Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-02 18:43:21    
AIDS (UKIMWI) 05

cri

    Nifanye nini nisipate UKIMWI?

    Ukitaka usipate UKIMWI(AIDS) jitahidi kutimiza mambo yafuatayo:

    1. Kama wewe hujaoa au hujaolewa epukana na matembezi ya aina yoyote; na zaidi ya hilo jiepushe hata kufanya michezo ya mapenzi na mtu yeyote aliye katika kundi la wale tuliosema kwamba ni maarufu kwa UKIMWI.

    2. Kama wewe umeoa au umeolewa kuwa mwaminifu katika unyumba wako; na endapo kuna shaka kwamba mkeo au mumeo hunda kwa bahati mbaya akawa ameingiliwa na viini vya UKIMWI kutokana na sababu mbalimbali, basi kila mara kabla ya kufanya kitendo cha ndoa hakikisha kwamba umechukua angalao tahadhari fulani fulani za kusaidia kuzuia kuambukizana ugonjwa?kwa mfano wewe mume unaweza kuvaa mpira (condom) unaotumika kwa uzazi wa majira.

    3. Endapo hapana budi upewe damu ili kuokoa maisha yako, basi jitahidi kila inapowezekana hao wahisani watakao jitolea kukusaidia damu wapimwe kwanza damu zao ili kuthibitisha kwamba hawana UKIMWI.

    4. Hakikisha kwamba vyombo vinavyotumika kukuhudumia (wakati wa kudungwa sindano yoyote, au wakati wa kuchanjwa dawa yoyote; au wakati wa kutahiriwa; au wakati wa kutibiwa vijeraha popote mwilini) ni safi kabisa na vimechemshwa vya kutosha. Kamwe usikubali kupokea hudumu za aina hiyo zitolewazo vichochoroni au kwenye mazingira yoyote yasiyo safi.

    5. Epuka kushirikiana na watu wengine (hasa wale usiowafahamu vizuri) vitu fulani fulani kama vile miswaki na nyembe za kunyolea.

    6. Kama wewe unashughulika kuwatibu au kuwauguza wagonjwa wa UKIMWI chukua tahadhari za kufaa kuzuia usiambukizwe.

    Ikiwa viini vya UKIMWI huishi katika chembechembe za damu inatokeaje vikaonekana kwenye maji ya kiume ya uzazi, utoko, mate, machozi n.k.

    Viini vya UKIMWI huweza kuwemo kwenye chembechembe za damu na pia kwa uchache kwenye maji ya damu ambamo chembechembe hizi huelea. Vitu hivi viwili (yaani chembechembe za damu zenye viini, au maji ya damu yenye viini) huweza kuchanganyikana na majimaji ya aina mbalimbali yanayomtoka mwenye UKIMWI katika sehemu mbalimbali kwa kuwa damu yake husafiri na kupitia katika kila sehemu ya mwili wake.

    Tunaposema kwamba viini vya UKIMWI vimeonekana katika maji ya kiume ya uzazi, ni katika sehemu ipi hasa?ni katika yale maji au katika mbegu zenyewe za kiume?

    Ni katika yale maji, na sio katika mbegu za kiume za uzazi.

    Je, viini vya UKIMWI vina uwezo wa kutoboa vyenyewe ngozi laini ya njia ya uumeni, ukeni n.k.?

    Hapana. Ni lazima pawepo jeraha ama hali ya kuchubuka kidogo katika sehemu hizo.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-02