Nitawatambuaje wenye UKIMWI (AIDS) ili nijiepushe nao?
Si rahisi kumtambua mtu mwenye UKIMWI kwa sababu dalili za ugonjwa zinahitilafiana kufuatana na ugonjwa uliomnyemelea baada ya kuburugika kwa baadhi ya silaha zake za kujihami. Kwa mfano mtu mwenye UKIMWI Baridi hataonyesha dalili zozote; na mtu mwenye UKIMWI Moto ambaye amenyemelewa na viini vya ugonjwa wa kifua ataonyesha dalili za magonjwa ya kifua kama vile kichomi, kukohoa, kutokwa na jasho usiku n.k.
Lakini kuna dalili fulanifulani ambazo mara kwa mara huonekana kwa wale wenye UKIMWI Moto au Vuguvugu. Baadhi ya dalili hizo ni:
1. Unyong'onyevu na uchovu usio na sababu maalum
2. Kuvimba tezi shingoni, kwapani na kinenani
3. Kukonda
4. Homa ya muda mrefu
5. Kuendesha endesha kwa muda mrefu
6. Utando mweupe kinywani, vidonda mdomoni, na vidonda kooni vyenye kusababisha maumivu wakati wa kumeza.
7. Ukurutu katika ngozi
8. Kuburugika akili
9. Kupungukiwa na damu.
Baadhi ya dalili kama hizo zinapoonekana kwa mtu ambaye haonyeshi kisa halisi cha ugonjwa unaozisababisha, basi anza kuwa mwangalifu zaidi kuhusu ushirikiano wa karibu sana naye ambao utaruhusu kugusana na vitu vitakavyokuwa vinamtoka?zaidi sana endapo mtu mwenye dalili hizo atakuwa ni yule aliye kwenye kundi la watu mashuhuri kwa ugonjwa huu.
Ni akina nani ambao wako kwenye hatari zaidi ya kukumbwa na UKIMWI?
Watu wafuatao ni maarufu kwa UKIMWI, yaani wana hatari zaidi kuliko wenzao ya kupatikana na ugonjwa huu:
1 Waasherati?yaani wenye kuruka mahali pengi hapa na pale badala ya kutulizana kwa uaminifu mahali pamoja.
2 Makahaba.
3 Wanaume wenye tabia ya kujuana kimwili na wanaume wenzao kwa njia ya tupu ya nyuma. Hawa ni mashuhuri kipindukia.
4 Wanaume au wanawake wenye kujuana kimwili na yeyote katika makundi matatu yaliyotajwa juu?iwe ni ndani au nje ya ndoa.
5 Wakazi katika eneo ambalo ugonjwa huu umetapakaa kwa wingi sana na ambao wamekuwa wakidumisha uhusiano wa karibu sana na watu walio kwenye makundi hayo manne yaliyotajwa.
6 Wenye kupewa (kusaidiwa) damu za watu wengine mara kwa mara.
7 Wenye mazoea ya kushirikiana kujidunga wenyewe sindano za madawa ya kulevya.
8 Watoto ambao mama zao wana UKIMWI, au mama zao ni maarufu kwa ugonjwa huu kama ilivyoorodheshwa.
Kwa nini waasherati, makahaba, n.k. wako kwenye hatari zaidi kuliko wenzao ya kupatikana na UKIMWI?
Kwa sababu ya kukaribiana kimwili na watu wengi tofauti kundi hili lina nafasi kubwa zaidi ya kubahatisha kuokota UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa kutoka kwa watu hao mbalimbali.
Pia kwa sababu ya kufanya zinaa mara kwa mara zaidi kuliko wenzao (au kufanya zinaa kwa mtindo iliyo tofauti na wenzao) kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa watu wa kundi hili kuchubuka katika via vyao vya uzazi pamoja na kuwa na vijeraha kutokana na magonjwa mengine ya zinaa. Vitu hivi (kuchubuka, vijeraha na utoko katika via vya uzazi) hufanya viiini vya UKIMWI vipate mteremko wa kupenya mwilini.
Idhaa ya Kiswahili 2004-06-17
|