Kutokana na mwaliko wa wizara ya mawasiliano ya China, waziri wa barabara, miradi ya umma na nyumba wa Kenya Bw. Raila Odinga aliitembelea China kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 26 mwezi May mwaka huu. Katika ziara yake nchini China, Bw. Odinga na ujumbe wake walitembelea Beijing na Shanghai naibu waziri mkuu wa China Huang Ju alionana naye na pia alifanya mazungumzo na mawaziri wa mawasiliano na biashara wa China. Walibadilishana maoni kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika fani za ujenzi wa miundo mbinu ya mawasiliano, nyumba na nyinginezo.
Kabla hajaondoka mjini Beijing, Bw. Odinga alihojiwa na mwandishi wetu wa habari kuhusu ziara yake nchini China na mafanikio yaliyopatikana. Alipozungumzia lengo la ziara yake nchini China alisema,
"Nimekaribishwa vizuri sana hapa China na tumekuwa na ziara ya fanaka kuweza kuzungumza na wenzangu Waziri wa ujenzi vile vile nimezungumza na waziri wa mambo ya biashara. Pia tumeona miji na mji kama wa Shangai na miji mikubwa zaidi ya Shangai na tukaona ujenzi wa nyumba huko na vile vile mabarabara yalivyojengwa vizuri.Tumekuwa na mazungumzo mengi sana wakati tumekuwepo hapa na nimeridhika na matokeo ya ziara yangu.Tumetia saini mkataba baina ya serikali ya China na Kenya na hii inalenga uhusianao wa ujenzi wa mabarabara na miundo mbinu kwa ujumla ,dhidi ya hayo tutakuwa na mpango kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa mabarabara vile vile tutaweza kushirikiana katika upande wa elimu na upande wa sayansi tutafanya utafiti kwa ajili ya kuboresha hali ya mabarabara katika nchi yetu."
Bw. Odinga alifahamisha uhusiano mzuri wa ushirikiano kati ya China na Kenya katika sekta ya ujenzi wa barabara na miradi ya umma:
"Serikali ya China na ya Kenya imekuwa na uhusiano bora kwa miaka mingi,kwa upande wa mabarabara China imesaidia Kenya sana .Katika ujenzi China imeweza kutujengea barabara na mojawapo ni barabara ya kima road huko Kenya.Pia kuna nyingine inaitwa" keep tiger mahoho"hiyo imejengwa na Serikali ya China.Wakati huu sisi tunaendelea na ujenzi wa makampuni ya ohii na kuna kampuni nyingine za China ambazo zinafanya kazi kwamfano ile ya Guine road and brige company imefanya kazi nzuri sana kule Kenya kwani imeweza kujenga barabara nzuri sana kutoka Mombasa chuma get hadi mtitu wa ndei ambayo imejengwa kwa njia ya juu kabisa ambayo hivi sasa inatumika kama kiwango cha ubora wa ujenzi wa mabarabara katika Kenya nzima."
Kenya ni nchi inayopendeza sana, ina mandhari nzuri na hifadhi kubwa za wanyama, watu wengi wanapenda kwenda Kenya kufanya utalii, lakini huwa wanapata picha mbaya kutokana na barabara mbovu. Bw. Odinga alisema kuwa, serikali mpya ya Kenya iko mbioni kukarabati miundo mbinu ya mawasiliano ili kuwavuta watalii wengi zaidi:
"Ni ukweli hali ya mabarabara imekuwa mbaya na hii ni kwasababu ya usimamizi mbaya ambao ulikuwa chini ya serikali ya KANU ambayo ilikuwa imesahau ukarabati wa mabarabara .Kuna barbara ambazo zilikuwa zimejengwa lakini zikaachwa na kuzeeka maana walikuwa hawazibi nyufa na vile wahenga walisema "usupoziba ufa utajenga ukuta" hivyo kwa kweli hali ya mabarabra ni mbaya hivyo tumeweza kutathimini kwamba 43% ya barabara ambazo zilikuwa zimejengwa zimeharibika hivyo sasa zinatakiwa zijengwe upya.Pia tulianza mpango wa dharura kuona kwamba barabara ambazo zilijengwa zamani zifanyiwe ukarabati hivyo tunachangisha kutoka kwa wananchi pia kwa wasafirishaji wa mizigo wanaotumia barabara .Vile vile tumezungumza na wafadhili wengi ili kutusaidia sisi katika ujenzi wa barabara ambazo zilikuwa zimesahaulika ambazo tunaona ni muhimu kwa uchumi wa nchi yetu,haswa barabara ambazo zinatumika kwenda kwenye mbuga za wanyama ambazo watalii wengi huzitumia .Mambo hayo yote tunayapa kipaumbele na mpango huo unagarimu pesa nyingi ndio maana tunawaomba wafadhili wetu na marafiki waweze kutusaidia ili tuweze kuinua uchumi wetu."
Bw. Odinga alizikaribisha kampuni za China kwenda Kenya kuwekeza vitega uchumi. Alisema:
"Tumefurahi sana kuona kwamba China imekuwa na maendeleo zaidi kweli mambo yanayofanyika China yanapaswa kuigwa kwani yanastajabisha.Tumekuwa tukiwekewa vikwazo vingi na nchi kama Marekani na nchi za pande za magharibi lakini tofauti na hayo yote China imeweza kumudu na kufanya maendeleo haswa baada ya kuanza kufungua soko lake nchini mwetu.Kuna hatua nyingi ambazo China iwechukuwa maana mimi mwenyewe nimeenda Marekani ,nimeenda Marekani ya kusini nimezunguka bara lote la ulaya lakini sijaona mabarabara ambayo yamejengwa katika hali ya juu na hali ya kisasa kama yale ambayo nimeona Shangai hivyo nasema kuwa China imeendelea.China hivi sasa imeingia katika orodha ya nchi zilizoendelea na mfano wa China unaweza kuigwa na nchi nyingine ambazo sasa ziko katika harakati za kuboresha uchumi wao,mfano wa China ni mzuri sana kwa bara la Afrika kuliko mfano wa nchi za ulaya ambazo ziliendelea zamani zaidi ,hivyo mimi nimefurahi sana kwa ujio wangu nchini China."
Hii ni mara ya kwanza kwa Bw. Odinga kuitembelea China alivutiwa sana na alivyoona kwa macho yake mwenyewe:
"Sisi kama Wakenya kwanza tumejitahidi sana kuchukuwa hatua kuwavuta watu toka nje kuleta rasmali zao katika uchumi wetu wa Kenya na kuona kwamba ukileta rasmali yako utakuwa huru na kuweza kotoa hela yako wakati wowote na tumefungua soko letu liko wazi.Pia tumepigana na adui wetu "ufisadi"ambaye alikuwa mara nyingi anashtua wageni wengi katika nchi yetu tumejatibu kufagia kabisa soko letu ili wafanyakazi wa umma wasionekane kama wao wenyewe wanajaribu kupata pesa za bure kutoka kwa wageni nje."
Idhaa ya Kiswahili 2004-06-11
|