Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-10 18:23:59    
Maisha ya wanakijiji katika kijiji kongwe kiitwacho Tunbao

cri
    Katika sehemu za milima zilizopo mpakani au mbali na miji, wenyeji wa huko walikuwa wanaishi maisha ya kawaida ambayo hajaathiriwa na mabadiliko ya nje. Hivi sasa, kutokana kuboreshwa na hali za usafiri na mawasiliano, watu wanaoishi milimani wamekuwa na nafasi nyingi za kukutana na wageni, hivyo maisha yao pia yanabadilika.

    Kijiji cha Tunbao kipo umbali wa kilomita 60 kutoka mji mkuu wa mkoa wa Guizhou, na kinaonekana kama ngome kongwe: barabara za mawe, kuta na mapaa ya nyumba pia zimejengwa kwa mawe miaka mia kadhaa iliyopita.

    Kijiji cha Tunbao kipo milimani. Tatizo la usafiri lilikuwa limekwamisha mawasiliano kati ya wenyeji na sehemu za nje. Kwa hivyo, katika kutekeleza mkakati wa taifa wa kustawisha sehemu za magharibi katika miaka ya karibuni, serikali ilitoa kipaumbele kwa tatizo hilo la usafiri. Serikali kuu ya China na serikali ya mkoa wa Guizhou zilitenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

    Hivi sasa, barabara kuu ya ngazi ya taifa imeunganisha kijiji cha Tunbao na sehemu za nje, na pia kuleta watalii wengi. Tunapokaribia kijijini, tunavutiwa na wimbo mtamu wa wanawake.

    Wimbo huu unasema, "karibuni wageni waheshimiwa kutoka mbali. Karibuni muangalie Tunbao na watu wake. Karibuni mnywe chai." Tuligundua kuwa, wanawake kadhaa wenyeji walikuwa wanaimba huku wanawakaribisha wageni chai. Mabirika ya chai na vikombe vinatengenezwa na wenyeji, na chai yenyewe pia ni aina maalumu ya sehemu hiyo. tulipokunywa chai, msichana mmoja anayetuongoza kwenye utalii alituelezea historia ya kijiji hicho.

    "katika karne ya 14, walikuwepo wakazi wachache sana mkoani Guizhou. Wakati huo, mfalme wa China aitwaye Zhu Yuanzhang aliagiza wafanyabiashara, wakulima na askari wengi kuhamia mkoani humo kutoka sehemu za mashariki zenye maendeleo ya kiuchumi. Na wenyeji wa kijiji cha Tunbao walitoka Nanjing, mji mkuu wa Mkoa wa Jiangsu, mashariki ya China."

    Tulitembelea kijiji hicho kidogo, tuliona kwamba, nguo na vitu vya mapambo ya wanawake wengi wazee bado ilikuwa ya mitindo ya zamani kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya historia. Kwa mamia ya miaka iliyopita, wanaume wa kijiji cha Tunbao walikuwa na tabia ya kwenda nje kufanya biashara, ambapo wanawake kubaki nyumbani kushughulikia mambo ya kilimo. Ndiyo maana, nguo za wanawake hazikubadikika kufuatia zile za sehemu za nje. Hivi leo, wenyeji bado wanadumisha utamaduni na mila zao.

    Barabara safi inawapeleka watalii huko Tunbao na pia kuwasafirisha vijana wa huko hadi sehemu za nje. Vijana hawataki kubaki nyumbani tu, bali wanaondoka na kutafuta ajira na nafasi za masomo. Wanaporudi wanaleta mambo mapya. Wanavaa jeans na T-shirt, wanatumia simu za mikononi. Inasemekana kwamba, familia nyingi za kijiji hicho zimenunua television, VCD, na majiko ya microwave. Baadhi ya wanakijiji wana mitambo ya kupokea matangazo ya satlaiti, ambapo wanaweza kutazama vipindi mbalimbali vya television.

    Katika kijiji cha Tunbao, tulivutiwa na nyumba kadhaa za matofali ambazo kuta zake zimepambwa na vigae vyeupe vya kauri. Tuliambiwa kwamba, nyumba hizo ni makazi ya Bw. Zheng Mingxi, familia yenye watu 6.

    Mzee zheng ana umri wa miaka 72. alituambia kwamba, mwaka 1996 alipojenga nyumba aliona kuwa, ni za kisasa. Lakini hivi sasa anaona kuwa, nyumba zake haziambatani na mtindo wa kijiji hicho kongwe. Hivyo atazipamba upya mwaka huu.

    Mzee Zheng alifanya kazi katika sekta ya kilimo ya serikali. Baada ya ustaafu, alinunua aina nzuri ya miche ya mchele kutoka idara ya sayansi na teknolojia ya kilimo, na kuiotesha kwa njia za kisayansi, akapata mavuno mazuri na kupata pesa nying. Baadaye yeye na mwanaye mdogo walianzisha kituo cha kutoa huduma ya teknolojia ya kilimo, na kuwafundisha wenyeji wenzao aina nzuri za mbegu na kuwasaidia kutatua masuala ya kiteknolojia katiak uzalishaji wa kilimo.

    Bw. Zheng alieleza kuridhika na maisha ya hivi sasa. Aliona kuwa, hayo yametokana na sera mwafaka za Chama cha Kikomunisti, ambacho ni chama tawala nchini China. Alieleza imani yake kwamba, China itasonga mbele zaidi baada ya mkutano mkuu wa chama hicho mwezi Novemba, mwaka jana, kwani kutokana na historia, kila baada ya mkutano mkuu wa chama, taifa lilikuwa limepata maendeleo mapya.

    Ingawa Mzee Zheng ana umri wa zaidi ya miaka 72, lakini bado ni mzima sana. Kuhusu huduma ya afya katika kijiji hicho, alieleza kuwa hana wasiwasi wowote. Alisema "Hivi sasa, zipo zahanati kadhaa karibu na kijiji, hizo ni za watu binafsi na za serikali, ni rahisi kuwaonana na madakatari. Na hospitali pia haipo mbali. Maisha ya sasa yameboreshwa na tutaweza kuishi kwa miaka mingi zaidi."

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-10