
Picha zilizotengenezwa kwa matete ni vitu pekee vya sanaa vinavyotengenezwa na Kampuni ya Sanaa ya Danhe ya mji wa Daqing, jimboni Heilongjiang. Nyenzo zake ni matete asilia. Kwa kutumia rangi za asili za matete na sifa yake ya ugumu usiokatika kwa urahisi, wasanii wanatengeneza picha mbalimbali kwa usanifu bora na jia za kukata, kuunganisha, kupachika na kubandika. Picha hizi zenye mtindo mzuri zinaonyesha vitu mbalimbali kama vile maua, ndege, wadudu, samki na hata mambo ya binadamu, hususan wanyama wenye manyoya kwenye picha wanapendeza sana.
Picha za matete zina sifa za kudumu, kuzuia umajimaji, kujikinga na wadudu, kutobadilika kwa umbo wala kutofifia rangi. Katika Maonyesho ya Tatu ya Sanaa ya Taifa, picha za matete zilipata tuzo ya ngazi ya pili ya usanifu wa sanaa na tuzo ya ngazi ya kwanza ya vitu vya sanaa. Sansa, picha za matete zinauzwa hadi Marekani, Ujerumani na nchi na maeneo mengi ya Asia ya Mashariki kusini na zinapendwa sana na wateja wengi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-11
|