi.

    Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Kamati ya Mambo ya Makabila ya Mji wa Guiyang iliendesha semina ya kwanza ya michoro kwenye nyungo na wanafunzi Wabuyi waliotoka vijijini mbalimbali walichora michoro mingi. Michoro hiyo ina rangi za kupendeza na mtindo wa kipekee, inasifiwa na wachoraji wa nchini na kupendwa sana na watalii wa China na nchi za nje.

Idhaa ya Kiswahili 2004-05-28