Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-06-15 19:41:16    
Maonyesho ya kimataifa ya magari ya Beijing mwaka 2004

cri
   Maonesho ya kimataifa ya magari mwaka 2004 Beijing, yalifunguliwa tarehe 10 mwezi juni. Kampuni karibu 1,900 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 20 zinashiriki kwenye maonesho hayo zikiona kuwa maonesho ya magari ya Beijing ni jukwaa bora kabisa la kuonesha magari yao na teknolojia yao mpya kabisa. Wafanya biashara wa kigeni wanasema kuwa soko la magari la China lina uwezo wa kuwa soko kubwa kabisa duniani katika siku za baadaye.

    Maonesho ya kimataifa ya magari mjini Beijing hufanyika kila baada ya miaka miwili, mwaka huu ni wa nane tangu maonesho hayo yaanze. Magari yanayooneshwa mwaka huu ni ya aina nyingi kuliko ya maonesho ya mika iliyopita. Kampuni mashuhuri za magari za nchini na za nchi za nje, zinayachukulia maonesho ya magari ya Beijing kuwa ni fursa muhimu ya kuonesha sura za kampuni zao na kuongeza ufahamu kuhusu magari yao kwa watazamaji.

    Eneo la maonesho ya magari ya safari hiyo limefikia mita za mraba laki 1.1 ambalo yanaoneshwa magari mengi ya kisasa na ramani za magari ya kisasa ambayo bado hayajatengenezwa ya kampuni mbalimbali zikiwemo Ford, General Motors na Audi. Kampuni ya magari ya Volvo ya Sweden ni maarufu sana katika bara la Ulaya ya kaskazini, inatia maanani sana maonesho ya magari ya mwaka huu. Mkurugenzi mkuu wa kanda ya China wa kampuni hiyo Bw. Wang Rong-xiang alisema kuwa kampuni ya Volvo toka mwaka huu imeinua kiwango cha maonesho ya magari yake sawa na maonesho ya magari yake katika sehemu nyingine duniani iwe kwa magari, teknolojia au banda la maonesho. Alisema,

    "Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni ya magari ya Volvo kuinua kiwango cha maonesho yake mjini Beijing kuwa ya kimataifa. Wasimamizi wote wa ngazi ya juu wa kampuni yetu wako hapa, maonesho yetu ni makubwa, majukwaa ya kuwekea magari pia tuliyasanifu sisi wenyewe, magari yetu zikiwemo ramani mpya za magari yanayotarajiwa kutengenezwa, yataoneshwa katika maonesho hayo katika siku za baadaye, maonesho ya magari yetu mjini Beijing yatakuwa maonesho ya kimataifa ya magari yetu."

    Habari zinasema kuwa baada ya kujiunga na WTO, sekta ya uzalishaji wa magari nchini China imeingia katika kipindi cha maendeleo ya kasi, ambapo soko la magari la China limekuwa soko lenye ongezeko na ushindani mkubwa duniani. Ili kupata nafasi katika soko la magari la China, wafanya biashara wakubwa wa uzalishaji wa magari duniani, licha ya kuonesha magari yanayowakilisha kiwango cha teknolojia yao, pia walionesha mipango yao kuhusu soko la magari la China. Kampuni ya magari ya Ford ilichagua maonesho ya magari mjini Beijing kuwa ni sehemu ya kwanza duniani ya kuuza aina mpya ya magari wanayotarajia kuyatengeneza yajulikanayo kwa jina la Focus, ambayo yatakuwa na kiwango cha kati na yatauuzwa zaidi katika sehemu ya Asia na Pasifiki. Kiongozi husika kutoka kampuni ya Ford alisema kuwa soko la China litakuwa soko muhimu kwake lenye ongezeko kubwa la mauzo ya magari ya matumizi ya familia, hivyo wamechagua China kuwa kituo chake muhimu zaidi cha uzalishaji wa magari ya aina Focus. Kampuni ya Ford na kampuni ya magari ya Changan ya China hivi karibuni zilijenga kwa ubia kiwanda cha uzalishaji wa mabasi, na hivi sasa zinanuia kujenga kituo cha pili cha uzalishaji katika sehemu ya mashariki ya China, hatua ambayo itapanua uwezo wake wa uzalishaji magari hadi kufikia magari laki 3 na eluf 50 kwa mwaka.

    Kampuni ya magari ya Mazda ya Japan katika maonesho ya hayo ilidokeza kuwa mauzo ya magari yao yatakuwa na ongezeko la 37% mwaka huu, yaani ongezeko la magari laki 1.1, na kufanya mauzo ya magari yao kufikia laki 3.3 nchini China utakapofika mwaka 2010. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya MAZDA Bw. Masazumi Wakayama alisema,

    "Mauzo ya magari ya MAZDA nchini China yamefikia kiwango cha mauzo yao katika masoko ya Ulaya na Latin America. Hivyo, soko la China limekuwa muhimu sana kwa kampuni ya MAZDA.

    Bw. Masazumi Wakayama anasema kuwa katika mwaka ujao, mauzo ya magari nchini China yataendelea kuwa makubwa. Naibu kiongozi wa umoja wa viwanda vya mitambo wa China, Bw. Zhang Xiaoyu anakubaliana na maoni hayo, alikadiria jumla ya uzalishaji wa magari nchini China, itakuwa na ongezeko la 50% mwaka huu. Alisema,

    Mwaka huu, kukuza mahitaji ya nchini na kupanua ununuzi wa bidhaa ni sera kuu za maendeleo ya uchumi wa China. Kupanua ununuzi wa magari kwa wakazi wa mijini ni lengo la kwanza la China mwaka huu. Hii ni mara ya kwanza kwa China kuweka ununuzi wa magari wa wakazi wa mijini katika nafasi ya kwanza ya kupanua ununuzi wa bidhaa. Endapo tutashikilia sera hizo, bila Shaka China itakuwa na ongezeko la kasi la uzalishaji wa magari."

    Habari zinasema kuwa idadi ya magari yaliyouzwa nchini China mwaka uliopita ilikuwa milioni 2 na elfu 40, ikiwa ni ongezeko la 80% kuliko mwaka uliotangulia. Baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa hadi mwaka 2005, idadi ya magari yatakayouzwa nchini China itakuwa kati ya milioni 4 na 5. kiwango hicho kinamaanisha kuwa China itakuwa soko la pili la magari kwa ukubwa dunia.

Idhaa ya Kiswahili 2004-06-15